Tiba Ya Dawa Za Green World: Kwa Nini Utumie Virutubisho Vya Green World?

 

 

virutubisho vya Green World

 

Mara nyingi sana ninapowapa watu dawa za kampuni ya Green World wajitibu na magonjwa, naulizwa maswali mengi sana. Swali moja ninaloulizwa mara nyingi ni; Jee, dawa hizi hazina madhara? Wengine huenda mbali zaidi na kuniuliza; dawa hizi unazotupa zinafanye kazi? Kwangu mimi maswali yote hayo ni ya msingi na hufurahi kuona kuwa jamii yetu sasa ina upeo mkubwa zaidi kuhusu masuala ya madawa.

Kutokana na hilo nimeona niandike ukurasa huu kuelezea kuhusu maana ya kirutubishi, umuhimu wake katika mwili, uhusiano wa virutubishi na maradhi, jinsi virutubishi vinavyoweza kuzuia na kuponya maradhi na mwisho kwa nini virutubishi vya kampuni ya Green World Tanzania vinasaidia kuboresha afya zetu na kuponya maradhi tuliyo nayo. Ni mada ndefu sana hivyo nitaviweka vile vya muhimu tu na kwa kifupi sana.

Awali ya yote nifanye masahihisho ya matumizi ya maneno Dawa za Green World Tanzania. Kampuni Ya Green Tanzania haiuzi dawa kama tulivyozizoea zile za mahospitalini ambazo ni za kemikali. Kampuni hii inauza bidhaa zake ambazo ni virutubishi vinavyotokana na mimea; matunda, mboga mboga, mizizi n.k. na madini. Po pote pale nilipotaja dawa katika mada hii, ieleweke kuwa ni virutubishi.

 

Umuhimu Wa Virutubishi Katika Mwili

 

Ili binadamu aweze kuishi anahitaji virutubishi. Virutubishi ni vitu vinavyopatikana kutoka kwenye chakula tunachokula. Chakula tukilacho huvunjwavunjwa na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na ndipo virutubishi hupatikana, ni vitu ambavyo huwezi kuviona kwa macho lakini ndivyo vinavyoiwezesha miili yetu kukua, kuwa na nguvu na kujilinda kutokana na maradhi. Kuna aina tofauti za virutubishi, unaweza kusoma zadi kwenye ukurasa wa “Virutubisho Vya Mwili-Nutrients.” Tunahitaji kula chakula cha aina nyingi ili mwili upate virutubishi muhimu unaovihitaji.

Mtoto anapozaliwa, ngozi yake, mifupa, nyama na viungo vingine vyote vimetengenezwa kutokana na virutubishi ambavyo vilitokana na chakula ambacho mama yake alikula yeye akiwa tumboni. Akiwa mkubwa bado mwili wake unahitaji virutubishi kila wakati ili mwili wake uweze kumudu shughuli mbalimbali. Mahitaji ya virutubishi kwa mwili wa mtu hutofautiana kutokana na umri alio nao, jinsia, mazingira anapoishi na kazi aifanyayo. Kwa mfano mama mjamzito anahitaji virutubishi vya kumjenga mtoto wake aliye tumboni tofauti na ajuza anayehitaji kuimarisha mifupa yake na kukarabati seli zake za mwili zinazokufa.

 

Ukosefu Wa Virutubishi Na Maradhi

 

Mgonjwa akienda kupata tiba hushauriwa ale zaidi chakula cha aina fulani na/au aache kabisa kutumia chakula cha aina fulani. Utaona kuwa chanzo cha magonjwa ni kukosa virutubishi muhimu katika mwili na kuwa tiba yake ni kupata virutubishi hivyo vilivyokosekana kwa kula chakula cha aina fulani. Dawa inayotolewa ni kwa ajili ya kuondoa dalili za ugonjwa zilizokwisha tokea na si kuondoa chanzo cha ugonjwa.

 

 

Tiba ya dawa za green world

 

Inabidi kutoa tahadhali hapa kuwa kutojisikia kuumwa si kwamba afya yako imeimarika kabisa kwani kuna baadhi ya magonjwa hujijenga polepole kwa muda mrefu, mara nyingine kwa miaka mingi kabla ya kujitokeza na kuanza kukusumbua. Hivyo basi, inafaa kila wakati kuhakikisha kuwa unaupa mwili wako chakula chenye virutubishi vya kutosha ili kujiweka sawa na magonjwa haya nyemelevu.

 

Kwa Nini Tunahitaji Virutubishi Vya Kiada

 

Maendeleo ya sayansi, teknolojia na viwanda yamechangia kwa kiwango kikubwa kubadilisha namna tunavyoishi na kupata chakula chetu cha kila siku. Matokeo makubwa ni kwamba sasa miili yetu haipati chakula chenye virutubishi vya kutosha kwa miili yetu na tunaingiza vitu vingi ndani ya miili yetu ambavyo havitakikani. Mifano ya vitu ambavyo hatuwezi kuvikwepa na vinatuathiri kila siku ni kama ifuatavyo hapa chini:

 

Uchafuzi Wa Hewa

Binadamu wa sasa tunaishi kwenye mazingira ambayo hewa yake inachafuliwa kwa namna nyingi. Uwepo wa magari mengi kwenye barabara zetu yanayotoa moshi unatufanya tuvute hewa hiyo chafu.

 

uchafuzi wa hewa

 

Uwingi wa viwanda huchangia katika kutufanya tuvute hewa ambayo si salama kwa afya zetu. Hewa iliyochafuliwa huchangia katika kutenengeza radikali huru (free radicals) katika miili yetu.

 

kuchafua hewa

 

Uwepo wa radikali huru kwa wingi katika miili yetu umehusishwa na magonjwa ya moyo na saratani. Radikali huru pia zimebainika kuchangia miili yetu kuzeeka haraka.

 

 

Uchafuzi Wa Maji

Vyanzo vya maji vinachafuliwa na mabaki ya kemikali kutoka kwenye viwanda na watu katika shughuli zao za kawaida za maisha.
uchafuzi wa maji
Hata katika uzalishaji wa kawaida wa maji ya kunywa na kupikia, kemikali (chlorine) hutumika katika jitihada za kuyafanya maji hayo kuwa salama. Binadamu tutumiapo maji haya, tunaingiza kemikali zisizotakiwa katika miili yetu.

 
Sumu Katika Chakula

Ili kupata mazao kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye mashamba yetu, matumizi ya mbolea za kemikali za aina mbalimbali hutumika ili kuotesha na kuikuza mimea. Aina mbali mbali za dawa za kuulia wadudu pia hutumika kwenye mashamba yetu.

 

uchafuzi wa mimea kwa dawa

 

Vitu hivi baadaye vyote huingia ndani ya mwili wa binadamu na kusababisha madhara kwenye afya zetu. Uchafuzi wa chakula chetu huongezeka pale nafaka na mimea vinapohifadhiwa na wakati wa maandalizi kabla havijaliwa, hii ni pamoja na utengenezaji wa maumbo au kuboresha rangi ya chakula.

Mionzi

Teknolojia ya sasa imekuja na vifaa vingi sana vinavyotumia mionzi. Binadamu wa sasa hatuwezi kukwepa kutumia simu za viganjani, televisheni, microwave ovens na kupata tiba kwa kutumia mionzi. Tatizo jingine ni kuishi karibu na nyaya za kusambazia umeme na mitambo inayotoa mionzo mikali.

 

uchafuzi kwa mionzi ya umeme

 

Matatizo mengi ya kiafya yanahusishwa na uchafuzi wa mazingira kwa mionzi ya umeme. Mionzi ya umeme huathiri DNA, hupunguza ujazo wa mbegu za kiume (low sperm count) na kusababisha ugumba kwa wanaume. Mionzi ya umeme husababisha saratani za aina mbalimbali, hupunguza uwezo wa kutuliza mawazo kwenye kitu kimoja – Attention Deficit Disorder (ADD), huleta hali ya kupenda upweke – Autism,  husababisha mfadhaiko, husababisha kukosa usingizi, maumivu ya mgongo, ugonjwa wa Parkinson’s na mengineyo.

Hivi vitu vyote na vingine vingi hupunguza ubora wa chakula tunachokula na kutufanya tule chakula ambacho hakina virutubishi vya kutosha kwa mahitaji ya miili yetu, kutufanya tule vitu ambavyo havihitajiki ndani ya miili yetu na kutusababishia magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kansa, magonjwa ya moyo na kisukari. Hii ndiyo sababu kubwa ya kuhitaji kutumia virutubishi vya kiada kwa afya za miili yetu.

 

Virutubishi Vya Green World Vinafanyaje Kazi?

 

Nchi ya China ina mchango mkubwa katika maendeleo ya dunia hii. Pamoja na ugunduzi katika maeneo ya usanifu wa majengo, baruti, dira, uchapishaji na utengenezaji wa karatasi, wachina pia waligundua maajabu ya mimea katiba tiba ya mwili wa binadamu. Waligundua kuwa baadhi ya chakula cha aina fulani kilikuwa na nguvu ya kuleta nafuu au kutibu magonjwa fulani na hapo ndio ulikuwa mwanzo wa tiba kwa kutumia mimea. Watu wengi duniani sasa wamekubali na wanatumia tiba hii mbadala ya mimea.

 

Dawa za Green World

Green World Research Centers

 

Kampuni ya Green World inafanya utafiti wa tiba hii asilia ya kichina kwa kutumia mimea na tayari imeweza kutengeneza bidhaa zaidi ya 100 katika viwanda vyake vilivyoko huko Tianjing na Nanjing. Bidhaa zake zimekubalika na zinatumika katika nchi nyingi za Asia, Afrika, Ulaya Ya Mashariki na Marekani. Hapa nchini Tanzania kampuni hii ilisajiliwa mwaka 2009 na imepasishwa na mamlaka ya kusimamia chakula na dawa Tanzania- Tanzania Food And Drugs Authority (TFDA).

 

pembe tatu ya dawa za Green World

Kampuni ya Green World hutengeneza bidhaa ambazo hufanya kazi katika muundo wa pembe tatu. Bidhaa hizo huondoa sumu mwilini, huupa mwili virutubishi unaovihitaji na kuongeza kinga za mwili wa mtumiaji.

 

Katika mada nyingine tutaona kwa nini kampuni ya Green world Tanzania ndiyo fursa bora ya biashara ya mtandao Tanzania.

Ndugu msomaji kuwa huru kuuliza maswali yo yote uliyo nayo au kutoa maoni yako kuhusu mada yetu hii ya leo. Tutafurahi sana kupata mchango wako na kukujibu maswali yako.

Kwa maoni au kupata maelezo zaidi, tuandikie kupita promota927@gmail.com au tupigie simu kupitia namba 0655 858027 na 0756 1818651. Unaweza pia kujaza fomu chini ya ukurasa huu.

 

Tafadhali tembelea blog yetu kujisomea mada mbali mbali zinazohusu biashara za mtandao na fursa za kufanya biashara za mtandao zinazotolewa na kampuni za Green World Tanzania na Trevo Tanzania Ltd. Humo unaweza kuona wasomaji wengine wana maoni gani kuhusu mada zetu tunazoziandika. Pia unakaribishwa kuona video mbali mabali zinazohusu biashara ya mtandao ya kampuni ya Green World kwenye channel yetu ya YouTube.

Kutembelea blog bofya HAPA.
Kutembelea channel yetu ya YouTube bofya HAPA.

 

 

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Namba Yako Ya Simu

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni Yako

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

404 Not Found

404 Not Found


nginx/1.10.3