Biashara Ya Mtaji Mdogo: Jee, Unatafuta Kuanza Biashara Kwa Mtaji Mdogo?

 

zawadi za magari kampuni ya Green World

VIDEO YA SHEREHE YA KUKABIDHIWA MAGARI – BLUE PEARL HOTEL, UBUNGO – 28-2-2015

 

Dunia ya sasa imekuwa na mabadiliko makubwa katika ufanyaji wa biashara. Makampuni makubwa ya kutoka nchi zilizoendelea yamegundua kuwa yanaweza kufanya biashara kwa wepesi na vizuri zaidi kwa kuwaruhusu watu binafsi kunadi na kuuza bidhaa zao. Makampuni hayo katika kufanya hivyo yanaondoa gharama kubwa za kutangaza bidhaa zao kwenye vyombo vya habari na kuwaachia wanachama waliojiunga na kampuni hizo kufanya kazi hiyo. Mwanachama anatakiwa kutoa kiasi kidogo cha pesa kwa ajili ya kifurushi cha kuanzia na anunue angalau kiasi kidogo cha bidhaa kila mwezi, hivyo kumwezesha kuanza biashara kirahisi na kutoa kiasi kidogo sana cha pesa kama mtaji wa biashara yake. Hii ni aina ya biashara ya mtaji mdogo sana ambayo nitaizungumzia katika mada yetu ya leo.

Biashara ya aina hii huitwa biashara ya mtandao. Kuna maoni mengi mno kuhusu aina hii ya biashara, wapo watu wengine wakilisikia tu hili neno – biashara ya mtandao- linawachefua. Watakuambia hizi ni biashara za kitapeli au ni biashara za watu walioshindwa maisha na maneno mengine mengi. Napenda leo tujue maana ya biashara ya mtandao na ukweli wake kuhusu kumsaidia mtu anayetaka kuanza biashara ya mtaji mdogo.

 

Nini Maana Ya Biashara Ya Mtandao (Network Marketing)

 

Biashara ya mtandao ni mfumo wa biashara ambapo mwakilishi wa kampuni husika anapata mafao kutokana na mauzo yake binafsi na mauzo ya watu aliowashawishi kujinga na kampuni hiyo na kuwafundisha mfumo wa biashara yake.

Biashara za mtandao hutoa kipato endelevu (Residual Income), maana yake ni kuwa mwanachama anaendelea kulipwa pesa muda mrefu baadaye kwa kazi aliyoifanya mara moja. Kwa mfano, mwanachama aliyemshawishi mteja kununua bidhaa fulani na yule mteja akatoa oda ya kupewa ile bidhaa kila mwezi, mwanachama huyu atalipwa mwezi ule ambao mteja alinunua ile bidhaa na kila mwezi baadaye ili mradi mteja yule ataendelea kununua bidhaa ile.

Biashara za mtandao humlipa mwanachama wake kutokana na mauzo yanayofanywa na wanachama walioingizwa kwenye kampuni hiyo kwa kupita jina lake. Kampuni hizi hutofautiana, kampuni nyingine humlipa mwanachama hadi kiasi fulani tu cha ngazi chini yake, wakati kampuni nyingine hazina ukomo wa ngazi za chini ya mwanachama huyo.

biashara ya mtandao

Kama mwanachama aitwaye John atawashirikisha Amina, Grace na Doreen kujiunga na kampuni, na Amina akawashawishi Juma na Lilian, John atakuwa na wanachama watatu wa ngazi yake ya kwanza ambao ni Amina, Grace na Doreen na katika ngazi yake ya pili atakuwa na Juma na Lilian. Hivyo hivyo John ataendelea kujenga timu kubwa chini yake. Kampuni itamlipa John kutokana na juhudi zake binafsi (Linear income) na kutokana na mauzo yanayofanywa na timu iliyo chini yake (Leveraged Income).

 

 Faida Za Biashara Ya Mtandao

 

Kuna faida nyingi sana zinazopatikana kutokana na mwanachama kushiriki katika biashara za mtandao. Nitajaribu kuelezea chache hapa chini:

Mtaji mdogo: Biashara hizi huhitaji mtaji mdogo sana wa kipesa, nyingine hukuwezesha kuanza biashara kwa kiingilio kidogo sana, pengine kama Tshs 24,000/= tu na nyingine zikitaka utoe laki chache za shilingi kama kiingilio na kifurushi cha kuanzia. Hazina masharti na ukiritimba wa kutaka vitambulisho na wadhamini. Kampuni hizi zinataka tu uwe na nia ya dhati ya kufanya biashara. Unaweza kufika kwenye kampuni na muda huo huo ukajisajili na kuanza biashara.

Wewe ndiye Boss: Hizi ni aina ya biashara ambayo haina mtu wa kukufuatilia mambo yako, wewe ndiye boss wa biashara yako – ni biashara ya kujiajiri mwenyewe. Maamuzi yote na mipango yote ya kibiashara yanakuwa juu yako wewe mwenyewe, hakuna mtu wa kukusukuma au kukufokea. Utajipangia ni muda gani ufanye kazi na muda gani upumzike, ukizembea umekosa kipato na ukifanya kazi umepata kipato.

