Kifurushi Cha Green World Cha Afya Ya Mifupa Na Maungio Ya Mifupa

 

Kifurushi Cha Mifupa Na Maungio Ya Mifupa

 

 

Kwa Nini Mifupa Na Maungio Ya Mifupa Yetu Ni Vitu Vya Maana Sana Kwetu?

 

Kila wakati unapotembea, cheza muziki, kaa kwenye kiti, au mkumbatia rafiki yako, unatumia mifupa na maungio ya mifupa yako. Vinginevyo hatungeweza kusimama, kutembea, kukimbia, au hata kukaa. Mtu mzima ana wastani wa mifupa 206 iliyounganishwa na maungio ya mifupa na kuleta umbo la mwili wa binadamu.

Unavihitaji vyote kuweza kufanya shughuli zako muhimu.

 

Kulinda viungo muhimu vya ndani ya mwili.

Mifupa, misuli ya kwenye mifupa, maungio ya misuli na mifupa na maungio ya mifupa kwa pamoja hufanya kazi ya kuruhusu miondoko mbalimbali.

Uboho, unaopatikana ndani ya sehemu za wazi za mifupa mirefu na kwenye nafasi za mifupa mingine, hutengeneza chembechembe nyekundu za damu.

 

Kitatokea nini kama hutaitunza vizuri mifupa yako na maungio ya mifupa yako?

 

Osteoporosis

 

Hii ni hali ya mifupa kupungua uzito, kuwa na vijitundu na kuvunjika kirahisi.

Osteoporosis ni ugonjwa wa mifupa unaoiweka mifupa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuvunjika. Ni ugonjwa unaowapata wanawake baada ya kukoma hedhi, ingawa unaweza kuwapata wanaume, au mtu ye yote endapo madini ya calcium yatanyonywa zaidi kutoka kwenye mifupa yake na kuiacha mifupa haina nguvu. Ugonjwa huu unaweza kupunguza kwa kiwango kikubwa wastani wa mtu kuishi au ubora wa maisha yake. Kila mwaka kuvunjika kwa nyonga kunakotokana na osteoporosis kunawaacha wahanga wengi kwenye viti vya magurudumu wakiwa na ulemavu wa kudumu na wakitegea misaada.

 

Nini Kinasababisha  Osteoporosis?

 

Katika mfupa wa kawaida, kila wakati kuna ukarabati unaoendelea, hadi asilimia 10 ya ukubwa wa mfupa inaweza kuwa inajikarabati kwa wakati fulani. Mfupa unanyonywa na seli ziitwazo osteoclast  (zinazotoka kwenye uboho), na baadaye mfupa mpya unajengwa na seli za osteoblast. Uwiano mzuri kati ya kunyonywa  kwa mfupa na ujenzi wa mfupa mpya huuweka mfupa kwenye afya nzuri.

Osteoporosis ni hali inayotokea pale unyonywaji wa mfupa huuzidi ujenzi wa mfupa huo wakati mfupa ukijikarabati. Vipengele vingi vinaweza kusababisha hali hiyo kama upungufu wa homoni ya estrogen kwa wanawake (kama; kutokana na kokoma hedhi) na upungufu wa testosterone kwa wanaume, upungufu wa madini ya calcium au vitamini D, kukosa mazoezi ya mwili, matumizi ya kahawa na pombe kwa wingi huongeza kasi ya kunyonywa kwa mifupa na kupunguza kasi ya ujenzi wa mifupa mipya. Matatizo makubwa ya figo huchangia vile vile kujitokeza kwa tatizo la osteoporosis.

 

Arthritis

 

Arthritis Ni Nini?

Arthritis ni kundi la matatizo yanayoathiri maungio ya mifupa ya mwili yanayojitambulisha kwa kuleta maumivu ya mgongo, shingo, nyonga, magoti na miguu. Rheumatoid arthritis na osteoarthritis ni aina za arthritis ambazo husumbua zaidi watu, zenye dalili zinazolingana ingawa zinasababishwa na vitu tofauti. Mara nyingi arthritis imewanyima watu uhuru wao na kuondoa uhai wa wanafamilia. Kwa kawaida, watu walioathiriwa sana na arthritis, hupunguza urefu wa maisha yao kwa kiasi cha miaka 10 hadi 20.

 

Rhematoid Arthritis Na Osteoarthritis

 

Rheumatoid Arthritis

Dalili – Maumivu kwenye maungio madogo ya mifupa kama vidole, vifundo vya mikono, magoti na viwiko

Chanzo – Kinga za mwili kushambulia mikusanyiko ya seli za mwili

Kundi La Umri – Zaidi ni kundi la watu wenye umri wa miaka 20 na zaidi.

 

Osteoarthritis

Dalili – Maumivu kwenye maungio makubwa ya mifupa kama mgongoni, nyonga au magoti

Chanzo – Kuchoka kutokana na shughuli za kawaida za kila siku

Kundi La Umri – Ugonjwa wa watu wenye umri mkubwa (wazee).

 

Rheumatoid arthritis ni namna ya ugonjwa ambapo mfumo wa kinga za mwili hurudi na kuanza kushambulia mikusanyiko ya seli za mwili (tishu). Ugonjwa huu kwa kawaida hushambulia ngozi laini inayotanda juu ya maungio ya mifupa na cartilage (utando mweupe juu ya sehemu ya mwisho ya mfupa, gegedu) ambapo mwishowe mifupa ya pande zote mbili huanza kumong’onyoka.

 

Rheumatoid_Arthritis_patient-

 

Rheumatoid arthritis huathiri maungio ya mifupa kwenye vidole, vifundo vya mikono, magoti na viwiko. Ugonjwa huu huathiri pande zote mbili za viungo na huweza kusababisha ulemavu baada ya miaka michache. Rheumatoid arthritis huwapata zaidi watu wenye umri unaozidi miaka 20.

 

rheumatoid arthritis joint

 

Tofauti na rheumatoid arthritis, osteoarthritis huathiri maungio ya mifupa mikubwa kama ya mgongoni, nyonga au magoti na kusababisha mmong’oyoko wa mifupa wa pande zinazotazamana kwa kuharibu cartilage kama ilivyo kwa rheumatoid arthritis.

 

Rheumatoid arthritis joint

 

Osteoarthritis lakini hutokana na uchakavu wa maungio kutokana na shughuli za kila siku na ni tatizo hasa la watu wenye umri mkubwa.

 

Gout

 

Gout Ni Nini?

Gout (au metabolic arthritis) ni ugonjwa unaosababishwa na dosari katika uvunjaji na ujenzi wa tindikali ya purine ambapo hutokea mwongezeko wa tindikali hiyo ya purine katika damu. Ugonjwa huu unajitambulisha kwa kuleta maumivu makali kwenye maungio ya mifupa yanayojirudiarudia – wekundu, maumivu makali, uvimbe kwenye maungio ya mifupa, na unadhaniwa kuwa ndio uletao maumivu makali kuliko magonjwa mengine yote ya maungio ya mifupa.

 

gout joints

 

Mkusanyiko huu mkubwa wa tindikali ya puric huisababisha kutuama kwenye maungio ya mifupa, maeneo misuli inapoungana na mifupa, na maeneo mengine ya tishu za karibu na kuleta madhara kwenye maungio hayo. Maumivu na uharibifu wa umbo la maungio ya mifupa sehemu linaponzia dole gumba ndiyo dalili kubwa ya ugonjwa wa gout. Sehemu nyingine ambazo huathirika mara nyingi na ugonjwa huu ni pamoja na magoti, vifundo vya miguu, vifundo vya mikono, vidole, na viwiko. Gout huathiri wanaume mara tisa zaidi ya wanawake. Mara nyingi gout huwashambulia wanaume baada ya balehe na wanawake baada ya kukoma hedhi.

 

Ni nini kinachosababisha kuongezeka kwa kiwango cha tindikali ya uric?

– Sababu ya kiurithi

– Mtindo wa maisha

– Kihistoria ugonjwa wa gout ulijulikana kama “ugonjwa wa wafalme” au “ugonjwa wa matajiri.” Matumizi ya kupitiliza ya pombe, sukari, chakula chenye uwingi wa purine kama nyama nyekundu, chakula cha baharini, nyama ya viungo na bidhaa zitokanazo na maziwa, kwa kiasi kikubwa huchangia ugonjwa wa gout.

– Vitu vingine vinavyochangia ni unene, pressure kuwa juu, na figo kutofanya kazi vizuri.

 

Ni nini unachoweza kukifanya kuhusu matatizo ya mifupa na matatizo ya maungio ya mifupa (Osteoporosis, arthritis na gout)?

Matatizo ya mifupa na maungio ya mifupa hayatokei siku moja ghafla. Matatizo haya huwa mtu anayo kwa miaka mingi kabla hajagundulika. Ingawa hakuna tatizo katika haya linaloweza kuzuiwa kabisa, unaweza kupunguza madhara yake kwa kufuata mtindo mzuri wa kuishi.

  • Mazoezi ya wastani ya kila wakati yatakusaidia kuiimarisha mifupa na maungio ya mifupa yako na kuvifanya kuwa na afya.
  • Kula chakula kilichokamilika chenye uwingi wa vitamini C, D, E na madini ya Calcium, punguza kula chakula chenye purines kwa wingi kama nyama na chakula cha bahari, punguza unywaji wa pombe na vyakula vyenye sukari ya fructose (asali, matunda n.k.) na epuka unene.
  • Kumbuka kuviweka viungo vyako kwenye hali ya uvuguvugu. Mabadiliko ya ghafla ya joto la mazingira yatachochea neva zinazozunguka maungio ya mifupa.
  • Imarisha utendaji kazi wa mfumo wa figo, ambao hudhibiti mifupa kulingana na TCM.

 

Tiba

 

Ni Vipi Kifurushi cha Green World cha Afya ya Mifupa na Maungio ya mifupa kitakusaidia?

ArthroPower Capsule (au Joint Health capsule) ya Green World

Matumizi ya muda mrefu ya bidhaa hii yatasaidia kuzuia na kupunguza makali ya dalili za aina mbalimabli za arthritis kama lumbago (maumivu ya sehemu ya chini ya uti wa mgongo), scelalgia (maumivu ya miguu), arthralgia (maumivu ya kwenye maungio ya mifupa), gonitis (maumivu ya goti), kuongezeka ukubwa kwa mifupa ya uti wa mgongo kwenye maeneo ya shingo na ya chini ya mbavu, maumivu ya maungio ya mifupa ya mabega, cervical spondylosis (uchakavu wa mifupa ya uti wa mgongo eneo la shingoni) , hyperosteogeny (mifupa kukua kuzidi kiwango), sciatica (maumivu yanayoanzia kwenye nyonga hadi nyuma ya mapaja) n.k.

 

Compound Marrow Powder, Calcium Capsule na Calcium Tablet za Green World

 

Compound Marrow Powder

Compound Marrow Powder – Bonyeza juu ya picha kusoma maelezo

 

Tunza kiwango na pata nyongeza ya calcium, madini muhimu katika ujenzi na utunzaji wa mifupa na meno. Tabia hiyo itasaidia kupunguza kutokea kwa osteoporosis.,

 

 

Kidney Tonifying Capsule na Cordyceps Plus Capsule za Green World

 

Kidney Tonifying Capsule ( Men)

 

Bidhaa zote mbili zina uwezo wa kuimarisha figo ambazo zina uhusiano mkubwa na mifupa na meno kulingana na Tiba Asili Ya China, kwa hiyo zinaimarisha mifupa na maungio ya mifupa yako kwa kuboresha utendaji wa figo.

 

Pedi Ya Green World Ya Kutoa Sumu

 

Detoxin Pads

 

Kwa kubandika plasta ya Green World Detoxin pad kwenye sehemu yenye maumivu na uvimbe (usikizuie kiungo kufanya kazi), itaondoa wekundu, uvimbe na maumivu kwenye eneo la maungio lililoathirika.

 

Plasta Ya Green World Ya Kutunza Mifupa

Viungo asilia vya mimea vilivyomo ndani ya Green World Bone Care Plaster vinapenyeza ndani ya sehemu laini zilizopata madhara, vitaondoa hewa iletayo magonjwa, unyevu na baridi, vitachochea  mzunguko wa damu, vitaondoa tatizo la kusimama kwa mtiririko wa damu na kuondoa maumivu.

 

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubishi vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

Tafadhali tembelea blog yetu kujisomea mada mbali mbali zinazohusu biashara za mtandao na fursa za kufanya biashara za mtandao zinazotolewa na kampuni za Green World Tanzania . Humo unaweza kuona wasomaji wengine wana maoni gani kuhusu mada zetu tunazoziandika. Pia unakaribishwa kuona video mbali mabali zinazohusu biashara ya mtandao ya kampuni ya Green World kwenye channel yetu ya YouTube.

Kutembelea blog bofya HAPA.
Kutembelea channel yetu ya YouTube bofya HAPA.

 

Kwa mawasiliano nasi tuma tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: +255 655 858027 au +255 756 181651.

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

404 Not Found

404 Not Found


nginx/1.10.3