Dawa Ya Jogoo Kushindwa Kuwika Ya Horny Goat Weed

 

uume hausimami

 

Katika ukurasa huu tutaizungumzia dawa inayoitwa Horny Goat Weed iliyotengenezwa kuwaondolea watu tatizo la jogoo kushindwa kuwika. Watu wengi hupatwa na tatizo la jogoo kushindwa kuwika (jongoo kushindwa kupanda mtungi) au kwa maneno ya mitaani uume kushindwa kusimama. Kwamza tufahamu kuwa ni jambo la kawaida hali hii kumtokea mtu katika mazingira fulani, tunasema mtu ana tatizo hili pale tu hali hii inapomtokea mtu mara nyingi au mara zote.

 

jogoo kushindwa kuwika

 

Tatizo la jogoo kushindwa kuwika (Erectile Dysfunction) ni hali ya uume wa mtu kukosa uwezo wa kusimama au kukosa kusimama kwa uimara wa kutosha ili kufanya tendo la ndoa.

Ingawa mtu anaweza kupata tatizo hili katika umri wo wote, watu wengi hupatwa na tatizo hili wanapokuwa na umri mkubwa. Takwimu za kawaida zinaonyesha kuwa asilimia 5 ya watu wenye umri wa miaka 40 na asilimia 15-25 ya watu wenye umri wa miaka 65 wana tatizo hili la uume kushindwa kusimama au kushindwa kusimama kwa uimara wa kutosha.

Tulishaona katika ukurasa mwingine wa “Jogoo Kushindwa Kuwika – Erectile Dysfunction” njia zinazotumika kupambana na tatizo hili na katika ukurasa ule tuliutaja mmea wa epimedium. Mmea huu ndio unaotumika kutengeneza dawa yenye jina la kuchekesha la Horny Goat Weed. Jina hili lilitokana na mchungaji aliyeona kuwa mbuzi wake walikuwa wakianza kuchakarika kimapenzi mara baada ya kula majani ya mmea huu. Nchi nyingi za mashariki ya mbali  kwa miaka mingi zimetumia mmea huu kuboresha viungo vya uzazi vya wanaume. Kwao mmea huu una majina mengi kama yin yang huo, barrenwort, rowdy lamb herd, randy beef grass na brain tonic of the immortals. Mmea huu asili yake ni China, Japan na Korea.

 

Horny Goat Weed Inafanya Vipi Kazi?

 

Mwanaume anapokuwa ameshikwa na shauku ya kufanya mapenzi, nitric oxide hutoa ishara kwa kemikali inayoitwa cyclic guanosine monophosphate (cGMP) ambayo huisababisha misuli laini kutulia na kupisha damu ipite kwenye mirija ya mviringo mitatu iliyopo ndani ya uume na hivyo kuufanya uume usimame.

Kunapotokea tatizo la uume kutosimama, kinachotokea ni kuwa enzyme imayoitwa protein phosphodiesterase type 5 (PDE5) inazuia ufanyaji kazi wa nitric oxide na cGMP inayofanya misuli laini kutulia ndani ya arteri. Matokeo yake ni damu kushindwa kupita ndani ya arteri ili kusababisha uume kusimama.

 

epimedium uume hausimami

 

Mmea wa epimedium ukikamuliwa hutoa Icariin ambayo huuzwa kama vidonge, unga au chai. Icariin huizuia PDE5 isifanye kazi na hivyo kuruhusu damu ijae ndani ya arteri na mirija mitatu iliyopo ndani ya uume na hivyo kusababisha uume kusimama.

Utafiti kuhusu ufanyaji kazi wa Horny Goat Weed katika mwili wa binadamu haujafanywa kwa kiwango kikubwa sana. Utafiti uliofanywa kwa kutumia panya ulionyesha kuwa panya hao waliongezewa uwezo wao na tafiti ya ndani ya vijichupa (test tubes) ulionyesha kuwa dawa hii inaizuia PDE5 kufanya kazi.

Kama mtu anatumia baadhi ya dawa zilizoorodheshwa hapa chini, anapaswa kupata ushauri wa dakatari kabla ya kutumia horny goat weed:

. Dawa za kutibu high blood pressure
. Dawa zinazoathiri mapigo ya moyo
. Dawa zinazosababisha damu kuwa nyepesi
. Dawa za magonjwa ya moyo
. Dawa za kansa za maziwa na kansa za ovari
. Dawa za kutibu thyroid

Dawa nyingine ambayo hutumika ni  Vig Power ambayo pamoja na kuondoa tatizo hili la jogoo kushindwa kuwika husaidia pia kuondoa matatizo mengine kama ilivyobainishwa katika ukurasa wa “Jogoo Kusindwa Kuwika“.

Katika ukurasa mwingine tutalijadili tatizo la kuwahi kufika kileleni na kueleza njia ambazo unaweza kuzitumia ili kuondokana na tatizo hilo.

 

Usisite kuuuliza maswali yako au kutoa maoni kuhusiana na ukurasa huu, itakuwa furaha kubwa kwetu kuweza kukujibu.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0 655 858027 au  0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Namba Yako Ya Simu

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni Yako

 

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

404 Not Found

404 Not Found


nginx/1.10.3