 

 

Hakuna ukomo wa kipato: Tofauti na kazi za kuajiriwa, biashara hizi hazina ukomo wa kipato, mwanachama atapata kipato kulingana na ujuzi wake wa kazi, juhudi zake za kazi na muda anaoutumia kufanya biashara yake. Wapo watu walioacha kazi baada ya kuona wanapata kipato ambacho ni mara dufu ya kile alichokuwa akipata wakati akiwa katika ajira.

Kipato endelevu: Mwanachama analipwa muda mrefu baadaye kwa kazi aliyoifanya mara moja, mara nyingine miaka mingi tu baada ya kuifanya ile kazi mara moja. Mwanachama akipata mteja mmoja wa kudumu, anakuwa amepata kipato cha kudumu, awepo asiwepo au yeye afanye kazi au asifanye kazi, kipato chake kipo pale pale. Hii ina msaada sana pale unapopata dharura au kuumwa na huwezi kushiriki kwenye biashara.

Biashara ya kurithisha: Kampuni nyingine zinamruhusu mwanachama kumrithisha biashara yake mtu anayemtaka yeye. Faida kuhusu hili na pale umri unapokuwa haukuruhusu tena kuendelea na pilikiplika za mitaani au kwa bahati mbaya mwanachama akapatwa na umauti. Mtu aliyeteuliwa ambaye anaweza kuwa mtoto wake, ataendelea kunufaika na matunda aliyopanda mwanachama aliyefariki.

 

Biashara Za Mtandao Ni Za Kweli?

 

Biashara za mtandao ni za kweli na ni halali. Nimeandika ukurasa tofauti kabisa kuhusu hoja hii kutokana na urefu wake. Hapo utaweza kuona historia ya biashara ya mtandao na watu maarufu duniani waliojihusisha na biashara hizi. Kutokana na ukweli wa biashara hii, raisi wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, alipata kuizungumzia. Raisi wa sasa hivi wa Marekani, Donald Trump ni mtu ambaye ameifanya sana akishirikiana na rafiki yake, bilionea Robert Kiyosaki. Unaweza kusoma zaidi kuhusu hili kwenye ukurasa wa “Kuna Ukweli Gani Katika Biashara Ya Mtandao?

Biashara za mtandao hazina tofauti na vitu vingine tunavyokutana navyo katika maisha, kama hukufanya utafiti wa kutosha kabla ya kujiunga, unaweza kuishia kwenye kampuni mbovu na mwisho wa siku ukawaambia watu kuwa biashara za mtandao si za kweli. Kuna makampuni ya watu wahuni ambayo yameshafika hapa nchini na kuwalaghai watu na kuna kampuni bora ambazo kila siku watu wananufaika nazo. Ukichagua kampuni yako vizuri, ukaielewa na kufanya kazi kwa juhudi, hakuna sababu ya kushindwa kubadili maisha yako. Kuna vigezo vya kuangalia kabla ya kuchagua kampuni ya kufanya nayo kazi ambavyo nilijaribu kuvielezea katika ukurasa wa “Namna Ya Kuchagua Kampuni Ya Mtandao“.

Kuchagua kampuni yako vizuri pekee hakukupi maendeleo tayari. Kampuni unayofanya nayo kazi inahitaji ipate faida kutokana na biashara yake, hakuna kampuni itakayokuja hapa kugawa hela – kamwe haitatokea. Lazima uuelewe vizuri mpango wa kibiashara wa kampuni “Compensation Plan” kwa kuhudhuria mafunzo na kuwasilikiza waliokutangulia (Upline Members). Kuna vitu vingi vya kuzingatia katika kufanya biashara yako ili upate maendeleo, lakini kwa bahati nzuri vyote ni vya kitabia na si vya kutumia pesa. Soma mada yetu kuhusu hili hapa “Siri Za Kufanikiwa Katika Biashara Za Mtandao“.

Kwa kutoa mfano tu, hapa nchini namfahamu dada mmoja ambaye alisomea ukunga (midwifery) akaacha kazi na kuanza kuuza duka la dawa pale Tabata (Dar). Akapata kusikia kuhusu kampuni moja ya kuuza madawa (Green World Tanzania) akaanza kununua dawa katika kampuni ile na kuwatibia wagonjwa wake kwa kutumia dawa za kampuni ile. Baadaye akaamua kuwa mwanachama kabisa wa ile kampuni (mwaka 2014).

 

biashara ya mtaji mdogo ya Green World Tanzania

Hilda Mahende, Tabata Kwa Bibi, Dar – 0719 609803 au 0767 609803

 

Dada yule alizingatia kanuni za biashara ya ile kampuni na katika miezi 10 tu, kipato chake hakikupungua milioni moja na nusu kila mwezi, kampuni ilimpeleka kuzuru nchi ya China kwa wiki mbili na akatunukiwa gari (Feb 2015) lenye thamani ya shilingi milioni 18. Unajua alianza biashara kwa mtaji gani? – Elfu ishirini na nne (Tshs. 24,000/=) tu.

Ni dada mpole, mcheshi anayependa kutoa ushauri kwa mtu ye yote na kwa ruksa yake nimeweka namba zake za simu endapo utapenda kupata ushauri kutoka kwake.

Umependa  kujua zaidi au kujiunga na biashara ya mtandao ya kampuni ya Green World? Wasiliana nasi kwa njia moja uipendayo kati ya hizi hapa chini:

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au  0756 181651.

 

 

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Namba Yako Ya Simu

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni Yako

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

404 Not Found

404 Not Found


nginx/1.10.3