Sababu Za Ugumba Kwa Mwanamke

 

wanandoa na ugumba

 

Katika ukurasa uliopita tulijadili sababu za mwanamke kutopata mtoto zinazotokana na mapungufu ya mwanamme. Katika ukurasa huu tatarejea kwenye mada kuu ya kuona sababu za ugumba au utasa kwa mwanamke na kutazama mapungufu katika mwili wa mwanamke yanayochangia tatizo hili. Kama ada, katika ukurasa mwingine tutaona njia zinazotumika kuondoa tatizo hili la mwanamke kukosa kizazi.

Tulisema kwamba ugumba ni hali ambapo mwanamme na mwanamke wamejamiiana kwa kipindi cha mwaka mmoja bila kinga na bado mwanamke hakuweza kupata ujauzito. Tuliona kuwa hali hii inachangiwa na jinsia zote na si mwanamke peke yake kama ilivyozooleka kuamini hapo zamani. Ilibainishwa kuwa theluthi moja ya nyumba zenye tatizo hili huwa imeathirika kutokana na mapungufu ya mwanamme, theluthi nyingine kutokana na mwanamke na inayobakia inaathiriwa na matatizo au ya wote wawili au yale ambayo hayaeleweki.Tulishauri kuwa linapotokea tatizo hili, wote wawili  wanatakiwa wapimwe ili kujua ni nani kati yao ndiye chanzo cha tatizo.

Sababu Za Mwanamke Kukosa Kizazi

 

Ili mwanamke apate mimba, sehemu zote za mwili wake zinazohusika na uzazi zinatakiwa zifanye kazi inavyotakiwa na katika hatua zote. Hatua katika utengenezaji wa mimba ni kama zifuatazo:

 

1. Moja kati ya ovari mbili za mwanamke kuachai yai lililokomaa
2. Yai hii kusafirishwa na mrija wa uzazi (fallopian tube)
3. Mbegu za mwanamme kusafiri hadi kwenye cervix, kupitia tumbo la uzazi (uterus) hadi kwenye mrija wa uzazi, kulifikia yai na kulipevusha.
4. Yai lililopevushwa kusafiri kupitia mrija wa uzazi hadi kwenye tumbo la uzazi  (uterus).
5. Yai kunata kwenye ukuta wa uterus na kukua

Ugumba kwa mwanamke unaweza kutokana na dosari katika hatua yo yote katika hizo tulizozitaja na mara niyingine kutokana na dosari katika hatua zaidi ya moja.

Pamoja na kuwa kuna sababu nyingi za mwanamke kutopata mimba, lakini sababu kuu  tatu ndizo zinazohusika zaidi kama tutakavyozielezea hapa chini.

 

tatizo la kukosa mtoto

 

 

Kushindwa Kuzalisha Mayai (Anovulation)

 

Hili ndilo tatizo ambalo linachangia ugumba kwa wanawake kwa asilimia 30 lakini kwa bahati nzuri asilimia 70 ya wanawake wenye tatizo hili hupata tiba na kufanikiwa kupata watoto. Mwanamke mwenye tatizo hili hutoa mayai mara chache au hatoi mayai kabisa. Chanzo cha tatizo huwa ni moja ya yafuatayo:

1. Matatizo Ya Homoni

Matatizo ya homoni ndiyo yenye mchango mkubwa zaidi kwenye kumfanya mwanamke ashindwe kuzalisha mayai. Uzalishwaji wa mayai hutegemea mchanganyiko wa homoni utakaofanya kazi kwa kuhusiana bila kuvurugwa katika utendaji wake wa kazi.

 

Soy Power Capsule

Dawa Ya Ugumba Kwa Wanawake – Bonyeza juu ya picha kusoma maelezo yake

 

Kuna matatizo ya aina tatu yanayoweza kuvuruga mpangilio huo.

Kuzalisha Mayai Yasiyokomaa:

Matatizo Ya Hypothalamus: Hypothalamus ni sehemu ya ubongo inayohusika na kutoa ishara kwa tezi ya pituitary  (pituitary gland) ambayo nayo huamsha homoni za ovari zinazoruhusu yai kukomaa. Hypothalamus isipofanya kazi yake, mayai hushindwa kufika ukomavu. Asilimia 20 ya dosari za ukomavu wa mayai husababishwa na matatizo ya hypothalamus.

Matatizo Ya Pituitary Gland: Tumeona hapo juu kuwa tezi ya pituitary inahuvusika katika kukomaza mayai. Endapo pituitary itatoa homoni kwa kiwango kidogo au kikubwa kupita kiasi, ovari zitashindwa kuzalisha na kutoa mayai ipaswavyo. Hali hii hutokea pale tezi hii inapoharibiwa kwa ajali, kunapotokea uvimbe ndani yake au kunapokosekana ulingano wa kikemikali ndani ya tezi hiyo.

 
2. Makovu Kwenye Ovari

Uharibifu kwenye ovari unaweza kusababisha ovari hizi kushindwa kuzalisha mayai. Operesheni za mara kwa mara hujenga makovu kwenye ovari hizo na kuzifanya zishindwe kuzalisha mayai. Maambukizi ya magonjwa huweza pia kusababisha ovari kushindwa kuzalisha na kutoa mayai.

3. Kukoma Hedhi Mapema

Kukoma hedhi mapema ni tatizo ambalo halijaeleweka vizuri kisayansi. Baadhi ya wanawake wanaacha kupata siku zao za
kawaida kwenye umri usiotegemewa. Dhana moja ni kuwa hifadhi yao ya mayai imekwisha au nyingine ni kuwa inatokana na wanawake hawa kuwa wenye historia ya kuwa wanariadha waliokuwa na miili yenye uzito mdogo na waliofanya mazoezi
ya nguvu kwa muda mrefu. Kuna uwezekano kuwa kukoma hedhi mapema ni suala la urithi.

4. Matatizo Ya Follicle

Kuna tatizo lisilo na maelezo ya kisayansi “unruptured follicle syndrome” ambapo mwanamke hutengeneza mfuko wa kawaida wa yai wenye yai ndani yake kila mwezi lakini mfuko huo hugoma kupasuka na kuachia yai. Hivyo kwamba, yai hubaki ndai ya ovari na utolewaji wa yai nje ya ovari kutotokea.

 

Mirija Ya Uzazi (Fallopian Tubes) Kushindwa Kufanya Kazi Vizuri

 

Magonjwa katika mirija ya uzazi huathiri asilimia 25 ya wanafamilia ambapo tatizo laweza kuwa dogo la kunata kwa yai au kubwa la mirija kuzibwa kabisa. Tiba kwa matatizo ya mirija ya uzazi mara nyingi ni upasuaji. Matatizo yanayopelekea kuziba kwa mirija ya uzazi ni kama yafuatayo:
1. Maambukizi Ya Wadudu

Maambukizi ya virusi na bacteria yanayoenezwa kwa ngono husababisha makovu na uharibifu, kwa mfano, maambukizi ya
Hydrosalpnix yanayosababisha mirija ya uzazi kuziba pande zote na kujaa maji .

2. Magonjwa ya Tumbo

Magonjwa ya appendicitis na colitis huleta madhara kwenye tumbo ambayo yanayoweza kuiathiri mirija ya uazazi kwa kujenga makovu au kuiziba.

3. Upasuaji

Hii ni sababu kubwa ya magonjwa na uharibifu wa mirija ya uzazi. Upasuaji wa kwenye maeneo ya kinena na tumbo huweza kusababisha uharibifu utakaozuia upitaji wa yai.

4. Mimba Ndani Ya Mirija Ya Uzazi (Ectopic Pregnancy)

Mimba zinazotunga ndani ya mirija ya kizazi huweza kuleta uharibifu kwenye mirija hiyo hata kama tahadhali ya juu
itachukuliwa kuziondoa.

5. Matatizo Ya Kuzaliwa Nayo

Mara chache huweza kutokea kuwa mwanamke akazaliwa akiwa na dosari katika mirija yake ya uzazi.

 

Endometriosis

Endometriosis ni kuota kwa seli (endometrial cells) zinazofanana na zile zinazotanda ndani na nje ya mfuko wa uzazi (uterus) kwenye eneo nje ya mfuko wa uzazi. Endometrial cells ndizo zinazoufunika mfuko wa uzazi na seli hizi hubadilishwa kila mwezi wakati wa hedhi. Seli hizi huweza kuota kwenye maeneo mengine yaliyo nje kabisa ya mfuko wa uzazi na huitwa endometriosis implants. Maeneo ambayo seli huweza kuota ni kwenye ovari, mirija ya uzazi (fallopian tubes), kuta za nje za nyumba ya uzazi, utumbo, pelvis, kuma , cervix, kibofu na mara chache kwenye maini, mapafu na ubongo.

 

tatizo la endometriosis

 

Endometriosis imegundulika zaidi kwenye kundi la wanawake wenye umri kati miaka 25 na 35, ingawa mara chache
imeonekana kwa wasichana wadogo wa miaka kama 11. Endometriosis ni nadra kuonekana kwa wanawake waliokoma hedhi. Wanawake warefu , wembamba wenye uzito mdogo huonekana zaidi na tatizo hili. Kupata ujauzito katika umri mkubwa sana, kutozaa na kukoma siku mapema huongeza uwezekan wa kutokea endometriosis.

Kuota kwa seli hizi za ziada – na tendo la kuziondoa kwa operesheni – huweza kusababisha makovu ambayo huweza kuzuia yai la mwanamke lisiungane na mbegu ya mwanamme. Kuathirika kwa utando huu juu ya uterus huweza kuzuia kutungwa kwa yai lililopevushwa.

 

Sababu Nyinginezo

 

1. Sababu Za Kitabia

Baadhi ya tabia zetu huathiri afya zetu ikiwa ni pamoja na afya ya viungo vya uzazi na kupunguza au kuondoa uwezo wetu wa kuzaa watoto. Bahati nzuri tabia hizi zinaweza kudhibitika.

. Chakula Na Mazoezi: Ili tuwe na uwezo mzuri wa kuzaa watoto tunahitaji kupata chakula kizuri na kuipa miili yetu mazoezi ya kutosha. Wanawake wenye unene wa kupindukia au uzito mdogo sana wanapata shida kushika mimba.

. Uvutaji Wa Sigara: Uvutaji wa sigara umethibitika kupunguza kiwango cha mbegu (low sperm count) kwa wanaume, kuongeza uwezekano wa mimba kutoka, kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo au kabla ya wakati (njiti) kwa wanawake.

. Pombe: Unywaji wa pombe huongeza uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye matatizo na unywaji uliozidi huweza kuleta ugonjwa, Fetal Alcohol Syndrome. Kwa mwanaume, pombe hupunguza kiwango chake cha mbegu.

. Madawa: Madawa kama bangi (marijuana) hupunguza kiwango cha mbegu kwa wanaume. Utumiaji wa cocaine kwa wanawake huathiri figo za watoto watakaozaliwa.

 
2. Sababu Za Kimazingira

Uwezo wa mwanamke kutunga mimba unaweza unaweza kuathiriwa na uwepo wake kwenye mazingira yenye sumu au kemikali. Hii inaweza kuwa kwenye mazingira ya kazi au sehemu anayoishi. Baadhi ya kemikali zilizobainika na kuandikwa kuwa
zinapunguza uwezo wa mwanamke kupata mimba ni:

. Lead – husababisha mimba kutoka.
. Tiba – tiba ya mionzi ya mara kwa mara na chemotherapy huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na matatizo ya ovari.
. Ethylene Oxide – kemikali inayotumika kuua wadudu kwenye vifaa vya upasuaji na kutengenza dawa za kuulia wadudu huleta dosari kwenye mimba changa na kusababisha mimba kutoka.
. Dibromochloropropane (DBCP) – Kemikali inayopatikana kwenye dawa za kuulia wadudu husababisha mwanamke kukoma hedhi mapema.

 

 

Katika mfululizo wa mada hii, tumejadili maana ya mzunguko wa hedhi wa mwanamke na kuona awamu nne za mzunguko wa hedhi kwa mwanamke. Tumeona pia sababu za ugumba kwa mwanamme.  Tumejadili kwa kina sababu za mwanamke kukosa mtoto na kuelezea tiba za ugumba kwa mwanamke.

Katika ukurasa unaofuata “Tiba Ya Ugumba Kwa Wanawake” tutaona jinsi ya kuondoa au kupambana na tatizo  hilo.

Usisite kutuuliza maswali yako au kuomba ushauri kuhusu matatizo ya kukosa watoto. Tumia njia yo yote iliyo rahisi kwako baina ya hizi tulizoziorodhesha hapa chini.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini, au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

 

Ukurasa          1            2            3         4         5

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

404 Not Found

404 Not Found


nginx/1.10.3