Matatizo Ya Tezi Kibofu (Tezi Dume)

 

Tezi Kibofu Ni Nini?

 

Tezi kibofu au tezi dume kama ilivyozoeleka kutamka, ni kiungo ambacho ni sehemu ya mfumo wa uzazi vya mwanamme kinachouzunguka mrija wa mkojo. Tezi dume ipo katikati ya kibofu cha mkojo na dhakari na ipo mbele kidogo tu ya rektamu. Mrija wa mkojo unapita katikati ya tezi dume ukitokea kwenye kibofu na kuelekea kwenye uume, na kutoa mkojo nje ya mwili.

Tezi dume hutoa majimaji yenye kazi ya kurutubisha na kulinda shahawa. Mwanamme anapofikia kileleni, tezi dume hukamulia maji haya ndani ya mrija wa mkojo na kutolewa pamoja na mbegu kama manii (semen).
Tezi kibofu
Mirija ya vasa diferentia hutoa mbegu kutoka kwenye korodani hadi kwenye seminal vesicles. Seminal vesicles huchangia majimaji kwenye manii wakati mwanamme anapofikia kumwaga manii.

Kwa vile nimetaja kuwa tezi dume ni sehemu ya mfumo wa uzazi wa mwanamme, swali linaweza kuja; Jee, wanawake hawana tezi dume?

Wanawake wana viungo vidogo viwili vinavyoitwa Skene’s glands vilivyopo eneo la chini la mwisho wa mrija wa mkojo, karibu na eneo ambalo linasadikika kuwepo kwa G-spot. Viungo hivi hutoa majimaji yanayosaidia kulainisha tundu la mrija wa mkojo. Viungo hivi ni vidogo ukilinganisha na tezi dume ya mwanamme. Bado kuna mjadala kuhusu kazi za skene’s glands katika mwili wa mwanamke na kuhusika kwake katika tendo la ndoa. Baadhi ya watafiti wanaamini kuwa viungo hivi ndivyo vinavyotoa majimaji (“female ejaculate”), mwanamke anapofika kileleni.

 

Magonjwa Ya Tezi Dume 

 

Wanaume wote wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya tezi dume na hasa wanapofikia umri wa miaka 50. Hapa chini tutapitia baadhi ya matatizo yanayowasumbua zaidi wanaume:

 

Benign Prostatic Hyperplasia (BPH) au Prostate Enlargement

 

Hii ni hali ambapo tezi dume huongezeka ukubwa. Zaidi ya theluthi ya wanaume wote walio juu ya miaka 50 wana dalili za kuvimba kwa tezi dume. Haijajulikana kwa uhakika ni kwa nini tezi dume huwa kubwa zaidi kadri umri unavyoongezeka, lakini kukua huku si dalili ya kansa na wala hakuongezi uwezekano wa kupata kansa. Hili si tatizo kubwa sana la kiafya.

 

tezi kibofu, picha ya

 

Tezi dume iliyoongezeka ukubwa huleta msukumo juu ya mrija wa mkojo na kibofu cha mkojo hali ambayo inaweza kuathiri namna mkojo utakavyotoka.

Dalili ya tezi dume iliyovimba ni:

. Shida katika kuanza kukojoa au kuubana mkojo
. Mtiririko dahifu wa mkojo
. Kukojoa kwa shida
. Kujisikia kuwa hujamaliza mkojo
. Mkojo kuendelea kudondoka kwa muda mrefu baada ya kumaliza
. Hali ya kujisikia kukojoa mara kwa mara au ghafla
. Kuamka mara nyingi zaidi usiku kwa ajili ya kwenda haja ndogo

Kwa baadhi ya wanaume, dalili zinaweza kuwa ndogo ambazo hazihitaji tiba. Kwa wengine, zinaweza kuwa kubwa na kuathiri maisha yao. Wanaume hupatwa hofu kuwa kuvimba kwa tezi dume kunasabihiana na upataji wa kansa ya tezi dume. Hii siyo kweli kwani uwezekano wa kupata kansa wa mtu mwenye tez i iliyovimba hauzidi ule wa mtu asiye na tatizo hili la tezi.

Sababu ya kuongezeka ukubwa wa tezi dume haijajulikana, lakini wataalamu wengi wanaamini kuwa inahusiana na mabadiliko katika homoni yanayotokea umri wa mtu unapokuwa mkubwa.

Tiba ya Tezi Iliyokua

 

Tiba ya tezi hutolewa kulingana na hali iliyofikiwa. Kwa dalili ndogo au za kati, hakuna tiba maalumu inayotolewa isipokuwa uangalizi na vipimo vya mara kwa mara ili kuona maendeleo ya tezi hiyo. Utashauriwa kubadili mtindo wako wa maisha, kama kupunguza utumiaji wa kahawa na pombe, na kufanya mazoezi ya mwili. Pamoja na kubadili mtindo wa maisha, dawa zinaweza zikatolewa, zikiwemo finasteride na dutasteride. Dawa hizi huzuia ufanyaji kazi wa homoni iitwayo dihydrotestosterone na kuweza kupunguza ukubwa wa tezi dume.

Upasuaji unaweza kufanyika endapo dalili za kati au mbaya za tezi dume zimeshindikana baada ya matumizi ya dawa.

Madhara yanayoweza kutokea kutokana na benign prostate enlargement ni; maambukizi kwenye njia ya mkojo – UTI, kutokana na kuwa wadudu kama bakteria waliomo kwenye njia ya mkojo hawataweza kusukumwa nje wakati wa kukojoa, na Acute Urinary Retention (AUR) ambayo ni hali inayotokea ghafla ya kushindwa kusukuma mkojo nje ya mwili. AUR inatakiwa kutibiwa mara moja kwani kushindwa kufanya hivyo kutasababisha mkojo kurudi nyuma hadi kwenye figo na kuziharibu.

Dalili Za AUR ni:

. Kushindwa kutoa mkojo ghafla
. Maumivu ya sehemu ya chini ya tumbo
. Kuvimba kwa kibofu cha mkojo kunakoweza kuonekana kwa kujipapasa na mikono

Prostatitis

Prostatis ni tatizo ambapo tezi dume huvimba. Mara nyingine hali hii hutokana na maambukizi ya bakteria, ingawa mara nyingi hakuna maambukizi ya bakteria yanayoonekana na inashindwa kufahamika sababu ya hali hiyo kutokea.

Tofauti na kukua kwa tezi dume (BPH) au kansa ya tezi dume ambavyo huathiri zaidi wanaume wenye umri mkubwa, prostatis inaweza kutokea kwa wanume wa umri wo wote. Hasa, huonekana zaidi kwa wanaume wenye umri kati ya miaka 30 na 50.

Baadhi ya dalili za prostatis ni:

. Maumivu kwenye nyonga, viungo vya uzazi vya nje, sehemu ya chini ya mgongo na makalio
. Maumivu wakati wa kukojoa
. Kujisika haja ndogo mara kwa mara
. Kukojoa kwa shida, kama kuanza au kuuminya mkojo
. Maumivu wakati wa kukojoa manii, ambayo yanaweza kusababisha uume kutosimama au kukosa hamu ya mapenzi

Wakati mwingine unaweza kusikia uchovu, miwasho kwenye maungio ya mifupa na misuli, baridi na joto kali.

Dalili hizi kwa kawaida huanza taratibu na huja na kutoka kwa kipindi cha miezi kadhaa, ingawa wakati mwingine huweza kutokea ghafla.

 

Nini Chanzo Cha Prostatitis?

 

Kuna aina kuu mbili za prostatitis:

. Prostatitis sugu (Chronic prostatitis) – dalili hutokea na kupotea katika kipindi cha miezi kadhaa, hii ni aina ya prostatitis inayoonekana zaidi

. Prostatitis kali (Acute prostatitis ) – dalili zake ni kali zaidi na hutokea ghafla; hujionyesha mara chache, lakini huwa ni hatari na huhitaji tiba ya haraka

Acute prostatitis husababishwa zaidi na maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo (figo, kibofu cha mkojo, na mirija inayoviunganisha) wanaoingia kwenye tezi dume.

Kwenye prostatitis sugu , madaktari mara nyingi hawaoni maambukizi kwenye tezi dume na sababu za tatizo huwa hazieleweki.

 

Prostasure capsule

Dawa Ya Kutibu Tezi Dume (bofya juu ya picha kupata maelezo)

 

Tiba Ya Prostatitis

Tiba ya prostatitis hulenga kuziondoa dalili za tatizo hilo. Dawa za kuondoa maumivu kama paracetamol au ibuprofen zinaweza kusaidia kuondoa maumivu.

Tiba iitwayo alpha-blocker (kama tamsulosin) inaweza luandikwa kama kuna matatizo katika kukojoa, na hizi husaidia kulegeza misuli katika tezi dume na kwenye kibofu cha mkojo.

Mara nyingine, matumizi ya antibiotics (kama ciprofloxacin) ya wiki 4 hadi 6 huweza kuandikwa hata kama maambukizi hayakuonekana. Hii hufanywa kuona kama kutatokea mabadiliko.

Tiba ya prostatitis sugu inaweza kuleta changamoto, kwa sababu kuna elimu kidogo sana kuhusu sababu za hali hiyo. Watu wengi hupona taratibu baada ya tiba, ingawa inaweza kuwachuka miezi au miaka.

Watu wengi wenye prostatitis kali hupona kabisa katika wiki chache, ingawa mmoja katika kumi hujikuta wakipata prostate sugu baadaye.

Watu wengine hujikuta wakirudiwa na matatizo baada ya tiba, hali ambayo itahitaji tiba zaidi. Prostatitis siyo kansa na ushahidi wa kuonyesha kuwa inaweza kuongeza uwezekano wa kupata kansa ya tezi dume.

 

Kansa Ya Tezi Dume (Prostate Cancer)

 

Nchini Uingereza, kansa ya tezi dume ndiyo aina ya kansa inayoonekana zaidi kwa wanaume, kukiwa na wagonjwa zaidi ya 40,000 wanaobainika kila mwaka. Haijajulikana kinaga ubaga kwa nini aina hii ya kansa inatokea, lakini yamkini ya kupata aina hii ya kansa huongezeka na umri. Kansa hii huwapata wanaume hasa wenye umri wa zaidi ya miaka 65, ingawa wanaume waliozidi miaka 50 nao huwa kwenye hatari.

Uwezekano wa kupata kansa ya aina hii ni mkubwa pale unapokuwa na kaka na baba mwenye tatizo hili, na watu weusi wa maeneo ya Caribbean.

 

kuchunguza kansa ya tezi dume

 

Dalili za kansa ya tezi dume hufanana sana na zile za kukua kwa tezi dume na ni vugumu sana kuzitofautisha. Dalili zinaweza kuwa:

. Kujisikia kukoja mara nyingi (na hasa usiku)
. Kusikia mkojo ghafla
. Shida katika kuanza kukojoa
. Kukojoa kwa shida na kuchukua muda mrefu
. Mkojo kutiririka kwa kiwango kidogo
. Hali ya kujisikia kutomaliza mkojo

Kansa ya tezi dume huanza na kukua taratibu sana. Watu wengi hufa na kansa ya tezi dume, na si kwa sababu ya kuwa nayo. Kansa ya tezi dume, kwa hiyo, haina haja ya kutibiwa mara moja.

 

Tiba Ya Kansa Ya tezi Dume

 

Kwa wanaume wengi kansa ya tezi dume haihitaji tiba ya mara moja.Kansa ikiwa kwennye hatua za awali na haina dalili, kitakachofanywa ni kuchukua uangalizi wa karibu.

Wakati mwingine, kansa inaweza kutibiwa ikiwa kwenye hatua za awali. Tiba inaweza kuwa upasuaji wa kuondoa tezi dume, tiba ya mionzi au tiba ya homoni (hormone therapy).

Kansa nyingine hugundukia wakati ambapo tayari zimeanza kuenea. Kansa iliyoenea kwenye sehemu nyingine za mwili, mara nyingi kwenye mifupa, haiwezi kutibika na kitakachofanywa ni kuchukua hatua za kumwongezea mgonjwa muda wa kuishi na kuondoa dalili za kansa hiyo.

Tiba nyingi za kansa hufanywa kukiwa na uwezekano wa kupata madhara mengine, kama kupoteza uwezo wa jogoo kuwika au kupata hali ya mkojo kutoka wenyewe. Kwa sababu hiyo, wanaume wengi huahirisha tiba hadi wanapoona kuwa kansa hiyo itasambaa sehemu nyingine za mwili.

Kwa sababu kansa ya tezi dume hukua taratibu sana, unaweza kuishi nayo miaka mingi bila kukusababishia dalili mbaya au kuhitaji tiba. Lakini inaweza kuathiri maisha yako au kukusababishia matatizo ya jogoo kushindwa kuwika na mkojo kutiririka wenyewe.

Katika ukurasa mwingine tutajadili tatizo la kushindwa kufanya tendo la ndoa kutokana na wasiwasi.

Ndugu msomaji, usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali kuhusu mada yetu ya leo. Tunaahidi kukujibu na kwa wakati.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

404 Not Found

404 Not Found


nginx/1.10.3