Punguza Unene

punguza uzito

 

Zipi Ni Njia Sahihi Za Kupunguza Uzito?

Watu wengi sana wanatafuta njia za kuweza kupunguza uzito wa miili yao au kwa maneno mengine, watu wengi wanene hutumia njia mbalimbali ili wawe wembamba. Kutokana na hilo, watu wengi wanajitokeza na kujipatia fedha kwa kudai kuwasaidia watu hao katika kupunguza uzito wa miili yao. Kwetu hapa Tanzania, njia zinazotumika ni dawa za asili (hapa namaanisha dawa zilizotengenezwa hapa hapa kienyeji au mitishamba) na dawa zilizoletwa na makampuni mbalimbali ya nje ya nchi, zikiwemo za asili na za kemikali. Kila mmoja aliyetumia dawa hizo amekuwa na maoni tofauti, wapo walioridhika na matokeo na wapo ambao waliona dawa hizo hazikuwafaa.

Katika kutumia dawa hizo yapo mambo ambayo yanapaswa kutazamwa, si tu kupungua au kutopungua uzito bali na matokeo mengine ambayo yanasababishwa na matumizi ya dawa hizo (side effects). Najua hakuna aliyechukua hatua ya kufanya utafiti huo, lakini kitu cho chote unachotumia huwa na matokeo mengine mengi ambayo hayakuwa yamekusudiwa.

Tatizo la kupunguza uzito si la hapa kwetu tu, ni la ulimwengu mzima. Sasa jee, wenzetu wenye utaalamu zaidi wanasemaje kuhusu hili?

Njia Sahihi Za Kupunguza Uzito

Pamoja na kwamba kuna mambo mengi yanayotajwa na kutumika kama njia za kupunguza uzito, kiutaalamu yote yanalenga kupunguza mafuta (fat) mwilini. Hivyo basi njia sahihi za kupunguza uzito huo ni mbili. Ya kwanza ni kuwa na mpango maalumu kuhusu chakula na namna unavyokula na ya pili ni kufanya mazoezi ili kupunguza mafuta yaliyojazana chini ya ngozi (adipose tissues) na kwenye maeneo mengine ya mwili. Katika kufanya hayo yote, inabidi kuwa na malengo katika kupunguza uzito wako. Kuna kiwango cha chini cha uzito ambacho kila mtu inafaa awe nacho kulingana na umri, jinsia  na urefu alio nao. Kupunguza uzito chini ya kiwango hicho kunaweza kuleta matatizo mengine ya afya baadaye. Inafaa basi kabla ya yote kujua unataka kupunguza uzito kwa kiasi gani. Sasa tutazame kila moja ya njia hizo hapo juu za kupunguza uzito.

Mpango Wa Chakula Na Namna Ya Kula

Kusudi mwili uwe na nguvu, kila wakati unahitaji kuvunjavunja na kuunguza mafuta yaliyomo mwilini. Endapo mwili utagundua hakuna chakula tumboni, utaacha kuunguza mafuta na badala yake utaanza kuvunjavunja misuli ya mwili. Imethibitishwa kwamba watu wanaokula milo mitatu kwa siku wanapunguza uzito wa miili yao haraka zaidi ya wale wanaopata milo pungufu. Hii ina maana gani? Maana yake ni kwamba siyo sahihi kufikiri kuwa unaweza kupunguza uzito kwa kupunguza kula. Kupunguza uzito kwa njia inayofaa ni kula milo yote ya kawaida na chakula cha aina fulani na kamwe si kwa kuruka milo.

 

panga namna ya kula

 

Chakula Cha Kupunguza Uzito

Kusudi kupunguza uzito, mwili unahitaji milo iliyokamilika. Milo hiyo iwe na chakula cha makundi yote yaani protini (protein), wanga (carbohydrates) na matunda. Kitu cha kuzingatia ni uwiano wa chakula hicho katika mlo mmoja. Kufanya yafuatayo kutasaidia kupunguza uzito wa mwili wako:

1. Kula chakula chenye kalori ndogo kwa wingi. Hapa ina maana inakupasa kula matunda na mboga kwa wingi zaidi ili kulifanya tumbo lako lijae. Waweza kutengeneza mlo wako ukawa hadi asilimia 50% kuwa ni mbogamboga tu.

2. Tumia zaidi nafaka nzima kuliko chakula cha wanga kilichosagwa

3. Tumia mafuta kidogo ya kupikia

4. Jenga tabia ya kula nyumbani na si hotelini. Kula hotelini kunasababisha ule zaidi ya kipimo na kuna tatizo jingile la kutokujua chakula hicho kiliandaliwa kwa kutumia viungo gani na kwa vipimo vipi.

5. Kunywa maji mara nyingi kwa siku. Kwa mwanamme kunywa maji hadi lita 3 kwa siku na mwanamke lita 2 kwa siku. Maji yana faida nyingi sana mwilini, lakini pia hujaza sehemu fulani ya tumbo na ni kitu kisicho na kalori kabisa. Maji baridi yanafaa zaidi kusudi mwili utumie kalori kuyapasha hadi kufikia joto la mwili. Ukijijengea tabia ya kunywa maji nusu lita, nusu saa kabla ya kula chakula itakusaidia sana, hasa kama una umri mkubwa.

Mazoezi Ili Kuunguza Kalori

Jiwekee mpango wako mzuri wa kufanya mazoezi. Ikiwa ulikuwa hufanyi mazoezi kabisa, anza taratibu kwa mazoezi ya nusu saa, mara tatu kwa wiki na kuongeza muda taratibu. Unaweza kuanza kwa kuzunguka hapo nyumbani tu kwanza.

Ukiweza kwenda kufanya mazoezi gym chini ya watu waliofunzwa itakuwa bora zaidi. Mazoezi mengine unayoweza kufanya ni kama yoga, karate, kickboxing n.k. Unaweza kujiunga na michezo kama mpira wa miguu, volleyball, tennis, haya yote yatakusaidia zaidi.

Mazoezi Ya Kupunguza Mwili Na Tumbo

Hapa chini nitaonyesha video mbili ambazo zitaweza kukusaidia kufanya mazoezi ya kupunguza mwili.  Angalia video hizo kisha changua moja ya kuanza nayo, hakikisha unajiwekea mpango mzuri wa kufanya mazoezi haya. Video ya kwanza ni ya dakika kama 8 yenye lengo la kupunguza vyote, mwili na mafuta ya tumbo. Bonyeza juu ya picha hii hapa chini kuangalia video hiyo:

 

 

Video ya pili ni fupi zaidi, kama dakika tano tu na inalenga zaidi katika kuunguza mafuta ya tumbo. Angalia video hiyo kwa kubonyeza juu ya picha hii hapa chini:

 

 

Unaweza kuchagua video nyingine ambazo utaona zinakufaa zaidi kwa kuingia kwenye mtandao. Hapa niliweka mbili ambazo mimi nilizipenda na ambazo nazitumia.

Katika ukurasa mwingine nimezungumzia matumbo makubwa au vitambi na namna ya kuondoa matumbo hayo makubwa au vitambi hivyo.

Ndugu msomaji kwa kusoma hadi hapa chini inaonyesha unaguswa na mada hii, hivyo usisite kutoa mchango ulio nao kuhusu mada hii au kuuuliza maswali.  Nitafurahi sana kusikia kutoka kwako.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

 

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii