Namna Ya Kuingia Kwenye Tovuti Yako Ya Green World

 

 

mawasiliano kwa simu

 

 

Kampuni ya Green World inatoa vifaa vingi vya kukusaidia kufanya biashara yako kwa ufanisi zaidi. Moja ya zana hizo ni tovuti yako binafsi ambamo utaona taarifa zote muhimu zinazohusu biashara yako. Utaona watu wote uliowaunganisha binafsi kwenye biashara hii na wale wote waliounganishwa na watu walio chini yako. Kiujumla, utaiona timu yako yote.

Utaweza kuona ni bidhaa za kiasi gani umekwisha nunua toka ulipojiunga na kampuni, vile vile kwa kila mmoja wa watu walio chini yako. Utaona kiasi ulichokinunua mwezi huu na kila mmoja wa watu wako amenunua kiasi gani. Kuna taarifa nyingine nyingi katika kurasa za tovuti hii ambayo ni mahsusi kwa biashara yako.

Faida za kuitumia tovuti hii ni nyingi, ikiwa ni pamoja na kukusaidia kukokotoa bonasi yako ya mwezi, kujua mwenendo wa kiutendaji wa watu walio chini yako, kukusaidia kupanga timu yako vizuri, na nyingine nyingi.

 

Hatua za Kufuata:

 

1. Kuingia kwenye tovuti ya kampuni kupitia google (au browser nyingine), andika en.world-food.com kisha weka cursor yako juu ya alama ya  V (ya kijani) kwenye kona ya upande wa kulia wa karatasi kama inavyoonyeshwa kwenye picha. Kwenye bendera zitakazotokea, chagua bendera ya nchi yako, kisha bofya juu yake.

 

Tovuti ya Green World

 

 

2. Kujaza IDs na password yako angalia sehemu ya juu ya ukurasa ambako utaviona vijisanduku vitupu vilivyoandikwa MemberID:,  PassWord:,  na 

Kujaza ID yako andika TZ01 (kwa watanzania) kisha ID yako, bila kuacha nafasi ndani ya kijisanduku kilichoandikwa Member ID: Kwa mfano, mwanachama mwenye ID namba 10160940 ataandika:

TZ0110160940

Kujaza password yako, hesabu namba sita kuanzia kulia kwenye ID yako, kisha ziandike nambari hizo ndani ya kijisanduku cha passWord. Kwa mfano, mwanachama wetu wa hapo mwenye namba  10160940  atahesabu namba zenye rangi nyekundu 10160940 na ataandika:

160940

Kujaza ID ya mwanchama aliyekudhamini (upline member wako), utaandika ID yake ukitangulia tena na TZ01 ndani ya kijisanduku kilichoandikwa . Mwanachma wetu wa hapo juu mwenye upline member mwenye namba 14005752 ataandika:

TZ0114005752.

 

 

3. Kuingia kwenye tovuti yako utabofya juu ya neno Login. Kama mabo yalienda vizuri, utakuwa umeingia ndani ya tovuti yako na utauona ukurasa huu.

 

Tovuti yako ya Green World

 

Kuingia kwenye ukurasa unaofanana na print-out unazopata kila mwezi, bofya kwanza juu ya maneno Bonus Management kisha BV Inquiry.

 

print out ya Green World

 

Kisha malizia kwa kubofya ndani ya kijimviringo (Network) na juu ya neno Display.

 

Nategemea umeweza kuingia kwenye tovuti yako na sasa unajionea wewe mwenyewe ni nini unakifanya ndani ya Green World. Kama bado unapata matatizo, omba msaada kwa upline member wako au nipigie 0655 858027 au 0756 181651.

 

WE CARE,    WE SHARE

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

404 Not Found

404 Not Found


nginx/1.10.3