Ugonjwa Wa UKIMWI Ni Nini?

 

Ugonjwa wa UKIMWI

 

Katika ukurasa wetu wa leo tutaona ugonjwa wa UKIMWI ni nini na zipi ndizo dalili za ugonjwa huu. UKIMWI (Ukosefu Wa Kinga Mwilini) ni ugonjwa unaosababishwa na VVU (Virusi Vya UKIMWI). UKIMWI hudhoofisha mfumo wa kinga za mwili na kumfanya mtu aweze kuambukizwa au kupata magonjwa mbalimbali. Uwezo wa mwili wa kujikinga na maradhi hupungua zaidi kadri ugonjwa wa UKIMWI unavyoongezeka ndani ya mwili wa mgonjwa.

 

Mtu mwenye virusi vya UKIMWI tunasema ameathirika. Virusi vya UKIMWI hushambulia seli za T (T-cells) katika mfumo wa kinga za mwili. Mara nyingi mtu mwenye virusi vya UKIMWI atapata ugonjwa huu wa UKIMWI lakini si kila mtu aliye na virusi vya UKIMWI ana ugonjwa huu. UKIMWI ni ugonjwa na mtu anakuwa na
UKIMWI pale ambapo virusi vya UKIMWI alivyonavyo ndani ya mwili vimefikia hali ya kudhoofisha kinga zake za mwili na mwili kushindwa kuzuia maradhi mengine yanayounyemelea. Mtu aliye na virusi vya UKIMWI baadaye huupata ugonjwa huu na asipotumia dawa, hufariki dunia.

Utafiti sasa unaonyesha kuwa ugonjwa ulianza miaka ya mwishoni mwa karne ya 19 na ya mwanzoni mwa karne ya 20 na utafiti huo unaonyesha kuwa ugonjwa huu ulianzia Afrika Ya kati na Afrika Magharibi. Mgonjwa wa kwanza alibainika kuwa na ugonjwa huu mwaka 1980.

Hadi sasa hakuna dawa ya kuondoa UKIMWI bali kuna tiba za kupunguza makali ya ugonjwa na kumsaidia mgonjwa kuongeza uhai wake. Baadhi ya watu waliotumia tiba hizi wameishi muda mrefu na maisha ya kawaida.

Ugonjwa unaweza kugundulika katika hatua zake za mwanzo kabisa hivyo kumsaidia mgonjwa kuweza kuanza kupata tiba ya kuzuia virusi kuongezeka kwa haraka katika mwili wake na hivyo kurefusha muda wake wa kupata UKIMWI. Mgonjwa anayetumia dawa za kurefusha maisha bado ana virusi hivi na anaweza kuambikiza
watu wengine.

 

UKIMWI UNAAMBUKIZWA VIPI?

 

VVU (Virusi Vya UKIMWI) hupatikana ndani ya majimaji yaliyomo mwilini mwa mgonjwa huyu, ikiwa ni ndani ya shahawa za mwanamme, damu na maziwa ya mama. Ugonjwa huu huambukizwa pale damu ya mtu inapokutana ana kwa ana na damu ya mtu aliyethirika au kwa ngono. Vile vile mama mwenye UKIMWI huweza kumuambukiza mwanae aliye tumboni wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au kwa kumnyonyesha maziwa.

Ugonjwa wa UKIMWI huambukizwa pia kwa kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo, kufanya mapenzi kinyume na maumbile, kuongezewa damu isiyo salama na kupitia sindano ambazo si salama.

Dalili Za UKIMWI

 

Watu wengi wenye virusi vya UKIMWI hawaoni dalili zo zote kwa miaka kadhaa. Wengine hupata mafua kati ya wiki mbili hadi sita baada ya kupata maambukizi ambayo hudumu kwa kipindi cha hadi wiki nne. Dalili nyingi zinazotokea zinatokana na maambukizi ya bacteria, virusi, fungus na wadudu wengine.

Dalili za awali za UKIMWI ni kama zifuatazo:

.   Homa
.    Kusikia baridi
.    Maumivu ya joints
.    Maumivu ya misuli
.    Koo kavu
.    Jasho (Hasa usiku)
.    Uchovu wa mwili
.    Udhaifu
.    Kukonda

Baada ya dalili hizi za awali kutoweka, mara nyingi hakuna dalili zo zote zitakazooneka kwa kipindi kirefu. Wakati huu wadudu hawa wanazidi kuzaliana, kuongezeka na kuharibu mfumo wa kinga za mwili. Kipindi hiki cha ukimya kinaweza kwenda hadi miaka 10 wakati huu wote mtu akijisikia vizuri tu na kuonekana mwenye afya.

Dalili za mwisho za UKIMWI zinaweza kuwa:

. Kutoona vizuri
. Kuharisha mfululizo
. Kikohozi kikavu
. Homa kali inayokwenda kwa muda mrefu
. Kuvuja jasho usiku
. Uchovu wa mwili mfululizo
. Kupumua kwa shida
. Kukonda
. Vijidoa vyeupe kwende midomo na ulimi

Mtu anapofika kwenye hatua hii na kuanza kuonyesha dalili hizi, anaweza sasa kunyemelewa na gonjwa lo lote linaloweza kumuua. Magonjwa hayo nyemelezi ni kama:

. Esophagitis (matatizo kwenye ngozi laini ya kooni)
. Maambikizi kwenye mfumo wa neva (acute aseptic meningitis, subacute encephalitis na peripheral neuropathy.
. Pneumonia.
. Kansa kama za Kaposi’s sarcoma, kansa ya shingo ya uzazi, kansa ya mapafu, rectal carcinomas, hepatocellular carcinomas, kansa za kichwa na shingo, na lymphomas.
. Toxoplasmosis (ugonjwa unaoshambulia ubongo).
. Tuberculosis (TB).

dalili za ukimwi

Vipimo Vya UKIMWI

 

Ili kugundua kama mtu ana virusi vya UKIMWI au la, damu hutolewa na kupimwa kutumia vipimo maalumu kwa virusi vya IKIMWI. Kama virusi hivi vikipatikana, majibu huitwa “Positive”. Damu ya mgonjwa huyo hupimwa zaidi ya mara moja kabla ya kumpa mgonjwa majibu ya positive.

 

 

kuzuia ukimwi

 

Mgonjwa aliyegundulika kuwa positive hushauriwa kuchukua vipimo vingine ili kuona virusi hivi vimesambaa kwa kiwango gani na kujua ni lini mgonjwa aanze tiba. Ni vizuri mtu kuchukua tahadhari ya kupima mara baada ya kuwepo kwenye mazingira hatarishi ya UKIMWI kwani ugonjwa huu ukigundulika mapema zaidi
uwezekano wa tiba kufanikiwa unakuwa mkubwa zaidi. Inachukua kiasi cha wiki tatu hadi miezi mitatu baada ya maambukizi, virusi hivi kuweza kuonekana kwenye vipimo.

 

Tiba Ya UKIMWI

 

Ugonjwa wa UKIMWI hushambulia taratibu seli maalumu za kinga za mwili ziitwazo CD4 T-cell na virusi vya ugonjwa huu huvitumia viini vya seli hizo kuzaliana na mwisho kuziua seli hizo. Kwa vile mgonjwa huyu atakuwa hajaanza kuonyesha dalili za mwisho za UKIMWI katika kipindi hiki ( asymptomatic period), yafaa idadi ya seli zake za CD4-T kufuatiliwa kwa karibu ili kuzuia zisishuke na mgonjwa kupata UKIMWI. Idadi ya seli hizo ikishuka chini ya 500 cells/mm3, mgonjwa huyu tayari atakuwa na UKIMWI na anapaswa kuanza tiba.

Hadi sasa hakuna chanjo ya UKIMWI wala tiba ya kuponya kabisa ugonjwa huu lakini kuna tiba zinazotolewa kuboresha maisha ya mwathirika na kumuongezea miaka yake ya kuishi.

Vidonge Vya Dharura – Emergency HIV Pills: Kama mtu anaamini kuwa amekuwa katika mazingira ya kuambukizwa ukimwi katika saa 72 zilizopita, anaweza kupewa dawa ya kuzuia maambukizi na akasalimika. Dawa hii huitwa PEP (post-exposure prophylaxis). Dawa hii inatakiwa kutumiwa mara tu baada ya kukutana na virusi vya UKIMWI. Dawa hii hutumiwa kwa wiki nne.

Dawa za ARVs – Antiretroviral drugs: UKIMWI hutibiwa kwa kutumia dawa zinazoitwa ARVs (antiretrovirals).

 

Tiba ya ukimwi

 

 

Dawa hizi huzuia maambukizi na kupunguza kasi ya kuongezeka kwa virusi vilivyomo ndani ya mwili. Kwa kawaida mgonjwa hupewa mchanganyiko wa madawa yanayoitwa HAART (highly active antiretroviral therapy). Mchanganyiko huu hutolewa kulingana na mahitaji ya mtu. Tiba ya UKIMWI kwa sasa ni ya maisha kwa vipindi atakavyopangiwa mgonjwa.

Tiba Mbadala: Kuna tiba nyingi zinazotolewa ikiwa ni pamoja na za majani, nyingi katika hizi hazijahakikishwa kuwa ni bora au si bora. Kwa ushauri kuhusu hili mwone dakatari wako au tuandikie kwa kutumia anuani yetu hapo chini.

 

Dawa Ya Kuongeza Kinga Za Mwili

Dawa Ya Kuongeza Kinga Za Mwili. Bonyeza Juu Ya Picha Kusoma Maelezo

 

Ukurasa wetu wa leo umezungumzia maana ya ugonjwa wa UKIMWI na kuelezea dalili za UKIMWI zikiwemo dalili za awali na dalili za mwisho za UKIMWI. Katika kurasa nyingine tofauti tunazungumzia VVU ni nini, Virusi vya UKIMWI vilitoka wapi na ugonjwa wa UKIMWI kwa binadamu ulitoka wapi.

Usisite kuuliza swali lo lote ulilo nalo au kutoa maoni yako kuhusu mada hii. Ni furaha kwetu kukujibu na kubadilishana mawazo na wewe msomaji wetu.

Kwa maelezo zaidi na ya kina, tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au tutumie barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo:  0655 858027 au 0756 181651.

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Namba Yako Ya Simu

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni Yako

 

Ukurasa    1      2       3

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii