Kampuni Ya Green World Tanzania

 

 

green world members at beach

 

Kampuni ya Green World Tanzania ilisajiliwa rasmi tarehe 9 Septemba 2008 kwa usajili namba 67366. Kampuni hii ni moja ya matawi ya kampuni ya Green World USA yenye makao yake makuu katika mji wa Michigan huko Marekani. Kampuni  ya Green World USA ina matawi katika nchi zaidi ya 70 duniani na barani Afrika kampuni hii ina ofisi zake katika nchi zaidi ya 20. Muasisi wa kampuni hii Dr Deming Li alikuwa na nia ya kutumia mimea ya asili ili kumsaidia binadamu po pote pale alipo katika dunia hii kuimarisha afya yake. Katika kufanikisha hili alitumia matokeo ya tafiti zake binafsi na kuungana na vyuo vikuu vya tafiti vya nchini Marekani katika kufanikisha nia yake. Kampuni hii, kwa hiyo, ni ushirika kati ya nchi za Marekani na China.

Kampuni ya Green World Tanzania inashughulika na usambazaji wa bidhaa za tiba-lishe ambazo zinalenga kuboresha afya ya watoto wadogo, kuondoa matatizo ya akina mama, matatizo ya wanaume na yale ambayo humtatiza binadamu yeyote kwa ujumla. Kuna bidhaa zaidi ya 150 sasa hivi zinazosambazwa na kampuni hii. Kujua zaidi kuhusu shughuli za kampuni hii soma ukurasa wa “Kampuni Ya Kuuza Dawa Ya Green world“.

 

Ofisi Za Green World Tanzania

 

Kampuni hii ina ofisi moja tu kwa sasa hivi iliyoko katika jiji la Dar Es Salaam. Mipango ipo mbioni kupata ofisi nyingine katika miji mingine ya mikoa. Kampuni ina maduka katika miji ya Mwanza na Mbeya. Kufika ofisi ya Dar es Salaam piga 0655 858 027 au 0756 181 651 na duka la Mwanza piga 0744 266 206.

 

ofisi za green world machinga complex

 

Bidhaa Za Kampuni Ya Green world Tanzania

 

Kampuni ya Green world Tanzania inashughulika na usambazaji wa bidhaa mbalimbali vikiwa ni virutubishi vilivyotengenezwa kutokana na mimea ya asili. Virutubishi hivi vimegawanyika katika makundi makuu matano.

1. Virutubishi vya kuondoa sumu mwilini (Detoxifiers)
2. Virutubishi vyenye lishe (Replenishers)
3. Virutubishi vya kuongeza kinga ya mwili
4. Virutubishi vya kuongeza siha ya mapenzi
5. Virutubishi vya usafi binafsi                                                                                       6. Mbolea ya majimaji

 

ubora wa mazao na green world

Mafanikio Ya Watanzania Katika Kampuni Ya Green World

 

Kampuni hii imekuwa ikiwanufaisha sana watanzania walioigundua kampuni hii na kujiunga nayo. Kwa mfano, tarehe 18 Augusti 2012 katika hoteli ya Holiday Inn, watanzania walitunukiwa zawadi mbalimbali likiwepo gari, tiketi za kusafiria kwenda China na kutalii kwa gharama ya kampuni na zawadi nyingine nyingi kama kamera, oveni za microwave na TV. Katika hafla hiyo. jumla ya wanachama 60 walipata zawadi.

Mafanikio makubwa zaidi kwa watanzania yalipatikana tarehe 28 Februari 2015 ambapo jumla ya watanzania 200 walipata zawadi mbalimbali. Katika hao 4 walipata magari yenye thamani ya milioni 18 kila moja, 14 walipata tiketi za kwenda kutalii China na wengine zawadi mbalimbali. Sherehe hii ilifanyika katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel (Ubungo Plaza).

Angalia kipande cha mkanda wa video hapa chini kinachoonyesha sherehe hiyo na wanachama waliofanikiwa kupata zawadi hizo za magari.

 

Zawadi za magari

 

Ieleweke kuwa zawadi hizi ni juu ya bonus za kila mwezi wanazozipata wanachama hao kulingana na ufanisi wao wa kazi katika kampuni. Zawadi hizo ni kwa wale waliofanya vizuri kufikia viwango fulani vilivyowekwa na kampuni hiyo.

Ukitaka kujua jinsi ya kujiunga na kampuni hii soma “Jiunge Na Green World Sasa” au wasiliana nasi moja kwa moja kwa namba za hapa chini.  Kwa maelezo mafupi ya mpangilio wa biashara wa kampuni hii, pitia ukurasa wa “Karibu Kwenye Kampuni Ya Green World“.

Fursa ya biashara ya Green World, haichagui watu kwa misingi ya elimu zao, kipato walicho nacho au uwezo wa familia wanazotoka – ni fursa kwa ye yote. Kigezo kikubwa hapa ni nia ya dhati ya kubadilika kimaisha na kuwekeza juhudi katika kufanya kazi. Unapojiunga na biashara hii, unakuwa umejumuika kwenye familia ya watu wapenda maendeleo, wanaopendana na wanaosaidiana na kunyanyuana.

 

 

 

Kama unataka kujiunga na kampuni hii au kama una maswali yo yote, usisite kuniandikia kupitia promota927@gmail.com au kwa kujaza fomu hapa chini. Pia unaweza kuwasiliana nami kwa simu moja kwa moja kupitia 0655  858027 au 0756  181651 (Usitume ujumbe (SMS) tafadhali).

 

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

Tafadhali tembelea blog yetu kujisomea mada mbali mbali zinazohusu biashara za mtandao na fursa za kufanya biashara za mtandao zinazotolewa na kampuni za Green World Tanzania na Trevo Tanzania Ltd. Humo unaweza kuona wasomaji wengine wana maoni gani kuhusu mada zetu tunazoziandika. Pia unakaribishwa kuona video mbali mabali zinazohusu biashara ya mtandao ya kampuni ya Green World kwenye channel yetu ya YouTube.

Kutembelea blog bofya HAPA.
Kutembelea channel yetu ya YouTube bofya HAPA.

 

Laurian.

 

 

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Namba Yako Ya Simu

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni Yako

 

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

404 Not Found

404 Not Found


nginx/1.10.3