Namna Ya Kuweka Malengo Ya Biashara Ya Mtandao

 

malengo ya biashara

 

Katika mada yetu ya leo tutaona namna ya kuweka malengo ya biashara ya mtandao. Pamoja na kwamba ninasema kuwa ni somo la namna ya kujiwekea malengo ya biashara ya mtandao, ukweli ni kuwa somo hili linahusu shughuli yo yote unayotaka kuifanya katika maisha. Hakuna kitu cho chote unachoweza kukifanikisha katika maisha kama hukujiwekea malengo. Kwa hiyo mada hii inahusu uwekaji wa malengo katika mambo yetu yote tunayotaka kuyafanya katika maisha yetu.

Watu wote waliopata mafanikio makubwa wamekuwa wakijiwekea malengo na kukazana kufanya kazi kuyafikia malengo yao – wanakuwa wanajua wanapotaka kupafikia. Ni kitu rahisi sana kujiwekea malengo ingawa asilimia kubwa ya watu – yapata asilimia 95 – wanafanya shughuli zao bila ya kuwa na malengo. Si ajabu kwa hiyo kuona kuwa ni asilimia 5 tu ya watu katika ulimwengu huu ndio wenye mafanikio na wenye kipato kikubwa. Utafiti uliofanywa kuhusu kuweka malengo ulionyesha takwimu za kustaajabisha. Kwa mfano, utafiti katika vyuo vya elimu ulionyesha kuwa wanafunzi waliosoma kwa malengo walifanikiwa kuwa baina ya wale waliopata maksi za juu kabisa.

“People with goals succeed because they know where they’re going.”-Earl Nightingale

Kujiwekea malengo na kuyapitia kila wakati ndiko kunakoleta tofauti kati ya mafanikio MADOGO na mafanikio MAKUBWA ambayo mtu anaweza kuyapata. Unapoanza kuyafikiria malengo yako kama shughuli za kawaida na kama hatua za kukutoa kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine unayotoka kuifikia – utaanza kujenga ari na kuuzoea mfumo utakaokusaidia kuyafikia malengo yako. Kwa hiyo huwezi kupuuzia kuweka malengo katika biashara yako kama kweli una nia ya kufanikwa katika biashara hiyo.

“The establishment of a clear, central purpose or goal in life is the starting point of all success. An average person with average talent, ambition and education, can outstrip the most brilliant genius in our society, if that person has clear, focused goals.”
-Brian Tracy

Mpango mzuri wa kuwa na malengo ni kuyachapisha malengo yako. Ukisha kuwa na malengo yako inafaa kuyachapisha kwenye karatasi na kuiweka ukutani karibu na sehemu unayofanyia kazi zako za biashara. Unaweza kuuona kuwa ni ushauri wa kipuuzi sasa hivi ukiusoma hapa, lakini kwa sababu ambazo hazina maelezo yaliyo bayana sasa hivi, imebainika kuwa kufanya hivyo kumekuwa na uamsho wa kisaikolojia ambao huamsha nguvu za mwili zilizojificha na kuzielekeza kwenye kuyafanikisha malengo uliyoyaweka.

“Put your goals in writing. If you can’t put it on a sheet of paper, you probably can’t do what it takes to achieve the goal.”
-Unknown

Hatua ya kwanza katika kufanikisha jambo lo lote ni kuamua ni nini unachotaka kukifanya.

 

Kuamua Unachotaka Kukifanya

 

Kwanza amua ni nini unahitaji kifanyike – siyo mwakani au miaka 10 ijayo, bali mwezi huu na mwezi ujao. Katika biashara za mtandao unahitaji kuwaelezea watu ubora wa bidhaa za kampuni na ubora wa fursa ya biashara ya kampuni yako. Unahitajika kutoka na kuonana na watu. Kitu cha kwanza basi ni kupata orodha ya watu utakaowaona – iandike orodha yako vizuri. Kama ni kipato cha ziada au mshahara wako kwa mwezi, andika ni kiasi gani umepanga kukipata. Andika vizuri ni saa ngapi kwa wiki utawekeza kwenye biashara hii ili kuyafikia malengo yako na panga vizuri ratiba yako ya biashara- utafanya nini weekends, jioni au asubuhi?

“The achievement of your goal is assured the moment you commit yourself to it.”
-Mack R. Douglas

 

Kuwa Na maono

 

Kuwa na maono hapa tunamaanisha kuwa na picha katika jicho la ubongo wako ya kile kitu unachokitaka. Unatakiwa kuanza kuona kuwa umefanikiwa kukifia na kukihodhi kile kitu ambacho umekuwa ukikifikiria. Inatakiwa uanze kuamini na kujiona kuwa ni yule mtu uliyekuwa umenuia kuwa. Siyo njozi sisizo na maana kwani wanasaikolojia wanatueleza kuwa watu wanaoanza kuamini na kuwa na tabia ya mtu mwenye mafanikio, wana nafasi kubwa sana ya kufanikwa kiukweli. Tumelielezea hili kwa namna tofauti katika mada nyingine ya siri za kufanikiwa katika biashara za mtandao ambako tulitumia kanuni ya “the law of attraction”.

Weka Mkakati Wa Kufikia Malengo

 

Nyumba kabla ya kuanza kujengwa, ramani huandaliwa ikionyesha vipengele vyote vya ujenzi. Hivyo hivyo, katika biashara yako lazima ujue ni nini unahitajika kufanya ili kufikia malengo yako. Jiwekee malengo ya muda mfupi na panga tarehe za kukamilisha malengo hayo. Kwa mfano, kama umepanga kufikia lengo fulani katika miezi miwili, gawanya kipindi hicho katika wiki 8 kisha panga malengo madogo ya kufikiwa katika kila wiki katika hizo 8. Mwisho ili kufikia malengo ya kila wiki, panga ni nini utafanya kila siku ili kuyafikia malengo ya wiki. Ni kiasi gani cha bidhaa utatakiwa kuuza kila siku? Ni wanachama wangapi utawasajili na kuwafundisha ili mafanikio yao yachangie kufanikwa kwako?

“People with goals succeed because they know where they’re going.”
-Earl Nightingale

Kufikia mafaanikio inachukua muda. Jipe moyo na amini kuwa utafanikiwa tu. Usiache kujipongeza pale unafanikisha jambo ambalo linakusogeza zaidi kwenye kukamilisha ndoto zako. Mwone kiongozi wa juu yako na mweleze kuhusu mafanikio yako, kwa vyo vyote naye atakupongeza.

 

Zoezi La Kupanga Malengo

 

Katika kupanga malengo ni muhimu kutumia kanuni ya SMART ambacho ni kifupi cha maneno ya kiingereza: Specific, Measurable, Achievable, Realistic na Timely. Tutaelezea kwa kifupi hapa chini:

 

Katika kuandika malengo hakikisha kuwa unazingatia yafuatayo;

. Andika malengo Yako. Usiishie kufikiria kichwani bali andika malengo yako.
. Malengo maalum. Changanua kiundani vipengele vya malengo yako.
. Matokeo yanayopimika. Taja matokeo au matunda unayoyategemea
. Uhalisia. Weka malengo ambayo yanaweza kutekelezeka
. Muda wa kukamilisha. Jipangie muda wa kukamilisha. Kuweka muda kunasaidia kuleta msukumo wa kuchukua hatua katika muda unaotakiwa.

“You can’t hit a target you cannot see and you cannot see a target you do not have.”
-Zig Ziglar

 

 
Hatua 1

Juu ya karatasi nyeupe andika vitu unavyohitaji vifanyike. Chagua kimoja kwenye orodha hiyo kisha kizungushie duara. Kichambue na kukielezea kwa undani.

Hatua 2

Anza kujiona kuwa umefanikwa kufikia malengo yako. Tafuta machapisho yanayoelezea kitu unachokiwazia. Weka picha ya kitu hicho mahali ambapo utakiona daima. Unaweza kukamilisha mawazo na ndoto zako.

“Take up one idea and act on it. Make that one idea your life. Think of it, dream of it, and live on that idea. Let the brain, muscles, nerves, and every part of your body be full of that idea and leave all other ideas alone. This is the way to success.”
-Unknown

Hatua 3

Andika vitu vyote utakavyotakiwa kuvifanya ili kufikia malengo yako – ni vitu vingapi au zana zipi. Ni wanachama wangapi utahitaji kuwasajili na kuwafundisha, ni nini watahitaji ili mafanikio yao yawe na mchango kwenye mafanikio yako? Tengeneza ratiba ya siku, wiki, mwezi na mwaka ili kuyafikia malengo yako…. andika kila kitu unachokipanga. Ni muda wa kuwajibika!

Hatua 4

Furahia kulifanya zoezi hili. Daima fikiria ni wapi utafika…..

 

Lazima ieleweke kuwa kupanga malengo si kuyafikia malengo hayo, na, katika kuyafikia hakutakosa kuwa na vikwazo njiani. Kutokuyafikia malengo yako na vikwazo utavyokumbana nayo vinaweza kukufanya ukate tamaa na kufikiria kuwa ndoto zako hazitaweza kutimia. Inakubidi kuchukua hatua za maksudi za kupambana na vikwazo hivyo ili kuhakikisha kuwa mwisho wa siku unashinda. Katika mada yetu nyingine tunaelezea jinsi ya kupambana na vikwazo vya biashara ya mtandao.

Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo, tutafurahi kuona kuwa tumekujibu kwa wakati.

Laurian.

 

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii