Ondoa Uzee

 

namna ya kuondoa uzee

Kwa Nini Mtu Huonekana Mzee?

Kupunguza uzee au kupunguza mwonekano wa uzee ni jambo ambalo watu wengi hulipenda. Watu wengi hupenda kuwa na mwonekano wa ujana. Katika somo la leo tutatazama kwa kifupi nini maana ya kuonekana mzee na kupitia njia mbalimbali za kusaidia kuondoa mwonekano huo. Karibu msomaji tuwe sote.

Kwa kifupi kuonekana mzee kunatokana na hali ya ngozi utakayokuwa nayo na afya yako kwa ujumla. Unapokuwa na umri mkubwa, karibu kila kiungo chako kitaonekana kutofanya kazi vizuri kama ilivyokuwa mwanzo na hapa ndipo tatizo la mwonekano wa uzee linapoanza. Hivyo basi, kupunguza tatizo la mwonekano wa uzee, ni swala la kujaribu kuuhudumia mwili wako ili upate yale mahitaji muhimu ambayo mwili wako unayakosa.

Ulipokuwa mchanga, wazazi wako walihangaika kukupatia virutiubisho ili kuufanya mwili wako ukue, baadae ujanani ulihangaika kuufanya mwili wako uwe na uzito unaofaa, na umri unapozidi mahitaji ya mwili wako hubadilika. Siri kubwa ni kuyajua mahitaji haya na kuutimizia mwili wako.

Kitu cha kwanza ni madini ya Calcium ambayo husaidia kufanya mifupa yako kuwa na nguvu. Bila calcium yakutosha, mwili huenda kwenye mifupa yako na kupata calcium inayohitaji. Kwa kufanya hivyo mifupa yako hudhoofika na maumivu huanza kutokea.

 

kuondoa uzee

 

Kitu cha pili ni collagen. Ngozi kama kiungo kingine chochote huzeeka. Mwili hushindwa kutengeneza collagen kwa kiwango ambacho ilikuwa ikitengeza zamani, hii husababisha ngozi yako kusinyaa na kupata mikunyanzi (wrinkles) kwa sababu hakuna mafuta ya kutosha chini ya ngozi ili kuifanya ikae vizuri.

Namna Ya Kuondoa  Uzee Au Kupunguza Uzee

Tupitie kwa juu juu njia ambazo zinatumika au nashauri uzitumie ili uondoe mwonekano wa uzee. Ili kuondoa uzee, watu wametafiti sana na wakapata njia ambazo zimeonyesha mafanikio, tena mara nyingine makubwa.

Kufanya Upasuaji (Cosmetic Surgery).

Njia hii ya kuboresha mwonekano wa mwili au kupunguza uzee inatumika sana katika nchi zilizoendelea na inaleta mafaniko makubwa sana. Sitaijadili zaidi ya kuitaja tu katika mazungumzo yetu ndani ya tovuti hii, kwani kwetu hapa bado mambo hayajafikia huko.

Chakula Kizuri Chenye Virutubisho

Nilieleza hapo juu kwamba mtu unapofikia umri mkubwa mahitaji ya mwili wako hubadilika na kwamba kujua nini unapaswa kula ndio siri kubwa ya kukufanya uonekane kijana kila wakati. Unahitaji kupata mlo wenye virutubisho vya kuusaidia mwili wako uwe na afya, nguvu  na ngozi isiyo na mikunyanzi  (wrinkles). Jielimishe kuhusu jinsi ya kupata mlo huo kutoka ukurasa niliouandika mahsusi kwa kipengele hiki cha jinsi ya kuondoa uzee kwa kupata chakula kinachosaidia kuzuia kuzeeka haraka.

Mazoezi Ya Kupunguza Uzee

Kufanya mazoezi ni kitu kinachosaidia mambo mengi sana katika mwili wa binadamu. Mazoezi pia ni kitu muhimu katika suala la kupunguza uzee. Yapo mazoezi ambayo yanafaa kwa lengo la kupunguza uzee na pia ipo njia nzuri ya kuyafanya mazoezi hayo.

 

Dawa Za Kupunguza Uzee (Anti Aging Products).

Kuna vitu vingi vilivyopo sokoni kwa lengo la kupunguza au kuondoa uzee. Zipo dawa za kunywa, cream za kupaka n.k. Soko hili la kuondoa uzee ni kubwa sana, hivyo katika kukidhi mahitaji yake, watu wasio wakweli wamejiingiza humo ili kupata fedha. Products za kweli zipo, tena nyingi tu. Lakini, products za uwongo nazo zipo tena nazo ni nyingi tu. Kuna vigezo vya kutazama wakati wa kuchagua products za kuzitumia.

 

namna ya kuondoa uzee

 

Kupata Usingizi Wa Kutosha

Jee, unapata usingizi wa kutosha? Pamoja na mambo yote tuliyoyataja hapo juu, kupata usingizi wa kutosha ni jambo muhimu ikiwa utataka mwili wako uwe na mwonekano mzuri.

 

Usisite kutoa maoni yako au kuuliza swali. Itakuwa furaha kwangu kukujibu.

Kwa maelezo zaidi na ya kina, tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au tutumie barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo: +255 655 858027 au +255 756 181651.

 

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

404 Not Found

404 Not Found


nginx/1.10.3