Ujue Ugonjwa Wa Homa Ya Ini (Hepatitis)

 

homa ya manjano

 

Homa ya ini (hepatitis) ni neno linalotumika kujumuisha magonjwa yanayoleta madhara kwenye ini kwa kushambulia na kuzidhuru seli za ini. Ugonjwa huu unaweza kupona wenyewe bila kuleta madhara makubwa au unaweza kuwa mkubwa kiasi cha kuacha makovu kwenye maini. Mara nyingi ugonjwa huu ukiwa mkubwa utamsumbua mgonjwa kwa kipindi kinachoweza kufikia hadi miezi sita. Ni ugonjwa unaoweza pia kuwa wa muda mrefu zaidi (chronic).

Kuna aina kuu 5 za ugonjwa huu na aina hizi zote huletwa na virusi. Karibu watu milioni 250 duniani wanashambuliwa na hepatitis C wakati watu wapatao milioni 300 ni wale wanaoweza kueneza ugonjwa wa hepatitis B bila wao wenyewe kudhurika (hepatitis B carriers). Aina nyingine za ugonjwa huu ni hepatitis A, D na E. Uharibifu mwingi wa maini ya binadamu hutokana na aina tatu za virusi wa hepatitis, hepatitis A, B na C.

Hepatitis ambayo haitokani na virusi huitwa hepatis X. Kuna aina ya ugonjwa wa homa ya ini unaotokana na kirusi wa aina ya kipekee kabisa (HGV) nayo huitwa hepatitis G.

Kuna aina nyingi za hepatitis ambazo haziambukizi. Unywaji wa pombe, utumiaji wa madawa na kemikali vyaweza kuleta uharibifu kwenye maini. Mtu pia anaweza kupata maradhi haya kwa kuzaliwa kwenye ukoo wenye historia ya maradhi haya, kutokana na hitilafu katika utendaji kazi wa mwili au kutokana na kuharibika kwa kinga zake za mwili. Ulafi waweza kuwa chanzo cha madhara kwenye ini. Homa za ini kutokana na vitu hivi haziambukizi kutoka mtu mmoja hadi kwa mwingine.

 

Kazi Za ini

 

Ini ni kiungo kikubwa kuliko kingine cho chote kile kilicho ndani ya mwili wa binadamu. Ini hujengwa kwa nyama na hukaa upande wa kulia wa tumbo.  Kazi kuu ya ini ni kuchuja damu kutoka kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kabla ya kuisambaza kuelekea sehemu nyingine za mwili.  Ini huwa na uzito upatao kilo 1.36. Ini limegawanyika katika vipande vinne vyenye ukubwa na urefu tofauti. Damu hulifikia ini kupitia hepatic artery na potal vein. Hepatic artery huchukua damu yenye oksijeni kwa wingi kutoka aorta na kuifikisha ndani ya ini.

 

kazi za ini

 

Ini linafanya kazi nyingi sana katika mwili wa binadamu, ikiwa ni pamoja na:

. Kuondoa sumu – ini huchuja vitu vyote vyenye madhara kutoka kwenye damu, kama pombe

. Kuhifadhi vitamini A, D, K na B12.

. Utengenezaji wa protini – hutengeneza baadhi ya amino acids vitu vinavyojenga protini

. Kutoa kemikali za kusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, kama nyongo ambayo humiminwa kwenye utumbo

. Kusaidia kuweka sawa kiwango cha sukari mwilini

. Kutengeneza cholesterol (asilimia 80 ya cholesterol hutengenezwa na ini)

. Kutunza glycogen (pia kubalisha glucose kuwa glycogen)

. Kuvunja chembe chembe nyekundu za damu

. Kutengengeneza plasma protein

. Kutoa homoni

. Kutoa urea (kitu muhimu katika mkojo)

 

Homa Ya Ini – Hepatitis A

 

Hepatitis A ni ugonjwa unaoambukiza kwa haraka sana na husababishwa na kirusi aitwaye hepatitis A virus (HAV). Unaweza kupata ugonjwa huu kutoka kwenye maji au chakula kisicho salama au kwa kuwa karibu na mtu mwenye maambukizi ya virusi hao. Ugonjwa huu huweza kuondoka wenyewe bila tiba na mtu aliyepatwa na ugonjwa huweza kutibiwa akapona kabisa bila ya kupata uharibifu kwenye maini yake. Unaweza kujikinga kutokana na ugonjwa huu kwa kujiwekea tabia ya kuosha mikono mara kwa mara. Mtu anaweza kupata chanjo endapo yupo kwenye mazingira hatarishi.

Dalili za Hepatitis A: Dalili za ugonjwa huu huanza kujitokeza baada ya angalau wiki moja baada ya kupata maambukizi, nazo huwa:

. Uchovu
. Kichefuchefu na kutapika
. Maumivu ya tumbo hasa maeneo ya ini upande wako wa kulia chini ya mbavu
. Kukosa hamu ya kula
. Homa
. Mkojo mweusi
. Maumivu ya joints
. Ngozi na macho kuwa njano

Unaweza kuwa na homa mfululizo kwa wiki kadhaa kama hepatitis A si kali sana au kuugua sana kwa miezi kadhaa. Lakini si watu wote wenye maambukizi ya hepatitis A wataona dalili hizi.

 

ugonjwa wa hepatitis A

 

Chanzo Cha Hepatitis A: Unaweza kupata hepetitis A kwa kula chakula chenye kinyesi hata kama ni kwa kiwango kidogo sana. Virusi wa hepatitis A hushambulia seli za maini na kusababisha maini kushindwa kufanya kazi yake. Pamoja na kula chakula na kunywa maji yasiyo salama, unaweza kupata virusi hawa kwa kula samaki wabichi kutoka kwenye maji yaliyochafuliwa na kinyesi au kujamiiana na mtu mwenye maambukizi ya virusi hao.

Hepatitis A haisababishi madhara ya kudumu kwenye maini na huwa haiwezi kuwa ya kudumu (chronic).

Tiba Ya Hepatitis A: Hakuna tiba maalum kwa ugonjwa huu hadi sasa.  Mwili wako wenyewe unaweza kupambana na ugonjwa huu. Mara nyingi ugonjwa huu hupona katika miezi sita bila kuacha madhara ya kudumu kwenye maini. Kinachotakiwa kufanya ni kupambana na dalili zilizojitokeza ikiwa ni pamoja na:

. Kupumzika – watu wengi wakishaambukizwa hupata uchovu wa mwili na miili kukosa nguvu.
. Kupambana na kichefuchefu – yafaa kula kidogo kidogo badala ya mlo mkubwa wa mara moja.
. Kupumzisha maini – yapumzishe maini kwa kuchagua dawa za kuzitumia na kuacha kunywa pombe.

 

 

Livergen Capsule

Dawa ya kutibu homa ya ini (bofya juu ya picha kusoma maelelzo)

 

Tutaendelea kuchambua aina nyingine za hepatitis,  hepatitis B, C, D, na E, katika ukurasa ujao.

Usisite kuuliza maswali uliyo nayo au kutoa maoni uliyo nayo kuhusu mada yetu ya leo. Tutafurahi sana kuona kuwa tumekujibu vizuri.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.
Ukurasa             1               2            3          4

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii