Chunusi: Chanzo, Aina Na Jinsi Ya Kuzuia Chunusi

 

chunusi nodules

 

Chunusi ni ugonjwa wa ngozi unaowapata watu wa mataifa yote na wa umri wote. Ugonjwa uliozoeleka zaidi ni ule unaowapata vijana wakiwa kwenye umri wa balehe. Zaidi ya asilimia 70 ya vijana wa umri huu hupata chunusi. Chunusi huwapata vile vile watu wenye umri mkubwa na, vichanga wengine hupata chunusi kutokana na mama zao kuwarithisha homoni kabla tu ya kuzaliwa. Ukurasa huu utajadili chanzo cha chunusi katika mwili wa binadamu, aina za chunusi na hatua zinazoweza kuchuliwa ili kuepukana na chunusi.

Katika mwili wa binadamu, chunusi huonekana zaidi maeneo ya usoni, mgongoni, kifuani, mabegani na shingoni. Kutegemeana na uwingi wa chunusi hizo, mwathirika huweza kunyanyasika kimawazo na kupata makovu juu ya ngozi yake. Kuna dawa za kutibu chunusi ingawa ni ugonjwa unaoweza kujirudiarudia. Chunusi huondoka polepole sana na wakati mwingine chunusi mpya huanza kujitokeza kabla nyingine kupona kabisa. Ni ugonjwa unaotakiwa kupewa tiba ya mapema ili kuepuka kupata madhara ya kudumu.

 

Chanzo Cha Chunusi Ni Nini?

 

Chunusi (Acne Vulgaris) ni ugonjwa unaohusisha tezi za kuzalisha mafuta (oil glands) zilizopo chini ya ngozi kwenye sehemu ya vijitundu vya vinyweleo (hair follicles). Picha hapa chini inaonyesha muundo wa kitengo kimoja cha kinyweleo (pilosebaceous unit).

 

umbo la kinyweleo

 

Kila kitengo huundwa na kijitundu cha kinyweleo (hair follicle), tezi ya mafuta (sebacious gland) na kinyweleo (hair). Vijitengo hivi vinapatikana sehemu zote za mwili isipokuwa maeneo ya viganja vya mikono, kwenye nyayo, sehemu za juu za miguu na kwenye midomo. vitengo hivi hupatikana kwa wingi usoni, shingoni na kifuani.

Tezi za mafuta hutoa sebum ambayo huvisaidia ngozi na vinyweleo kutokuwa vikavu.

Mtu anapokuwa kwenye balehe, tezi hizi za mafuta hupanuka na kuwa kubwa na hutoa sebum (aina ya mafuta) kwa wingi zaidi, hali inayochangiwa na kuongezeka kwa homoni za androgens. Baada ya umri wa miaka 20, utengenezaji wa sebum hupungua.

Sebum hii iliyotengenezwa na sebacious gland huchanganyikana na seli za ngozi zilizokufa na kwa pamoja hutolewa nje ya mwili kupiti vijitundu vya vinyweleo. Vijindu hivi vikijaa mchanganyiko huo, humwaga ziada juu ya ngozi na na kuifanya kuwa laini. Hali hii ikiendelea bila dosari, ngozo hubaki laini na yenye afya.

Chunusi za aina mbalimbali hutokea pale kunapotokea dosari katika ufanyaji kazi wa vijitengo hivi vya kwenye ngozi. Tutaelezea dosari mabilimbali zinazoweza kutokea, na nini kitaonekana juu ya ngozi ya mtu huyu. Kuna dosari ambazo zitaleta vijipele vya kawaida na nyingine kuleta mapele makubwa, mara nyingine yaliyotunga usaha.

Kuna hali mbalimbal ambazo zinaweza kutokea kwa chunusi kwenye ngozi. Kwa kawaida chunusi huanza kwa sababu zifuatazo:

. Seli za ngozi zilizokufa (corneocytes) hugeuka na kuwa nzito na katika kutembea kwenye kijitundu cha kinyweleo
huganda badala ya kutoka nje ya tundu

. Seli nyingi za ngozi kutokea sehemu ya juu ya tundu kuliko sehemu ya chini ya tundu la kinyweleo

. Uzalishaji wa mafuta (sebum) kuongezeka

Kuongezeka kwa vitu hivi ndani ya kijitundu cha kinyweleo, huziba sehemu ya juu ya kijitundu na kuzuia vitu hivi visitoke nje, hali ambayo kiutaalamu huitwa microcomedone. Bakteria waitwao Propionibacterium acnes, huishi ndani ya vijitundu hivi vya vinyweleo na hutumia sebum kama chakula chao. Kuongezeka kwa sebum hufanya bacteria hawa kuongezeka ndani ya vijitundu hivi lakini hawaleti madhara yo yote kwa sababu hadi sasa wanaishi ndani ya vijitundu tu – hawana madhara kwenye ngozi.

 

Whitehead – Closed Comedone

chunusi whitehead

 

chunusi whiteheads

 

Kuongezeka kwa sebum na seli zilizokufa kutajaza vijitundu vya vinyweleo na kuufanya mchanganyiko huu kuwa mzito. Endapo vijitundu vitakuwa vidogo au vimeziba hali inayoitywa closed comedone au whitehead itajitokeza.

Kuendelea kujazana kwa mafuta kutasababisha eneo linalozunguka kijitundu hicho kuvimba. Whiteheads huweza mara nyingine kuambatana na mashambulizi ya bacteria – P.acnes bacteria – kutegemeana na kama bakteria hao waliweza kushambulia seli zinazolizunguka tundu.

 

Blackhead – Open Comedone

 

chunusi blackhead

 

chunusi blackheads

 

Kama katika kuongezeka huku kwa sebum na seli za ngozi zilizokufa, kijitundu cha kinyeweleo kitakuwa wazi, hali inayoitwa open comedone au blackhead itatokea.

Kuzidi kuongezeka kwa mafuta kutoka sebacious glands, kutalifanya eneo linalokizunguka kijitundu cha kinyweleo kuvimba. Blackheads zinaweza kuambatana na mashambulizi ya bakteria wa P.acnes endapo wataweza kushambulia eneo linalozunguka kijitundu cha kinyweleo.

 

Chunusi – Pimple

 

chunusi papule

 

chunusi pimples

 

Kuzidi kuongeka kwa sebum kutoka kwenye sebacious glands na seli zilizokufa kutajenga msukumo kwenye seli zinazokizunguka kijitundu cha kinyweleo. Msukumo ukiwa mkubwa wa kutosha, kuta za kijitundu hupasuka na mafuta kupenya kwenye ngozi ya karibu. Kwa sababu mafuta haya yana uwingi wa bakteria wa P.acnes, ngozi hii inayozunguka kijitundu hushambuliwa na bakteria hawa na kuifanya ngozi hiyo kuwa na uvimbe nwekundu (pimples). Hali hii
kiutaalamu huitwa inflammatory papule.

 

Chunusi – Pustule

 

chunusi pustule

 

chunusi - pustules
Chunusi za aina ya pustule hutofautiana na pimples au papules kwa kuwa na chembechembe nyeupe za damu (usaha). Wakati mwili unapambana na bakteria wa P.acnes, chembechembe nyeupe za damu ambazo ni sehemu ya kinga za mwili, hujazana na kutunga usaha katika vijitundu vya vinyweleo. Kwa sababu ambazo bado hazijafahamika vizuri kisayansi, chunusi nyingine hutunga usaha wakati nyingine hazitungi.

 

Chunusi – Cyst (Nodule)

 

chunusi nodules

chunusi -  nodules

 

Wakati mwingine mafuta na bakteria wanaposambaa kwenye ngozi inayozunguka kijitundu, maambukizi husambaa eneo kubwa na huelekea chini zaidi ndani ya ngozi na kusababisha vijinundu (nodules or cysts) na makovu. Vijinundu hivi huleta maumivu makali na haviponi kwa urahisi.

 

Mambo Gani Huongeza Uwezekanao Wa Kuwa Na Chunusi?

 

Chunusi ni kitu cha kurithi, endapo wazazi wako walikuwa na chunusi basi uwezekano wa wewe kuwa na chunusi ni mkubwa sana. Chunusi pia hushambulia watu wakiwa katika umri wa barehe na ujanani wakati homoni kama za testosterone zinaongezeka mwilini. Wanawake hupata chunusi zaidi wanapofikia umri wa kuanza kupata siku za mwezi. Wanawake wengi huota chunusi siku chache kabla ya kuingia mwezini.

Kuna vitu vinavyoweza kuchangia kupata chunusi:

. Kuvaa vitu vinavyobana, vinavyosugua juu ya ngozi, kama, helmets, mikanda ya sidiria, sweta za kukaba shingo n.k.

. matumizi ya vipodozi vya ngozi au nywele vyenye vitu vibaya

. Kuosha uso mara nyingi au kuusugua uso kwa nguvu. Matumizi ya sabuni zisizofaa au maji ya moto sana huongeza makali ya chunusi.

. Kuwa na msongo wa mawazo mara kwa mara.

. Kugusa uso mara kwa mara.

. Kuvuja jasho.

. Kuacha nywele zining’inie juu ya uso na kuufanya uso kuwa na mafuta zaidi.

. matumizi ya baadhi ya madawa.

. Kufanya kazi kwenye mazingira ya mafuta au kemikali kwa muda mrefu.

 

Tiba Ya Chunusi

 
Tiba ya chunusi itazingatia zaidi aina ya chunusi iliyotokea. Lakini kwa ujumla tiba hizo zinalenga kufanya yafuatayo:

. Kupunguza kunata kwa seli za ngozi zilizokufa ili ziliweze kutiririka kiurahisi na kutoka nje ya vijitundu vya kwenye ngozi. Lotion kama salicylic acid 2% zinaweza kutumika.

. Kuua bakteria wa P.acnes kwa kutumia antibiotics za aina mbalimbali, kwa mfano, benzoyl peroxide.

 

Katika mada nyingine tutazungumzia mikunyanzi ya juu ya ngozi na jinsi ya kuipunguza mikunyanzi hiyo. Tafadhali usisite kuuliza swali lo lote ulilo nalo au kutoa maoni yako kuhusu mada hii. Tutafurahi sana kuona tumeshiriana na wewe.

 

Unasumbuliwa Na Chunusi? 

 

Wasiliana nasi kwa njia yo yote uipendayo kati ya hizi hapa chini ili tuweze kukusaidia.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

 

 

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Namba Yako Ya Simu

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni Yako

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

404 Not Found

404 Not Found


nginx/1.10.3