Mbolea ya Green World Yapata Usajili

 

ubora wa mazao na green world

Pamoja na bidhaa za kulinda afya ya binadamu, kampuni ya Green World inatengeneza na kusambaza mbolea ya aina mpya inayotokana na mabaki ya viumbe hai. Madhumini ya kutengeneza aina hii ya mbolea ni kumlinda binadamu kutokana na kemikali za mbolea za Inorganic Fertilizers. Mbolea hiyo pamoja na kuwa na viambato vyote vinavyohitajika kwa wingi katika ustawi wa mimea (macronutrients), ina viambato vingi vinavyohitajika wa kiwango kidogo (micronutrients). Kwa kufahamu kuwa mimea huhitaji amino-acids, mbolea hii imejumuisha aina 18 tofauti za amino-acids ndani yake.

Kufahamu undani wa mbolea hii, unaweza kusoma hapa:  http://topantiagingproducts.sagalawebs.com/mbolea-ya-green-world-green-world-nutriplant-organic-plus-fertilizer/

 

Nchi kadhaa za barani Afrika zimeikubali mbolea hii baada ya wizara husika za nchi hizo kuipeleka mbolea hii kwenye maabara zao, kuifanyia vipimo na kubaini kuwa inakidhi viwangi vinavyohitajika. Nchi hizi ni pamoja na Nigeria.

 

 

mbolea ya green world
Baada ya kupita kwenye maabara za hapa nchini Tanzania, hatimaye mbolea hii imekubalika na kupewa usajili rasmi na Tanzania Fertilizer Regulatory Authority (TFRA). Mbolea hii imesajiliwa kwa jina la Nutriplant Organic Plus Fertilizer tarehe 18/09/2017 na kupewa usajili namba 0239.

 

Mbolea - green world

 

Tunawashauri watanzania kuanza kuiutumia mbolea hii kwani ina faida nyingi zaidi ya zile zinazopatikana kwenye mbolea nyingine tulizozizoea za kufukia ardhini. Faida ya zaidi ya kuongeza uwingi na ubora wa mazao yako, mbolea hii huiboresha ardhi yako badala ya kuiharibu kama ilivyo kwa mbolea nyingine.

Green World Yashiriki Maonyesho Ya 12 Ya Nchi Za Afrika Mashariki

 

Moanyesho ya rock city mall mwanza

 

Kampuni ya Green World ilishiriki maonyesho ya 12 ya nchi za Afrika Mashariki yaliyofanyika katika jiji la Mwanza kwenye viwanja vya Rock City Mall. Maonyesho hayo yalianza tarehe 25 Agosti 2017 na kwisha tarehe 3 Septemba 2017. Katika maonyeshio hayo, kampuni ya Green World iliweka bidhaa zake kwenye hema namba 28.

Maelfu ya wananchi wa Mwanza walipata maelezo kuhusu bidhaa za  na fursa ya biashara ya kampuni hii. Wananchi kwa ujumla walizifurahia sana bidhaa hizo na wengi walizinunua ili wakazijaribu.

Pamoja na kununua na kupata maelezo hayo, wananchi pia walipata kujua ofisi ya kampuni hii iliyopo mtaa wa Rufiji karibu kabisa na soko la Mirongo (soko la mkulima).

 

wanachi kwenye maonyesho ya rock city mall mwanza

 

Kampuni ilitunukiwa cheti kwa kushiriki na kuonyesha bidhaa bora katika maonyesho hayo.

 

Laurian.

 

Wanachama Wa Green World Washiriki Maonyesho Ya 41 Ya SabaSaba

 

 

maonyesho ya sabasaba

 

Wanachama wa kampuni ya Green World wameshiriki kwenye maonyesho ya biashara ya 41 yaliyofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Dar Es Salaam.  Maonyesho hayo yalianza tarehe 28 mwezi  Juni 2017 na kuisha tarehe 13 mwezi wa Julai 2107.

Wanachama hao walionyesha bidhaa za kampuni wakiwa ndani ya hema la Benjamin Wiliam Mkapa, chumba namba 21.

Wananchi kwa mamia kila siku walipata fursa ya kuelezwa kuhusu bidhaa za kampuni na fursa ya biashara inayotolewa na kampuni hiyo. Kwa ujumla, watu walizifurahia sana bidhaa hizo na baadhi walizinunua ili wakazijaribu. Wengi pia waliipenda fursa inayotolewa na kujiorodhesha ili waanze kupewa mafunzo mara baada ya kumaliza maonyesho.

 

sabsaba 2017

Video fupi ya maonyesho ya Green World – Sabasaba

 

Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi, wanachama hao wameamua kutoa fursa kama hiyo kwa wananchi wa Mwanza kupitia maonyesho ya 12 ya nchi za Afrika Mashariki (The 12th East Africa Trade Fair 2017) yatakayofanyika kwenye viwanja vya  Rock City Mall kuanzia tarehe 25 Agosti hadi tarehe 3 Septemba 2017.

Kwa hakika hii ni nafasi ya kipekee kwa wakazi wa Mwanza.

 

 

SEMINA YA PILI KIBAYA-KITETO

 

Kiteto may 2017

 

 

Siku ya jumamosi ya tarehe 6 Mei 2017, semina ya pili ya kampuni ya Green World ilifanyika mjini Kibaya- Kiteto. Semina hiyo iliandaliwa na wanachama wa Green World wa mjini humo, ndugu Thomas Mpalazi na Dorcas Manyama.  Maandalizi yalifanywa kwa ustadi mkubwa na mnamo saa 9.15 za alasiri, semina ilifunguliwa na ndugu Thomas Mpalazi.

Semina hiyo iliendeshwa kwa ushirikiano na wanachama wawili waliotoka Dar Es Salaam, ndugu Laurian Mwajombe na ndugu Hilda Mahende. Semina hiyo ilizungumzia umuhimu wa kulinda afya zetu kutokana na mazingira mabaya yanayotokana na uchafuzi wa mazingira na staili mpya za maisha zinazoendana na kiwango cha sayansi na teknolojia ya sasa. Semina hiyo pia ilitoa fursa kwa wananchi wa Kiteto kujiunga na kampuni ya Green World ili waweze kuboresha vipato vyao.

Kutokana na umakini wa waliohudhuria semina hiyo na kuwa na maswali mengi ya msingi, semina hiyo iliendelea hadi saa 12.30.

 

Hilda Kiteto may2017

 

Ndugu Hilda Mahende aliwasimulia washiriki historia yake ya mafanikio aliyoyapata katika kipindi cha miaka 3 toka alipojiunga, ambapo alielezea safari  mbalimali alizozipata kutokana na kampuni ya Green World na jinsi hamu yake ya kumiliki gari binafsi ilivyobarikiwa na kampuni hii.

Semina ilikuwa na mafanikio makubwa na wananchi walipata nafasi ya kununua bidhaa walizozihitaji. Wote kwa pamoja waliwashukuru waandaaji na waendeshaji wa semina na kuwaomba kuwa wawe na moyo wa kurudi mjini hapo kwa mafunzo zaidi.

 

Laurian.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

SEMINA KUHUSU ELIMU YA AFYA YA MWANAMKE

 

 

semia za green world ndogo

 

 

Kufuatia mahitaji ya jamii kuhusu elimu ya afya, kampuni ya Green World imaeanza kuendesha semina katika ofisi yake ya Dar
Es Salaam ili kuitoa elimu hiyo kwa wananchi. Elimu hii inatolewa BURE kabisa kila siku ya jumamosi kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana.

Jumamosi ya tarehe 8 Aprili 2017, daktari Frank alitoa elimu kuhusu afya ya saratani ya maziwa na shingo ya uzazi. Daktari alieleza kwa kutumia lugha nyepesi chanzo cha saratani hizi, namna ya kujikinga, dalili zake na tiba ambazo hutolewa pale ambapo imebainika kuwa una tatizo.

 
Baada ya maelezo ya Dokta Frank, ndugu Mwajombe, mwanachama wa kampuni hiyo ya Green World alielezea kuhusu bidhaa zitokanazo na mimea zinazotengenezwa na kampuni hiyo zinavyoweza kuzuia saratani hizi au kusaidia uponyaji wake.

 

 

picha ya laurian

 

 

 

Baada ya kipindi cha maswali na majibu, wananchi wenye matatizo walipewa fursa ya kumwona daktari huyo na kumweleza matatizo waliyokuwa nayo, ambapo walijibiwa na kupewa ushauri Bure Kabisa!

Kampuni itaendelea na mafunzo haya jumamosi ijayo ambapo wananchi wanakaribishwa kuja kwa wingi kupata mafunzo haya yanayotolewa bure kabisa.

 

Laurian.

Semina Ya Green World Kibaya- Kiteto

 

Kiteto Green World Group picture

 

Katika mfulululizo wa mafunzo kwa wageni yanayotolewa na kampuni ya Green World, mwezi March 2017, tarehe 5, semina ilifanyika katika mji wa Kibaya- Kiteto. Semina hiyo iliandaliwa na mwanachama Thomas Mpalazi wa mji huo na mwanachama mmoja, ndugu Laurian Mwajombe, alitoka Dar Es Salaam kwenda Kiteto kushirikiana naye kutoa mafunzo hayo.

Mafunzo yalianza saa 10.30 na yalifanyika katika ukumbi wa Community uliopo hapo mjini Kiteto.

Wageni kwa ujumla walionyesha hamasa ya juu ya kuijua fursa hii na walikuwa makini sana katika kusikiliza yale yaliyofundishwa. Kuonyesha kuwa walifuatilia vizuri kile kilichofundishwa, waliuliza maswali mengi na ya msingi mara baada ya kupewa nafasi ya kuuliza maswali yao.

 

semina ya Green world Kibaya-Kiteto

 

Wengi wa waliohudhuria semina hiyo, waliomba kupewa nafasi nyingine kama hii ili waweze kuwajulisha ndugu zao ambao hawakupata bahati ya kuhudhuria semina hii ya mwanzao.

 

Laurian.

Semina Ya Green World – Nzega – Desemba 2016

 

John Bwana  semina ya Nzega

 

Kutokana na kuwa watu wengi wa mjini Mwanza wameona ubora wa bidhaa za kampuni ya Green World na kuifurahia fursa ya biashara inayotolewa na kampuni hiyo, ombi la kufanya semina mjini Nzega ili ndugu zao waweze pia kunafaika lilitolewa. Mkufunzi wa kampuni ndugu Victor, aliongozana na wanachama wawili wa kampuni kutoka Dar Es Salaam, ndugu Hilda Mahende na ndugu Laurian Mwajombe, ili kufanya semina katika mji huo wa Nzega. Pamoja nao, wanachama wawili kutoka Mwanza, ndugu John Bwana na ndugu Charles Ngalula walijumuika kwenye semina hiyo.

Semina ilifanyika katika ukumbi wa Ukwala Lodge siku ya jumamosi ya tarehe 17 Desemba 2016. Mwanachama mwenyeji wa mji huo, ndugu Zuhura Salum ndiye aliyefungua semina hiyo mnamo saa 10 ya alasiri.

Baada ya ufunguzi, ndugu John Bwana kutoka Mwanza alitoa mafunzo kuhusu historia ya kampuni ya Green World, bidhaa zinazosambazwa na kampuni hiyo na umuhimu wa kutumia bidhaa za virutubishi katika ulimwengu wa sasa uliondelea kisayansi na kiteknolojia.

Katika sehemu ya pili, mkufunzi kutoka Dar, ndugu Victor, alitoa mafunzo ya jinsi mwanachama anavyoweza kunufaika kimapato na kubadili kabisa maisha yake katika kipindi kifupi tu.

 

semina ya nzega

 

Tofauti na miji mingine mingi, watu wa Nzega walijitokeza kwa wingi na kuonyesha umakini wa hali ya juu sana katika kusikiliza yale yaliyofundishwa na kudhihirisha hilo, waliuliza maswali mengi na ya msingi sana.

Mwisho kabisa, muda ulitolewa kwa wale waliopendezewa na fursa hiyo ya biashara ili waweze kujiunga, ambapo baadhi wajiunga moja kwa moja.

 

 

Mkutano Wa Green World – Gold Crest Hotel Mwanza – 26 Novemba 2016.

 

Mkutano wa Green World, Gold Crest Hotel, 26 Novemba 2016

 

Kampuni ya Green World hutoa kila aina ya nyezo na mafunzo ili kumwezesha mwanachama wake kufanya kazi zake kwa urahisi na ufanisi zaidi. Mwezi Septemba 2016, kulikuwa na mfululizo wa semina zilizofanywa na mkufunzi mkuu wa kampuni hiyo, ndugu Budiman kutoka Canada, ambaye alitembelea miji ya Morogoro, Mbeya, Arusha, Dodoma na Mwanza.

Kuanzia 24 hadi 26 Novemba 2016, wanachama wawili kutoka ofisi ya Dar Es Salaam, ndugu Hilda Mahende na ndugu Laurian Mwajombe, waliendesha mafunzo katika jiji la Mwanza wakiandamana na mkufunzi wa kampuni ndugu Victor.

Tarehe 24 Novemba 2016, mafunzo yalifanyika katika hoteli ya Vizano kuanzia saa 9 alasiri, ambapo wanachama wapya walifunzwa (New Distributor Training). Siku iliyofuata, wanachama walipewa mafunzo katika hoteli hiyo hiyo yaliyolenga kuwapa mbinu za kuzianza biashara zao kwa ufanisi zaidi (Star Training).

 

Mkutano wa Gold Crest Hotel, Mwanza

Video Ya mkutano wa Green World uliofanyika Gold Crest Hotel Mwanza.

 

Mafunzo katika mji huo wa kanda ya ziwa yalihitimishwa siku ya jumamosi, tarehe 26 Novemba 2016, ambapo watu wote walikaribishwa katika ukumbi wa Mandela wa hoteli ya Gold Crest, na maelezo ya kina ya fursa ya biashara ya kampuni ya Green World yalitolewa.

Kwa ujumla, mafunzo hayo yalikuwa na mafanikio makubwa na wananchi wa mji huo walifurahishwa sana na fursa hii. Wananchi walijitokeza toka miji ya karibu ya Geita, Kwimba, Nzega, Musoma na hata Tabora. Wengi walijiunga ili waanze kubadili maisha yao kupitia fursa hii iliyo tofauti na nyingi ambazo zinatolewa hapa nchini.

Baadhi ya wananchi kutoka kampuni nyingine zinazotoa fursa za biashara walikiri kuwa hii ilikuwa fursa ya kipekee kutokana na kuwa ilikuwa na mpango rahisi wa kukua kibiashara tofauti na kampuni nyingi ambazo hutaka mwanachama kuanza kutetea upya daraja lake kila mwezi na kutoa malipo kutokana na idadi fulani tu ya vizazi vilivyo chini yao.

 

Mkutano wa Gold Crest Hotel Mwanza

 

Kikubwa zaidi ni shuhuda halisi kuhusu utendaji kazi wa bidhaa za kampuni hii na bei za bidhaa ambazo hata mwananchi wa kawaida anaweza kuzimudu, bila kusahau uhakika wa kupata bidhaa wakiwa hapo hapo mjini Mwanza na malipo yao kila mwisho wa Mwezi.

Laurian.

Mkutano Wa Fursa Ya Biashara Ya Kampuni Ya Green World – MWANZA

 

Mkutano Wa Fursa Ya Biashara Ya Kampuni Ya Green World – MWANZA

 

Gold Crest Hotel mwanza

 

Jiulize maswali yafuatayo:

 

1. Jee, ninapenda kupata kipato cha ziada?
2. Ninapenda fursa ya kufanya biashara binafsi?
3. Ninapenda kujiajiri?
4. Nina ndoto za kumiliki gari nzuri au kuwa na nyumba nzuri au kusafiri nje?
5. Ninapenda uhuru wa muda na wa kipesa?

Kama umejibu NDIYO kwa maswali angalau matatu katika hayo, usikose kuitumia nafasi hii:

Kampuni ya Green World Tanzania itafanya mkutano mkubwa katika hoteli ya Gold Crest, iliyoko mjini Mwanza, siku ya jumamosi ya tarehe 26, Novemba 2016.

Mamia ya wakazi wa Mwaza wanategemewa kuhudhuria mkutano huu kutokana na kuwa mji huo una wanachama wengi ambao tayari wamesambaza huduma za kampuni hii na wananchi wengi kuona kuwa bidhaa za kampuni hii zinatoa matokeo mazuri sana katika kuboresha afya zao. Wengi wamaeondokewa na matatizo yaliyowasumbuakwa muda mrefu.

Mbali na kuondoa matatizo ya kiafya, wanachama hao wamejihakikishia wenyewe kuwa kampuni inatoa malipo mazuri kila mwezi kwa kazi waifanyayo.

Historia ya kukua kwa kampuni hii mjini Mwanza inaanzia Desemba 2015 ambapo kwa mara ya kwanza kampuni ilifanya mkutano wake katika hoteli ya New Mwanza Hotel, na kufuatiwa na mkutano mwingine uliofanyika April 2016 katika hoteli hiyo hiyo.

 

green world group photo mwanza

 

Septemba 2106 ndipo mkufunzi wa kampuni ya Green World kutoka Canada, ndugu Budiman alipowasili na kufanya mkutano mkubwa katika hoteli ya Gold Crest. Kipindi chote hiki wananchi wamakuwa wakijihakikishia ukweli wa mafunzo yanayotolewa na kampuni.

Ni fursa kwako wewe ambaye umekuwa ukihangaika kutafuta kitu cha kweli cha kukuwezesha kutimiza ndoto zako.

Mkutano huu utatanguliwa na siku 2 za mafunzo kwa wanachama wa zamani katika hoteli ya Vizano. Ratiba nzima ni kama ifuatavyo:

 

 

 

Tarehe 24 Novemba 2016  – Vizano Hotel – Wanachama wa zamani
Tarehe 25 Novemba 2016  – Vizano Hotel  – Wanachama wa zamani
Tarehe 26 Novemba 2016  – Gold Crest Hotel –  Watu Wote

 
Kiingilio ni BURE kabisa!

 

Kupata maelezo ya kampuni ya Green World bofya HAPA.

Semina Ya Budiman Palace Hotel – Arusha

 

Semina ya Budiman Arusha

 

Katika mfululizo wa semina za mkufunzi kutoka Toronto Canada, ndugu Budiman, ya mwisho ilifanyika siku ya jumamosi ya tarehe 1 Oktoba 2016. Semina hii ilifanyika mjini Arusha katika ukumbi wa Jumbo Hall na ilianza muda wa saa 10 jioni.

Kama ilivyotarajiwa, wakazi wa mji wa Arusha walikuja kwa wingi kumsikiliza mkufunzi huyu wa kimataifa. Semina hii ilianza kwa mkufunzi kuitambulisha kampuni ya Green World International. Alitoa historia ya kampuni hii na kutoa mifano ya watu wengi walioweza kunufaika na kampuni ya Green World katika kuboresha afya zao za kimwili na afya za mifuko yao.

Kivutio kikubwa katika semina hii ni maelezo yaliyotolewa na mwanachama wa kampuni hii ya Green World, ndugu Mbuya, ambaye ni mwenyeji wa Arusha alipoelezea mafanikio yake. Mwanachama huyo alieleza kuwa alijiunga na kampuni hii mwaka 2008 na hadi sasa pamoja na kuwa amekuwa akipata kipato kikubwa kila mwezi, ameweza kupata ziara zaidi ya sita za kwenda kupumzika nje ya nchi na zawadi za magari 15 kila moja likiwa na thamani ya Tshs. milioni 20.

Semina hii ilifungwa kwa namna ya kipekee pale sista wa madhehebu ya kikatoliki alipotoa sala iliyoambatana na wimbo mtamu aliouimba kwa lugha ya kiingereza. Kwa hakika waliohudhuria semina hii walipata mafunzo yenye thamani kubwa, kiingilio kikiwa ni BURE – kwa hisani ya mkufunzi huyo.

Mkufunzi huyo anatarajiwa kuondoka tarehe 6 Oktoba, kuelekea kwao Canada.

 

Laurian.

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii