Maumivu Ya Mifupa

 

 

Katika mada ya leo tatazungumzia baadhi ya matatizo au magonjwa yanayosababisha maumivu katika mifupa. Kwa sababu matatizo yanayoleta maumivu katika mifupa ni mengi mno, tutajaribu kuzungumzia yale tu amabayo huwapata watu wengi zaidi. Magonjwa ya mifupa hutokana na kukua kusiko kwa kawaida kwa mifupa au dosari katika kukua huko kwa mifupa. Dosari hizi huweza kusababisha mifupa isiwe na nguvu au maumivu katika maungio ya mifupa (joints). Kwa kawaida mifupa ya binadamu huanza kupungua uzito wake umri wa mtu unapoanza kuzidi miaka 20, lakini magonjwa au upungufu wa madini ya calcium na vitamini D katika lishe husababisha mifupa hiyo kupungua uzito na uimara wake kwa kasi zaidi.

Baadhi ya magonjwa ya mifupa ambayo huwasumbua watu wengi zaidi ni:

Osteoporosis: Ugonjwa huu ni hali ambapo mifupa ya mtu inakosa viungo muhimu vya kuunda mifupa na kusababisha mifupa yake ikose uzito wa kutosha na kuifanya iwe myepesi kuvunjika. Mtu mwenye tatizo hili huweza kupungua urefu, huweza kupata maumivu makali na kubalilika katika ukaaji au utembeaji wake. Ugonjwa huu huweza kusababisha ulemavu wa kudumu.

Mtu hupata ugonjwa huu kutokana na:

  •  kuwa na umbo dogo au kuwa mwembamba
  • kuzaliwa katika familia yenye historia ya ugonjwa huu
  •  kuwa amekoma hedhi na hasa anapokoma hedhi mapema mno
  • kuwa mwanamke mwenye matatizo ya kupata siku zake
  • matumizi ya madawa hasa yale ya kutibu asthma, matatizo ya           thyroid n.k.
  • kukosa madini ya kutosha ya aina ya calcium katika mlo
  • kutokufanya mazoezi ya mwili
  • kuvuta sigara
  • kutumia pombe kwa wingi

Ugonjwa huu huendelea kukua taratibi bila kuonyesha dalili zo zote hadi mgonjwa atakapovunjika mfupa. Ni ugonjwa ambao hadi sasa hauna tiba kamili lakini unaweza kupunguzwa kwa kutumia madini ya calcium na vitamini D na kufunya mazoezi ya viungo.

 

maumivu ya mifupa

 

Paget’s Disease: Ugonjwa huu husababisha mifupa kukua na kuwa mikubwa kuliko kawaida. Mifupa hii huwa haina uimara. Mgonjwa huweza kupata maumivu na matatizo mengine ya kiafya. Ugonjwa huu hutibika kwa dawa za hospitalini, kwa kufanyiwa upasuaji na mazoezi ya kimwili.

Osteogenesis Imperfecta: Huu ni ugonjwa wa kurithi ambapo mifupa ya mgonjwa huweza kuvunjika kiurahisi kabisa. Pamoja na kuwa na mifupa dhaifu mgonjwa anaweza kupata tatizo la kutosikia vizuri, kuwa na meno dhaifu na kupinda uti wa mgongo.

Bone Cancers: Kansa ya mifupa inaweza ni ya kuanzia ndani ya mifupa au ile iliyoanzia katika viungo vingine vya mwili na kusambaa hadi kwenye mifupa, kwa mfano, kansa ya mapafu, kansa ya maziwa au kansa ya prostate. Kuna aina nyingi za kansa ambazo huanzia ndani ya mifupa kama leukemia, osteosarcoma, Ewing sarcoma, malignant fibrous histiocytoma na chondrosarcoma.

Rickets: Huu ni ugonjwa wa watoto wadogo ambao husababisha mifupa kuwa dhaifu na inayoweza kuvunjika kwa urahisi. ni ugonjwa ambao unaambatana na maumivu ya misuli. Chanzo cha ugonjwa huu ni ukosefu wa vitamini D kwa hiyo ni ugonjwa unaoweza kuzuilika kiurahisi.

ugonjwa wa rickets

Osteomyelitis: Osteomyelitis ni ugonjwa unaotokana na bacteria ambao hushambulia mifupa. Ni tatizo ambalo huweza kutokea ghafla au likawa la muda mrefu. Tiba ya ugonjwa huu ni kutumia antibiotics na kama hali ni mbaya sana ni kufanya upasuaji kuondoa kile kipande kilichoshambuliwa.

Magonjwa mengine ni kama Osteomalacia, Acromegaly, Perthes’ Disease, Fibrous Dysplasia n.k.

 

Katika mada nyingine tutazungumzia magonjwa ya maungio ya mifupa (joints) ambayo kwa ujumla huitwa Arthritis ambapo tatajadili aina za arthritis na kupitia zile ambazo husumbua zaidi watu kwenye jamii yetu. Usisite kutoa maoni yako au kuuliza swali lo lote kuhusiana na mada hii, tutafurahi sana kupata mchango wako na kukujibu.

 

Kwa maelezo zaidi na ya kina, tuma ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au tutumie barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo:  0655 858027 au 0756 181651.

 

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Namba Yako Ya Simu

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni Yako

 

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

404 Not Found

404 Not Found


nginx/1.10.3