Afya Ya Nyeti Za Mwanamme

 

afya ya nyeti za mwanamme

 

Afya Ya Sehemu Nyeti Za Mwanamme

 

Afya ya maungo ya uzazi au sehemu nyeti ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila mmoja wetu bila kujali umri ulio nao au tabaka lako katika jamii unayoishi. Ni kitu kikubwa sana na cha msingi katika maisha yako ya ndoa. Afya ya sehemu nyeti pia huongeza thamani ya maisha yako. Kwa kukosa afya bora, maisha yako  hupungua thamani na pengine kuwa chanzo cha matatizo mengine ya kiafya na hasa ya kisaikolojia. Kwa kuzingatia hayo basi, mambo tunayoyajadili hapa ni ya msingi sana katika kuboresha maisha yetu ya ndoa na kuyafanya maisha yetu kwa ujumla yawe na thamani.

 

Kuna matatizo mengi yanayoweza kumfanya mwanamme ashindwe kutekeleza tendo la ndoa kwa ufanisi.  Katika ukurasa huu, tutaorodhesha baadhi ya matatizo hayo na katika kurasa nyingine tutajadili kwa kina sababu za matatizo hayo, dalalili na namna ya kujitibu pale unapokuwa tayari umeathirika.

 

1. Kukosa Hamu Ya Kufanya tendo la ndoa

 

Mwanamme mwenye tatizo hili, hatajisikia kuvutiwa na jinsia tofauti na wala hatafikiria kufanya mapenzi. Tatizo hili la  kukosa hamu ya kufanya mapenzi (loss of libido), linaweza kusababishwa na mambo mengi kama utakavyoweza kusoma kwenye katika ukurasa tuliouandika mahsusi kwa somo hilo.

 

Jogoo Kushindwa Kuwika (Erectile Dysfunction)

 

Tatizo la jogoo kushindwa kuwika (Erectile Dysfunction) ni tatizo linalohusu kiungo cha mwanamme. Tatizo hili husababisha uume kushindwa kusimma kabaisa , au kusimama ukiw a legelege au pengine kuwa imara kwa muda mfupi sana, hali ambayo itamsababishia mwanamme huyu kushindwa kukamilisha tendo la ndoa.

 

3.  Kuwahi Kufika Kileleni (Premature Ejaculation)

 

Kuwahi kufika kileleni ni hali ya mwanamme kutoa manii muda mfupi sana baada ya kuanza kufanya tendo la ndoa au pengine kutoa manii hayo hata kabla ya uume kuingia kwenye uke.

 

 4. Kupinda Kwa Nyeti Ya Mwanamme (Peyronie’s Disease)

 

Hili ni tatizo la kupinda uume au kuwa kuwa mwembamba , mara nyingine hambatana na maumivu. Kuharibika kwa umbo la uume hutokea baada ya kuumia na hasa upande wa juu wa kiungo hiki. Baada ya kuumia , hutokea maumivu wakati uume ukisimama kwa kipindi kama cha miaka miwili hivi. Baadaye maumivu hupotea, lakini uume hubaki ukiwa umepinda.

 

 5. Uume Kusimama Kwa muda Mrefu Sana (Prolonged Erection-Priapism)

 

Mwanamme unapotokewa na hali ambapo uume unasimama kwa muda unaozidi saa nne, ujue moja kwa moja hilo ni tatizo. Yanafaa hatua za matibabu zichukuliwe mapema ili kuepuka madhara ya kudumu. Hali hii huweza kutokea baada ya mtu kufanya jitihada za kuponya tatizo la uume kutokusimama. Mara nyingine laweza kutokea baada ya kutumia viagra na hasa pale viagra inapotumika kwa kudunga sindano kwenye uume. Sababu nyingine ni matumizi ya cocaine au ugonjwa wa sickle cell.

 

 6. Maumivu Wakati Wa Kufanya Mapenzi

 

Tatizo hili lipo ingawa si sana kama ilivyo kwa akina dada na akina mama. Laweza kutokea kwa sababu ya kuwa na mchubuko, kuumia au ugonjwa wa ngozi.

 

Kwa maelezo zaidi na ya kina, tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au tutumie barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo:  0655 858027 au 0756 181651.

 

Your Name (required)/Jina Lako

Your Email (required)/Anuani Ya Barua Pepe

Subject/Andika Swali Au Maoni Yako

Enter the captcha code in the field below/Andika Herufi Unazoziona:captcha

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii