Mkanda Wa Jeshi Ni Nini?

 

Mkanda wa jeshi - shingles

 

Mkanda wa jeshi (shingles) ni jina linalotumika mitaani kuutaja ugonjwa unaoshambulia ngozi na kujenga tabaka la vijipele vikubwa venye majimaji ambavyo mara nyingi hukamata upande mmoja wa mwili. Ingawa vijipele vya mkanda wa jeshi vinaweza kutokea sehemu yo yote ya mwili, mara nyingi hupenda kuota kifuani, shingoni, usoni, mgongoni na mikononi. Vijipele hivi hukaa juu ya ngozi kwa muda wa wastani wa wiki mbili hadi sita kisha hupotea. Vipele vya mkanda wa jeshi huambatana na maumivu makali na kusikia ngozi kuwaka moto. Aghalab ugonjwa huu humrudia mtu zaidi ya mara moja.

Mkanda wa jeshi huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa, zaidi ya miaka 50, utafiti ukionyesha kuwa zaidi ya nusu ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 80 hupatwa na mkanda wa jeshi. Vilevile huwapata zaidi watu waliopatwa na magonjwa yanayopunguza kinga za mwili, kama vile, UKIMWI na saratani. Tiba za mionzi na chemotherapy huweza kupunguza kinga za mwili za mgonjwa na kumfanya awe kwenye hatari kubwa ya kupata mkanda wa jeshi.

 

Mkanda Wa Jeshi Husababishwa Na Nini?

 

Mkanda wa jeshi husababishwa na kirusi aitwaye varicella-zoster, kirusi yule yule anayesababisha tetekuwanga (chickenpox). Varicella-zoster ni moja ya kundi la virusi waitwao herpes viruses, likijumisha virusi wanaosababisha mafua na vipele vya sehemu za siri. Mtu ye yote yule ambaye alishawahi kupata tetekuwanga anaweza kupata mkanda wa jeshi. Baada ya kupata tiba ya tetekuwanga na kupona, virusi hawa wanaweza kuingia kwenye mishipa ya mfumo wa fahamu na kutulia kimya kwa miaka kadhaa. Baadaye virusi hawa huamka na kusafiri kupitia mishipa ya fahamu hadi kwenye ngozi – na kusababisha mkanda wa jeshi. Hii ndiyo sababu ya ugonjwa huu kuitwa kwa jina jingine la herpes- zoster. Sababu za kurudiwa na ugonjwa huu baadaye hazijawa bayana lakini huenda hii inatokana na kuwa kinga dhidi ya maambukizi hupungua umri unapokuwa mkubwa.

 

Mkanda Wa Jeshi
Mtu mwenye mkanda wa jeshi anaweza kumwambukiza mtu mwingine ambaye mwili wake hauna kinga dhidi ya tetekuwanga.
Hii itatokea pale mtu huyo atakapogusa vipele vilivyo wazi vya mkanda wa jeshi, mtu huyu aliyeambukizwa, badala yake, ataugua tetekuwanga na siyo mkanda wa jeshi.

Dalili Za Mkanda Wa Jeshi

 

Mkanda wa jeshi mara nyingi huathiri sehemu ndogo ya upande mmoja wa mwili. Vitu ambavyo vinaweza kujitokeza ni pamoja na:

. Maumivu, kuwaka moto, kufa ganzi na vitu kuchezacheza.
. Maumivu sehemu husika ikiguswa
. Malengelenge
. Kuwashwa

Pamoja na dalili hizo mtu atasikia:

. Homa
. Maumivu ya kichwa
. Hali ya kutopenda mwanga
. Uchovu

Maumivu yatetegemea sehemu ambayo vipele hivyo vimeota, yanaweza kuwa ya kawaida au makali sana. Maumivu haya
yanaweza kuchanganya sana ikadhaniwa kuwa mtu huyu ana matatizo ya moyo, mapafu au figo. Watu wengine hupatwa na
maumivu haya hata kabla ya kutokwa na vipele.

 

Mkanda wa jeshi - chanzo

 

Kikawaida, vijipele vya mkanda wa jeshi huota kama tabaka (mkanda) la malengelenge linalozunguka upande mmoja wa mwili kuanzia kifuani. Vipele vya mkanda wa jeshi vyaweza kujenga kuzunguka jicho moja, upande mmoja wa shingo au uso.

 

Tiba Ya Mkanda Wa Jeshi

 

Hadi sasa hakuna tiba maalumu kwa ajili ya mkanda wa jeshi. Linalotakiwa kufanyika ni kumpa mgonjwa dawa ya kuua virusi ili kumsaidia kupona haraka na kumpa dawa za kusaidia kuongeza kinga zake za mwili. Mgonjwa pia anaweza kupewa dawa za kupaka juu ya ngozi kupunguza maumivu.

Jee, Unasumbuliwa na mkanda wa jeshi?

Wasiliana nasi kwa ushauri na maelezo ya kina zaidi.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

 

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Namba Yako Ya Simu

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni Yako

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii