Fibroids Ni Kitu Gani? Ni Nini Tiba Ya Fibroids?

 

 

tiba za fibroid

 

Fibroids Ni Kitu Gani? Ni Nini Tiba Ya Fibroids?

 

Fibroids ni uvimbe wa misuli laini wenye mizizi ya kuiunganisha unaoota na kukua kwenye uterus. Majina mengine ya uvimbe huu ni uterine fibroids, myomas, au fibromyomas. Fibroids ni aina ya uvimbe unaoonekana kwa wingi zaidi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Fibroids ni uvimbe ambao mara nyingi (asilimia 99) hauna madhara kiafya na wala kuhusiana na ugonjwa wa kansa.

aina ya fibroids

Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 20 hadi 50 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa, miaka 30 hadi 50, wana fibroids ingawa wengi wao hawahangaiki kuchukua vipimo vya fibroids. Uvimbe wa fibroids unakuwa na ukubwa tofauti tofauti, unaweza kuwa mdogo kama haragwe au kufikia ukubwa wa tikiti maji.

 

Chanzo Cha Fibroids

 

Sababu hasa za kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri ingawa inaamika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya musuli wa uterus ambayo imeamua kuwa na tabia ya tofauti na nyingine na ikaanza kukua kwa haraka ikichangiwa na uwepo wa homoni ya estrogen.

Wanawake wanaokaribia kufikia ukomo wa kupata siku zao za mwezi wanaonekana kuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata fibroids kwa sababu ya kuwa wameishi na homoni ya estrogen kwa muda mrefu zaidi. Wanawake wenye asili ya mchanganyiko wa wamarekani na waafrika (wamarekani weusi) nao wanaonekana kupatwa na fibroids zaidi ya wanawake wengine ingawa sababu bado haijajulikana.

daili za fibroids

Utafiti umeonyesha pia kuwa idadi ya wanawake wanaopatwa na fibroids katika kundi la wanawake ambao wamezaa watoto angalau wawili wakiwa hai huwa ni nusu ukilinganisha na wale ambao hawajazaa hata mara moja. Hapa haieleweki kama kuzaa kulizuia wanawake hawa wasipate fibroids au fibroids ndizo zilizozuia wanawake wa kundi la pili wasizae. Utafiti kuhusu hilli bado unaendelea.

 

Dalili Za Fibroids

 

Akina mama wengine wenye uvimbe wa fibroids huwa hawaoni dalili zo zote zile (wengi hawajui kama wana fibroids) au kuona dalili kidogo na kwa wengine dalili hizi hujitokeza sana na kuwasumbua hadi kufikia kutafuta tiba. Baadhi ya dalili za fibroids ni:

– Kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku au kutokwa na damu        kwa muda mrefu

– Kutokawa na damu kusiko kwa kawaida katikati ya siku za mwezi

– Mauvimu ya nyonga (uvimbe kugandamiza kwenye viungo vya             nyonga)

– Kupata haja ndogo mara kwa mara

– Maumivu ya mgongo

– Maumivu wakati wa tendo la ndoa

– Upungufu wa damu kwa sababu ya kutokwa na damu kwa wingi            wakati wa siku

– Maumivu ya kichwa

– Maumivu kwenye miguu

– Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo (Fibroids kubwa)

– Uzazi wa shida

– Mimba za shida

– Kutopata mimba

– Kutoka kwa mimba mara kwa mara

 

Aina Ya Fibroids

 

Kuna aina nne za Fibroids

  • Intramural: Fibroids aina hii hukua kwenye kuta za uterus. Hii ndiyo aina ya fibroids inayowapata wanawake wengi.
  • Subserosal fibroids: Fibroids aina hii hukua nje ya kuta za uterus na huweza kuwa na shina. Subserosal fibroids huweza kukua na kuwa kubwa sana.
  • Submucosal fibroids: Fibrioids aina hii huota na kukua kwenye         misuli chini ya ngozi laini ya kuta za uterus.
  • Cervical fibroids: Fibroids aina hii hujenga kwenye shingo ya tumbo la uzazi (Cervix).

 

Fibroid ni nini

 

Tiba Ya Fibroids

 

Kama mwanamke hapati usumbufu wa namna yo yote katika shughuli zake za kawaida, anaweza asipewe tiba ya aina yo yote hata kama imegundulika kuwa ana uvimbe wa fibroid kwa sababu mwanamke anapokaribia kukoma hedhi fibroids hunyauka zenyewe na mara nyingine kutoweka kabisa.

Endapo tiba imekuwa ni ya lazima, anaweza kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji kutokana na hali iliyopo.

 

Tiba Ya Fibroids Kwa Kutumia Dawa

 

Tiba kubwa ya fibroids ni kwa kutumia dawa aina ya GnRHA (gonadotropin released hormone agonist) ambayo hutolewa kama sindano. Dawa hii huufanya mwili wa mwanamke upunguze utengenezaji wa estrogen hivyo kusababisha fibroids kunyauka.

Tiba nyingine ni Tranexamic acid, vidonge vya kuzuia maumivu, vidonge vya kuzuia mimba (kuzuia mwanamke asipate siku) na LNG-IUS (Levonorgestrel intrauterine system) ambacho ni kifaaa cha plastiki kinachowekwa kwenye uterus.

 

 

Tiba Ya Fibroids Kwa Upasuaji

 

Kama dawa zimeshindwa kufanya kazi, mgonjwa hufanyiwa upasuaji kwa moja ya njia zifuatazo:

Hysterectomy– Kuondoa uterus. Hii hufanywa pale fibroids zinapokuwa kubwa sana au pale ambapo mgonjwa anatokwa na damu nyingi sana. Upasuaji huu una madhara ya aina mbili: 1. Kupunguza hamu ya kufanya mapenzi 2. Kukoma hedhi mapema

Myomectomy– Fibroids kuondolewa kutoka wenye ukuta wa uterus. Hii hufanyika pale ambapo mgonjwa anapenda kuendelea kuzaa. Tiba hii haoifanywi kwa fibroids kubwa au zile ambazo kwenye maeneo nyeti ya uterus.

tiba ya fibroids

Endometrial ablation: Kuondoa wa ngozi laini ya ndani ya uterus.

UAE (Uterine Artery Embolization): Hii ni kuzuia fibroids zisipate damu na hivyo kunyauka. UAE hufanywa kwa fibroids kubwa.

Magnetic-resonance-guided percutaneous laser ablation: Sindano nyembamba hupenyezwa kupitia ngozi hadi kulifikia fibroid. Fibroid humulikwa na mionzi ya laser kupitia waya fiber-optic uliopitishwa kwenye sindano na kulinyausha Fibroid.

Magnetic-resonance-guided focused ultrasound surgery: Kifaa maalumu hutumika kugundua eneo la fibroid, kisha mawimbi ya sauti huelekezwa kwenye fibroid. Mawimbi hayo hulinyausha fibroid.

 

Katika mada ya leo tumeona fibroids ni nini, chanzo cha fibroids, dalili zake, aina za fibroids na tiba zinazotumika kuondoa fibroids. Mategemeo yetu ni kwamba umeielewa vizuri mada hii, lakini endapo bado una swali lo lote kuhusu somo letu la leo, usisite kutuuliza. Katika mada nyingine tutazungumzia tatizo la mwanamke kutoa uchafu ukeni.

 

Una Tatizo la Fibroids?

 

Kwa maelezo zaidi na ya kina au kupata msaada, tuma ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au tutumie barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

 

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Namba Yako Ya Simu

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni Yako

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii