Tatizo La Kukosa Hedhi (Amenorrhea)

 

 

amenorrhea cover

 

Katika mada yetu ya leo tutalijadili tatizo la kukusa hedhi ambalo kitaalamu huitwa amenorrhea. Mwanamke anakuwa na tatizo hilo pale ambapo anakosa hedhi kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo, au msichana ambaye hajaanza kupata hedhi akiwa na umri wa miaka 15.

Sababu ya kawaida ya kukosa hedhi ni ujauzito. Sababu nyingine ya kukosa hedhi ni dosari katika viungo vinavyojenga mfumo wa uzazi au tezi zinazosaidia kudhibiti viwango vya homoni katika mwili. Tiba ya chanzo cha tatizo mara nyingi huondoa tatizo hili la mwanamke kukosa hedhi.

Amenorrhea hugawanywa katika aina mbili ambazo ni  Primary amenorrhea na Secondary Amnorrhea

. Primary amenorrhea ni kukosekana kwa hedhi na mabadiliko ya kijinsia (kama kuota maziwa na kuota mavuzi) kwa msichana wa miaka 14 au kukosekana kwa hedhi kukiwa na mabadiliko ya kijinsia kwa msichana wa miaka 16.

 
. Secondary amenorrhea ni kukosekana kwa hedhi kwa mwanamke ambaye awali alikuwa anapata hedhi lakini baadaye akasimama kwa miezi 3 au zaidi bila ya kuwa na ujauzito, bila ya kuwa na maziwa ya kunyonyesha, bila kuzuia mzunguko wa wa hedhi kwa vidonge, au kukoma hedhi.

 

amenorrhea cover image

 

Ili mwanamke awe na mzunguko wa hedhi mzuri, hypothalamus, tezi ya pituitary, ovari, na uterus vyote vinatakiwa vifanye kazi ipaswavyo. Hypothalamus huiamuru tezi ya pituitary kutoa homoni za follicle-stimulating (FSH) na luteinizing (LH). FSK na LH husababisha ovari kutoa homoni za estrogen na progesterone. Estrogen na progesterone zinahusika katika mzunguko wa mabadiliko katika endometrium (utando unaofunika uterus), pamoja na hedhi. pamoja na hayo yote, mkondo wa uke lazima uwe wazi ili kuruhusu damu ya hedhi.

 

Nini Kinasababisha Kukosa Hedhi?

 

Amenorrhea inaweza kutokea kwa sababu nyingi. Baadhi zikiwa ni za kawaida katika maisha ya mwanamke, wakati nyingine zikisababishwa na matumizi ya madawa au zikiwa ni ishara ya tatizo la kiafya. Tatizo la kukosa hedhi linaweza kusababishwa na dosari yo yote kwenye hypothalamus, pituitary, ovari, mkondo wa uke au ya kiutendaji kimwili.

 
Sababu za kawaida

. Ujauzito
. Kunyonyesha
. Kukoma hedhi

 

Dawa za Kuzuia Mimba

Wanawake wengine wakitumia vidonge vya kuzuia mimba hukosa hedhi. Hata baada ya kuacha matumizi ya vidonge hivyo, huwachukua muda miili yao kurudi kwenye hali za kawaida na kuanza kuona hedhi zao. Njia za sindano au kupandikiza zaweza pia kuleta tatizo la kukosa hedhi.

 

Mitindo Ya Maisha

Baadhi ya mitindo ya maisha huweza kuchangia mwanamke kukosa hedhi. Kwa mfano:

. Kuwa na uzito mdogo sana. Kuwa na uzito mdogo kupita kiasi – asilimia 10 chini ya uzito wa kawaida – husimamisha shughuli nyingi za homoni ndani ya mwili, hivyo kusimamisha uzalishaji wa mayai

. Mazoezi zaidi ya kawaida. Wanawake wanaoshiriki shughuli zinazodai mazoezi ya juu, hujikuta wakipoteza hedhi zao. Baadhi ya sababu zinachangia kwa wanariadha, ikiwa ni pamoja na uzito mdogo, kuwa na mafuta kidogo ndani ya mwili, msongo wa mawazo na matumizi makubwa ya nishati ya mwili.

. Msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo huweza kubadilisha kwa muda utendaji kazi wa hypothalamus – sehemu ya ubongo inayosimamia homoni zinazoratibu hedhi. Uzalishaji wa mayai na hedhi, hivyo vyaweza kusimama. Hedhi za kawaida hurudi baada ya msomgo wa mawazo kupungua.

 

Kukosa Uwiano Wa Homoni

Matatizo kadhaa katika viungo vya mwili huweza kuvuruga mpangilio wa homoni katika mwili, ikiwa ni pamoja na:

 

Sababu Zinazotokana Na Hypothalamus
. Uvimbe karibu na tezi ya pituitary (Craniopharyngioma)
. Kallman syndrome (upungufu wa gonadotropins, homoni zenye uwezo wa kusimamia ukuaji na ufanyaji kazi wa viungo vyz uzazi )
. Upungufu wa lishe
. Uzito mdogo au kuchelewa kukua

 
Sababu Za Tezi Ya Pituitary
. Uwingi wa homoni ya prolactin, homoni inayosimamia utoaji wa maziwa wakati mama ananyonyesha, katika damu. Hali hii kitaalamu huitwa prolactilemia na husababishwa na uvimbe (prolactinoma) katika tezi ya pituitary.

. Dosari zinazoanzia kwenye uvimbe wa aina nyingine wa kwenye pituitary (kama, cushing syndrome, acromegaly, au thyroid-stimulating hormone)
. Kufa kwa seli za pituitary baada ya mwanamke kujifungua

. Seli za pituitary kufa baada ya kushambliwa na kinga za mwili (autoimmune hypophysitis)

. Uvimbe ndani ya tezi ya pituitary

. Ugonjwa ambao hushambulia pituitary (sarcoidosis)

 
Sababu Zinazotokana Na Ovari

 
. Kutozalishwa kwa mayai (anovulation)

. Kuwa na uwingi wa homoni za kiume ndani ya damu (hyperandrogenemia)

. Kuvurugika kwa homoni (Polycystic ovary syndrome)

amenorrhea polycystic ovarian syndrome

 

. Kufeli kwa ovari mapema

. Ugonjwa wa kurithi unaodumaza ovari,  kuzuia hedhi (Turner syndrome)

. Seli za ovari kushambuliwa na kinga za mwili (Autoimmune oophoritis)

. Mionzi au tiba za chemotherapy

. Ugonjwa wa kurithi unaojaza galactose ndani ya damu (Galactosemia)

. Dosari za kimaumbile katika mkondo wa njia ya uzazi

 
Sababu za Kiutendaji

. Kuwa na uzito mdogo kwa sababu ya kuogopa kula (anorexia)/kula kupita kiasi (bulimia)

 

amenorrhea uzito mdogo

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

. Magonjwa sugu kama TB

.Kunenepa au kukonda kupita kiasi

. Utapiamlo

. Mfadhaiko au matatizo mengine ya kiakili

. Msongo wa mawazo wa kupitiliza

 

Matatizo Ya Kimaumbile

Matatizo katika viungo vya uzazi yanaweza kusababisha amenorrhea. Mifano ni kama:

Makovu kwenye tumbo la uzazi. Tatizo lilitwalo Asherman’s syndrome – kujenga kwa makovu juu ya ngozi ya juu ya uterus – huweza kutokea baada ya oparesheni ya uzazi, au baada ya tiba ya fibroids. Makovu kwenye uterus huzuia ujenzi wa kawaida na kujibandua kwa ngozi hiyo ya juu.

amenorrhea ovary

 

 

 

 

 

 

 

Kukosa Viungo Vya Uzazi. Wakati mwingine matatizo yanaanzia kwenye ukuaji wa mtoto tumboni yanayosababisha msichana azliwe bila baadhi ya viungo vya uzazi, kama uterus, cervix au uke. Kwa sababu viungo vyake havikukua vizuri, haweza kupata hedhi.

Dosari Za Kimamumbile Za Uke. Kitu kitakachoziba njia ya uke kinaweza kusababisha kuonekana kwa hedhi ya wazi. kunaweza kukatokea utando au ukuta katika uke ambao utazuia utokaji wa damu kutoka kwenye uterus na cervix.

 

Dalili Za Amenorrhea

 

Amenorrhea ni dalili kuwa kuna tatizo lililochificha na si ugonjwa ka yenyewe. Dalil nyingine huwez kutokea kulingana na chanzo cha tatizo hilo la kukosa hedhi.

. Kutoka maziwa kwa mwanamke ambaye hana ujauzito, hali ambayo kitaalamu huitwa Galactorrhea, maumivu ya kichwa, kutokuona vizuri kingo za vitu vinaweza kuwa dalili za uvimbe ndani ya fuvu la kichwa.

. Kuongezeka kwa uotaji wa nywele kwa mtindo wa kiume (hirsutism), sauti nzito, chunusi kunaweza kusababishwa na kuzidi kwa androgen (homoni inayochangaia ujenzi wa tabia za kiume).

. Uyabisi wa uke, vipindi vya mwili kuwa na joto, kutoa jasho usiku, kukosa usingizi mzuri vinaweza kuashiria dasari katika ovari au kufeli kwa ovari.

. kuongeza kwa mwili au kukonda.
. Kuwa na wasiwasi kunaweza kujitokeza kwa mwanamke mwenye matatizo ya kiakili

 

Katika kurasa nyingine tutazungumzia matatizo ya maumivu kabla ya hedhi, maumivu wakati wa hedhi na matatizo ya kukoma hedhi. Jisike huru kuuliza maswali uliyo nayo au kutoa ushauri wako kuhusu mada yetu hii ya leo. Tutafurahi sana kukujibu.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

404 Not Found

404 Not Found


nginx/1.10.3