Maumivu Kabla Ya Hedhi (Premenstrual Syndrome – PMS)

 

maumivu ya hedhi

 

Katika mfululizo wa mada zetu za leo, tutazungumziia matatizo yanayoambana na hedhi. Wanawake wengi hupata matatizo kabla ya kuanza hedhi, wakati wa hedhi na mara ya baada ya kukoma hedhi. Nafikiri ni wakati muafaka wa kulizungumzia pia tatizo la kukosa kabisa hedhi. Katika kila moja ya hayo, tutajaribu kuona sababau za tatizo na jinsi ya kuepuka tatizo hilo.

Tunaanza kwa kulitazama tatizo la kupata maumivu kabla ya hedhi (Premenstrual syndrome). Premenstrual syndrome ni hali ambayo humwathiri mwanamke kihisia, afya yake aya mwili na tabia yake katika kipindi fulani cha mzunguko wake wa hedhi, kwa kawaida kabla tu ya kuingia mwezini. Tatizo hili ni la kawaida kwa wanawake na huathiri karibu asilimia 85 ya wanawake wanaopata hedhi. Maumivu huanza siku 5 hadi 11 kabla ya kuanza hedhi.

Kuna mlolongo wa dalili za tatizo hili la maunmivu kabla ya hedhi, lakini mwanamke anaweza kupata baadhi ya dalili zifuatazo:

 

Dalili Za Kihisia Na Kitabia

 

shida za hedhi

 

. Kuwa na msongo wa mawazo au wasiwasi
. Kuwa na mfadhaiko
. Kulialia
. Madadiliko ya mara kwa mara ya kihisia na hasira
. Mabadiliko ya ulaji na kupenda sana kula
. Matatizo ya kupata usingizi
. Kujitenga na jamii
. Kushindwa kutuliza mawazo

 

Dalili Na Mabadiliko Katika Maumbile ya Mwili

 

. Maumivu kwenye maungio ya mifupa na misuli
. Kuumwa kichwa
. Uchovu
. Kunenepa
. Maumivu kwa mbali maziwa yakiguswa
. Kuchipuka kwa chunusi
. Kukosa choo au kuharisha

Kwa baadhi ya wanawake, madadiliko haya ya kitabia na maumivu ya mwili yanaweza kuwa makubwa kiasi cha kuathiri shuguli zao. Pamoja na kuwa wengine huathirika sana, matatizo haya huisha ndani ya siku nne baada ya kuanza hedhi.

Kwa wanawake wachache, maumivu haya ya kabla ya hedhi huwafanya washindwe kabisa kuendelea na shughuli zao za kila siku, na huwatokea kila mwezi. Aina hii ya PMS huitwa premenstrual dysphoric disorder (PMDD).

Dalili za premenstrual dysphoric disorder ni pamoja na mfadhaiko, hisia za ghafla zinazobadilika, hasira, wasiwasi, kushindwa kufikiri, hasira za ghafla na kuwa na msongo wa mawazo.

 

Chanzo Cha Maumivu Ya Kabla Ya Hedhi – Premenstrual Syndrome

 

Chanzo kamili cha tatizo la kupata maumivu kabla ya hedhi hakijathibitika, lakini sababu zifuatazo zimeonyesha kuwa na mchango mkubwa:

. Mabadiliko Katika Mzunguko Wa Homoni. Dalili za maumivu kabla ya hedhi zinabadilika na mabadiliko ya homoni katika mzunguko wa hedhi. Viwango vya homoni ya estrogen na progesterone huongezeka wakati fulani katika mwezi. Mwongezeko huu husababisha mabadiliko ya mara kwa mara ya namna mwanamke atakavyojisikia, kuleta wasiwasi na kusababisha hasira za haraka.

. Mabadiliko ya viwango vya kemikali katika ubongo. Mabadiliko katika viwango vya serotinin katika ubongo vinaaminika kusababisha premenstrual syndrome. Viwango vya Serotinin huathiri namna mwanamke atakavyojisikia. Serotinin ni kemikali katika ubongo inayoamsha namna ya kujisikia, hisia na mawazo. Kuwa na kiwango kidogo cha serotinin kunasababisha mfadahiko, uchovu, kupenda kula sana na kukosa usingizi.

. Mfadhaiko. Wanawake wengine waliobanika kuwa na matatizo mazito ya maumivu kabla ya hedhi, walikuwa na mfadhaiko, ingawa mfadhaiko huo haukuwa sababu ya matatizo yao yote.

 

Mambo Ya Kufanya Kupunguza Maumivu Ya Kabla Ya Hedhi

 

Unaweza kuondokana na au kupunguza makali ya tatizo la maumivu kabla ya hedhi kwa kufanya mabadiliko katika namna ya kula, kufanya mazoezi na namna unavyoishi kwa ujumla. Unaweza kujaribu yafuatayo:

Badili Namna Ya Kula

. Punguza mlo, kula mara nyingi zaidi kuzuia tumbo kuvimba na hali ya kujisikia tumbo limejaa

. Punguza chumvi na chakula chenye chumvi nyingi kuzuia tumbo kujaa
. Chagua chakula chenye complex carbohydrates, kama matunda, mboga za majani na nafaka nzima

. Chagua chakula chenye uwingi wa calcium
. Jizuie kutumia kahawa na pombe

Jipangie Ratiba Ya Mazoezi Ya Mwili

Panga ratiba ya kutembea angalau kwa dakika 30, kuendesha baiskeli, kuogelea au mazoezi mengine ya kukutoa jasho siku kadhaa kwa wiki. Mazoezi ya kila  siku yataboresha afya yako na kukuondolea baadhi ya dalili, kama uchovu na mfadhaiko.

Punguza Msongo Wa Mawazo

. Pata usingizi wa kutosha
. Fanya mazoezi ya misuli au upumuaji mzito ili kuondoa maumivu ya kichwa, wasiwasi na matatizo ya kukosa usingizi
. Jaribu kufanya yoga au massage ili kuondoa msongo wa mawazo.

 

Tiba Ya Maumivu Kabla Ya Hedhi

 

Kwa wanawake walio wengi, kubadli mtindo wa maisha kumweza kuwasaidia kuondokana na PMS. Kulingana na ukubwa wa tatizo, daktari anaweza kukuandikia dawa moja au zaidi ya dawa za kusaidia PMS. Utendaji kazi na msaada wa dawa hizi hutofautiana kutoka mwanamke mmoja hadi mwingine. Dawa ambazo hutolewa ni pamoja na:

. Antidepressants
. Nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs)
. Diuretics.

Tiba Mbadala Ya Maumivu Kabla Ya Hedhi

Kuna vitu vinafahamika kuondoa au kupunguza makali ya tatizo la maumivu kabla ya hadhi:

. Calcium. Kupata calcium ya kutosha katika mlo au matumizi ya vidonge vya calcium kunaweza kuondoa dalili za maumivu kabla ya hedhi – premenstrual syndrome.

 

Calcium Capsule

Bofya Juu Ya Picha Kusoma Maelezo

 

. Magnesium. Kutumia magnesium kila siku kutasaidia kuondoa maumivu ya kwenye maziwa na kujaa kwa tumbo kunakoambatana na premenstrual syndrome.

. Vitamin E. Matumizi ya vitamini E ya kila siku yanaweza kuondoa PMS kwa kuzuia utengenezaji wa prostaglandins, namna ya homoni inayosababisha mkakamao wa misuli na maumivu kwenye maziwa.

. Tiba ya mimea. Baadhi ya wanawake wameeleza kupata nafuu ya PMS kwa kutumia mimea kama ginkgo, tangawizi, chasteberry na mingine ingawa njia hii haijathibitishwa na vyombo vya kusimamia chakula na dawa.

Katika ukurasa unaofuata, tutazungumzia tatizo la maumivu wakati wa hedhi (Dysmenorrhea). Katika kurasa za mbele tutazungumzia tatizo la kukosa hedhi (Amenorrhea) na matatizo baada ya kukoma hedhi (Menopausal syndrome).

Tunaomba mchango wako wa mawazo kuhusu mada hii, na usisite kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu tatizo la kupata maumivu kabla ya hedhi (PMS).

Laurian.

 

 

1               2                3                     4

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii