UZINDUZI WA WASAJILIWA – ‘FAST START TRAINING’

 

mafunzo kwa wanachama wapya

 

 Hebu tumtazame bwana Goodluck ambaye mara baada ya kujiunga na kampuni yake aliambiwa kuwa ili kupata kipato kikubwa katika kampuni yake alitakiwa  kusajili wanachama wengi chini yake. Baada ya neno hilo, Goodluck alianza kufanya kweli. Aliwaelezea watu fursa ya kampuni yake na watu wakajiunga chini yake kila siku. Aliendelea kufanya hivyo na akawa na kikosi kikubwa cha wanachama chini yake. Lakini, baadaye akashtuka kuwa hakuwa anapata bonasi ambayo ililingana na juhudi zake. Taratibu akaanza kukata tamaa. Hii inaweza kumtokea ye yote. Tatizo la Goodluck ni kusajili na kuwaacha bila ya kujua cha kufanya.

 

Baada ya kusajili inatakiwa mara moja kuwa karibu nao na kuwafundisha namna ya kuanza kujenga biashara zao.

Kampuni ya Green world inatoa bonasi ya usajili (Outstanding Sponsoring Bonus) ya asilimia 20 kwa mshauri wa nyota 2 au asilimia 41 kwa wanachama waliohitimu ushauri wa nyota 3 na zaidi pale tu mtu uliyemsajili anapoanza kufanya manunuzi ndani ya mwezi ule aliojisajli. Akijisajili akakaa kimya mwezi wa kwanza, na akanza biashara mwezi wa pili, umekosa bonasi yako ya usajili. Kwa hiyo, hakikisha mwanachama uliyemsajili chini yako ananunua angalau BV 80 ndani ya mwezi wake wa kwanza.

Kitu kingine muhimu katika urudufu ni mafunzo anayoyapata mwanachama mpya mara baada ya kumsajili. Imedhihirika kuwa unaweza kumjenga au kumpoteza mwanachama katika wiki mbili – na saa 48 za kwanza ndizo za muhimu kuliko muda mwingine wo wote.

Mwanachama anayeanza biashara mara moja kwa kawaida hubaki ndani ya biashara. Asiyeanza biashara mara moja, huanza kupata hofu, kusikia uzito na kuanza kuahirisha ahirisha mambo, vitu ambavyo vitamfanya ashindwe kuianza biashara yake.

Utafiti unaonyesha kuwa muda mzuri wa kumzindua mtu kibiashara ni katika saa 48 tangu ulipomsajili. Muda ukipita mtu huyu anaanza taratibu kupunguza mdadi aliokuwa nao mwanzo na hatimaye anasahau kabisa. Imeonekana kwamba ikipita wiki 2 baada ya kujisajlili mwanachama anakuwa amepoteza ari kwa kiwango kikubwa sana na ukipita muda mrefu zaidi, itabidi mtu huyu huyu uanze naye upya. Kwa hiyo, hakikisha unamzindua aanze kufanya biashara katika muda huo.

Mtu aliyejiunga chini yako na hafanyi manunuzi hana faida kwenye biashara yako.

Kwa mantiki hiyo hiyo, mwanachama atakayesajili watu chini yake mapema, kufanikiwa huko kutamjengea imani na kumfanya ajiamini, na kumwongezea kasi na ari ya kuendelea. Akikosa mafanikio ngalau hata madogo mwanzoni, wasiwasi na kukosa maamuzi humfanya ashindwe kuendelea kufanya biashara.

Ukisababisha wanachama waanze kufanya kazi ndani ya saa 48, utapunguza asilimia ya watakaokata tamaa.

Kwa hiyo, unahitaji kuwa na mafunzo ya uzinduzi wa haraka (fast start or quick start training) wa wanachama, ambayo yatatolewa kwa wanachama wote wapya. Unahitaji kuwafundisha yafuatayo:

1. Kutengeneza Orodha Ya Watarajiwa

Kwa sababu wengine wanakuwa wageni kabisa kwenye biashara hizi, msaidie kujenga orodha yake ya watu anaowafahamu ambao anafikiria kuwa wanaweza kuhitaji kutumia bidhaa za kampuni au kuhitaji kuisikia fursa ya biashara ya Green World. Jikumbushe namna ya kutengeneza orodha hiyo hapa:

http://sagalawebs.com/Biashara/mbinu%20za%20kuuza%20na%20kusajili%20wanachama.html

2. Kuratibu Biashara

Mwelezee faida za kuwa na mpangilio mzuri wa biashara yake na mshauri achukue hatua za awali za kuanza kuiratibu biashara yake. Baadhi ya hatua muhimu za kuchukua mara moja zimeorodheshwa hapa:

http://sagalawebs.com/Biashara/kuratibu%20biashara%20yako%20ya%20green%20world.html

3. Mawasilisho (Presentations)

Kwa sababu nyenzo kubwa ya usajili ni kutoa mawasilisho (kufanya presentation), hakikisha unampa ppt tunayoitumia kufanyia mawasilisho na kumpa mazoezi ya namna ya kufanya presentation hadi aweze. Mfundishe vitu vya kuzingatia wakati wa kufanya presentations za mtu mmoja mmoja na presentations za kundi. Siku za mwanzo, ongozana naye ili ukamsaidie kutoa fursa kwa watu aliofanya nao ahadi. Ni vizuri uusome mwongozo wa Green World kuhusu namna ya kufanya presentations na wafundishe wanachama wa chini yako kufuata misingi hiyo hiyo. Unaweza kuupata mwongozo huo hapa:

http://sagalawebs.com/Biashara/namna%20ya%20kufanya%20presentations.html

4. Kuanza Kufanya Mauzo

Mfundishe pia vitu vya kuzingati wakati wa kufanya mauzo ya mwanzo. Unaweza kumfundisha kwa kutumia ppt ifuatayo:

https://drive.google.com/file/d/0B0YMP6WNoFRFNEdHMFlyR2pXSVU/view?usp=sharing

5. Kuweka Malengo

Mfafanulie mwanachama mpya umuhimu wa kuwa na malengo katika biashara yake ili kutimiza ndoto zake. Hakikisha kuwa ameweka malengo ya muda mrefu, ya kati na malengo ya muda mfupi. Mwongozo wa namna ya kuweka malengo umewekwa na kampuni. Unaweza kuutumia ukurasa huu kwa msaada:

http://sagalawebs.com/Biashara/hatua%20za%20kufikia%20mafanikio.html

Ni kitu cha kawaida mtu kusikia woga anapoanza kukifanya kitu kigeni kwa mara ya kwanza, kwa hiyo kuwa karibu naye ili taratibu aanze kubadilika kitabia, atoe woga, ajenge imani na kuanza kukiona kuwa ni kitu cha kawaida. Kumbuka kuwa ukimzindua yeye akaanza kufanya biashara vizuri peke yake, unakuwa umejijengea mkondo wa uhakika wa mafanikio yako kwa sababu yeye pia ndivyo atakavyofanya na wengine pia vizazi vingi chini yako. Unaweza ukawa na kikosi kidogo cha watu chini yako lakini bonasi yako ikawa kubwa, tofauti na Goodluck.

Ukifanya hivi, watu uliowasajili hawapotei na utaondokana na kazi kubwa ya kusajili kila siku watu wapya, na watu wako watafanya kazi kwa sababu wameelewa nini wanatakiwa wafanye na waanzie wapi.

Kazi ya kusajili wanachama, ni kazi ya kuchagua watu mahiri watakaokuwa kwenye kizazi chako cha kwanza, utakaofanya nao biashara.  Ni watu utakaodumu nao kwa muda mrefu. Ikiwa utajitengenezea mikondo minne tu ya watu hawa mahiri, utajihakikishia kufikia ngazi ya 3* Manager kwenye kampuni yetu ya Green World – maana yake unatembelea gari yenye thamani ya dola 35,000 (milioni 70) na unaishi ndani ya nyumba yenye thamani ya dola 150,000 (milioni 300).

Jee, huoni kuwa ni muhimu kuufuata mfumo huu uliowekwa, ambao ni rahisi kuufuta, ili kujihakikishia mafanikio yako ndani ya Green World?

 

Usisite kuwasiliana nami pale unapokuwa na swali lo lote.

 

Laurian.

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii