Virutubishi Vya Mwili – Nutrients

 

umuhimu wa virutibisho vya mwili

 

Umuhimu Wa Virutubishi Vya Mwili

 

Viumbe wote hai huhitaji chakula ili kuishi. Chakula huwapa binadamu nguvu ili waweze kufanya shughuli zao za kila siku, huwawezesha kujenga na kuikarabati miili yao,  na huwawezesha kupambana na maradhi mbalimbali. Ili mwili uweze kuyafanya yote hayo na kuwa na afya nzuri, inabidi upate chakula cha aina mbalimbali. Mada ya leo inahusu umuhimu wa virutubishi katika mwili wa binadamu ambapo tutavitaja virutubishi hivyo na kuelezea umuhimu wa kila kimoja.

 

 Kirutubishi  Cha Mwili Ni Nini?

 

Chakula tunachokula ndicho kinachoupatia mwili virutubishi au vitu vinavyotoa nguvu mwilini, kuusaidia mwili kukua, kupambana na maradhi n.k. Kusudi mwili upate virutubishi hivyo kutoka kwenye chakula tunachokula, chakula hicho lazima kivunjwevunjwe kwanza. Zoezi hilo linaanza kwa kukitafuna chakula mdomoni, kukimeza na kwisha kufika tumboni. Kikifika tumboni, chakula hicho huchanganyika na maji na vimimina vingine zikiwemo tindikali na kisha kitaelekea kwenye utumbo mdogo. Virutubishi hufyonzwa na kuingia kwenye mfumo wa damu kupitia kuta za utumbo mdogo na kusambazwa mwilini. Mabaki yasiyofaa mwilini huelekea kwenye utumbo mpana na kisha kutoka nje ya mwili.

Virutubishi hivyo ambavyo huchukuliwa na mwili vinaweza vikagawanywa katika makundi kuu sita:

1. Protini
2. Wanga
3. Mafuta (fats)
4. Madini
5. Vitamini
6. Maji

Protini:  Protini ni moja ya virutubishi vitatu vinavyohitajika kwa wingi katika mwili (macronutrients ), vingine vikiwa ni wanga na mafuta. Unapokula chakula chenye protini, huvunjwavunjwa na kuwa amino acids. Amino acids hutumika katika kujenga na kukarabati misuli ya mwili. Hii ni muhimu kwa watu wale ambao huwa na shughuli nzito au wanaofanya mazoezi. Sehemu zote za mwili zina misuli hivyo ni vizuri kupata chakula chenye protini ili kuirudishia kwenye hali yake. Protini vile vile husaidia katika kujenga kinga za mwili na afya ya ubongo. Vyanzo vikuu vya protini ni nyama, samaki, maziwa, siagi na mayai. Protini pia hupatikana kutokana na mimea; maharage, njegere zilizokaushwa, mbegu n.k.

Wanga: Chakula cha wanga hukupa nguvu  ili mwili uweze kufanya shughuli zake za kila siku vizuri. Glycogen ndani ya misuli ndicho kitu muhimu katika kukusaidia kuweka sawa kiwango cha nishati siku nzima. Chakula chenye wanga kikiliwa kongosho hutoa homoni iitwayo insulin. Insulin husaidia wanga uweze kuhifadhiwa kwenye misuli au kama mafuta. Wanga uliohifadhiwa ndani ya mwili huitwa glycogen. Glycogen iliyohifadhiwa ndicho chanzo cha nishati katika mwili wako. Wanga hutokana na mahindi,  ngano, shayiri, mchele na pia kutoka kwenye matunda na mboga.

Wanga hugawanywa katika makundi mawili: simple na complex. Wanga kutoka kwenye sukari ni simple carbohydrates na wanga kutoka kwenye nafaka ni complex carbohydrates. Wanga hutoa karibu kalori 4,000 kwa gramu na ndicho chanzo cha mwanzo cha nishati kwa misuli na ubongo.

Mafuta: Mafuta ni moja ya virutubishi vitatu vinavyohitajika kwa wingi na mwili, bila mafuta mwili hauwezi kuishi. Pamoja na kutoa kalori 9 kwa kila gramu, mafuta husaidia kuupa mwili joto wakati wa baridi. Mafuta pia hulainisha maungio ya mifupa. Mafuta hutunza baadhi ya vitamini kama A, D, E na K. Chakula cha aina ya nyama na maziwa kina uwingi wa saturated fats na mboga zina kiwango kikubwa cha unsaturated fats. Mafuta hutoa kalori mara mbili ya protini. Mafuta hutunza afya ya ngozi na nywele.

Vitamini Na Madini: Vitamini na madini ni muhimu kwa miili yetu kwani huusaidia mwili kufanya kazi zake vizuri na kuongeza kasi ya ufanyaji kazi wa kemikali ndani ya mwili. Madini ya calcium na magnesium ni muhimu kwa mifupa yetu na chuma (iron) kinahitajika katika chembechembe nyekundu za damu ili kusafirisha oksijeni.

Kuna vitamini 13, ikiwa ni pamoja na vitamin A,B complex, C, D, E na F. Kwa sababu vitamini nyingi hazitengenezwi na miili yetu, zinatakiwa zipatikane kutoka kwenye chakula.

Pamoja na kwamba ni vitu muhimu, vitamini na madini huhitajika kwa kiwango kidogo. Vitamini na madini hupatikana katika chakula tunachokula, lakini kwa kawaida mahitaji ya mwili ya vitamini na madini ili uwe na afya huwa ni makubwa kuliko kiwango kinachopatikana kwa kula chakula.

Maji: Maji hujenga asilimia 65 ya mwili wa binadamu. Ni lazima mwili uwe na maji ili mwanadamu aweze kuishi. Maji yana kazi ya kusafirisha virutubishi kwenda kwenye seli na kutoa vitu visivyohitajika kutoka kwenye seli. Inashauriwa mtu anywe glasi 8 za vimiminika kwa siku, ambavyo vinaweza kuwa ni maji matupu, juisi, maziwa , supu au chakula chenye maji kwa kwa wingi kama mboga na matunda. Maji hutoa sumu na kuusafisha mwili. Wakati wa kufanya mazoezi, maji hufanya kazi ya kuupoza mwili.

 

Mlo Kamili (Balanced Diet)

 

Mlo kamili (balanced diet) ni mlo ulio na virutubishi vinavyohitajika na mwili ili uweze kufanya kazi ipasavyo. Ili kupata virutubishi vinavyotakiwa kutoka kwenye mlo, unahitaji upate kalori nyingi kutoka:

. kwenye matunda
. mboga
. nafaka nzima
. jamii ya kunde
. njugu
. nyama isiyo na mafuta

 

Kalori Ni Nini?

 

Kiwango cha kalori katika chakula ni kipimo cha nishati iliyohifadhiwa ndani yake. Mwili hutumia kalori kutoka katika chakula ili kukuwezesha kutembea, kufikiri, kupumua, na kufanya shughuli nyingine muhimu. Mtu wa kawaida anahitaji kiasi cha kalori 2,000 kila siku ili kuwa na uzito wa kawaida.

Lakini kiwango cha kalori kwa siku kwa mtu kinatofautiana kulingana na umri, jinsia, na uzito wa kazi zake. Kwa kawaida, wanaume huhitaji kalori nyingi kuliko wanawake, na watu wa mazoezi huhitaji kalori nyingi kuliko wale wasiofanya mazoezi.

Chanzo cha kalori katika mlo wako ni muhimu kama kilivyo kiwango cha kalaori. Inashauriwa kupunguza matumizi ya kalori tupu (empty calories), au zile ambazo hazina au zenye thamani ndogo ndogo ya lishe. Kalori tupu ni zile zinazotokana na sukari na mafuta ya kuganda, kama siagi.

 

chati ya kalori
Baadhi ya chakula chenye kalori tupu ni:

. bacon
. soseji
. keki
. jibini
. vinywaji vya kuongeza nguvu (energy drinks)
. vinywaji vya matunda
. ice cream
. pizza
. soda

 

Kwa Nini Mlo Kamili Ni Muhimu

 

Mlo kamili ni muhimu kwa sababau viungo vya mwili na tishu vinahitaji lishe inayotakiwa ili kufanya kazi vizuri. Madhara ya kukosa lishe bora ni magonjwa, maambukizi ya wadudu, uchovu, udhaifu wa mwili. Watoto wanaokosa lishe bora hupata matatizo ya kukua na kufanya vibaya katika masomo. Ulaji mbaya huweza kuendelezwa maisha yao yote.

Magonjwa yafuatayo yanahusishwa na ulaji mbaya wa chakula:

. magonjwa ya moyo
. saratani
. kiharusi
. kisukari

 

Namna Ya Kupata Mlo Kamili

 

Siri ya kupata mlo kamili ni kula chakula chenye mafuta na sukari kwa kiwango kidogo na chenye uwingi wa vitamini, madini na virutubishi vingine.

 

mlo kamili

 

Chakula kifuatacho ni muhimu katika mlo wako; matunda, mboga za majani, nafaka, protini, maziwa na mafuta yasiganda.

 

 Virutubishi Vya Mwili Vya Kiada (Nutritional Supplements)

 

Green World super nutrition

 

 

Mara nyingi mwili unahitaji kupata virutubishi vya kiada (siyo tafsiri rasmi), yaani virutubishi vilivyotengenezwa na kuliwa kama chakula. Mara nyingi vitu hivi huwa ni vitamini, madini n.k. na vinasaidia kuziba mapengo yaliyoachwa na ulaji wa chakula kinacholimwa au kuandaliwa kwa njia za kisasa.  Virutubishi hivi husaidia kuboresha afya kwa ujumla, husaidia kujenga kinga ya mwili, husaidia ufanisi wa wanariadha na wanaojenga miili yao (body builders), husaidia kupambana na hali ya mwili kuzeeka na pia husaidia mwili kupona haraka unapokuwa umepatwa na magonjwa.

Kuna makampuni mengi yanayojihusisha na utengenezaji wa virutubishi vya kiada na ni biashara kubwa sana katika nchi zilizoendelea.

Kutokana na maendeleo makubwa sana katika sayansi na teknolojia yaliyofikiwa katika karne moja iliyopita, matumizi ya virutubishi vya kiada hayakwepeki. Ili kuona umuhimu wa kutumia virutubishi hivyo, unaweza kusoma mada hiyo kwenye kwenye wa “Kwa nini utumie virutubishi vya Green world?“.

 

uchafuzi wa hewa kwenye mazingira

 

Unaweza kusoma kuhusu baadhi ya kampuni zinazofanya biashara ya virutubishi kwenye kurasa za “Kirutubishi cha TREVO” na “Kampuni ya kuuza dawa ya Green world“.

Usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu mada yetu ya leo. Ni furaha kwetu kuwa nawe.

 

Kwa maelezo zaidi na ya kina, tuma ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au tutumie barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni

 

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii