Mazoezi Ya Kegel

 

kukojoa upesi

 

Katika ukurasa mwingine katika tovuti yetu tulijadili tatizo la kuwahi kufika kileleni au kumaliza tendo la ndoa upesi. Tuliona kuwa kuna dawa unazoweza kutumia kupunguza tatizo hili na tulitaja kuwa kuna mazoezi ambayo unaweza kuyafanya yakakusaidia kuongeza muda wako wa kufika kileleni. Leo tutazungumzia mazoezi ya  Kegel ambayo yana manufaa mengi kwa mwanamme (na mwanamke pia). Mazoezi haya yamepewa jina hilo baada ya mtu wa kwanza kuyaelezea, Arnold Kegel mwaka 1948.

 

 Faida Za Kufanya Mazoezi Ya Kegel

 

Mazoezi ya Kegel yamethibitishwa kusaidia kuondoa matatizo ya kutokwa na mkojo bila kukusudia hali ambayo kwa wanawake hujidhihirisha zaidi baada ya uzazi. Kwa wanaume mazoezi haya husaidia tatizo la kuwahi kufika kileleni au kwa maneno mengine kumaliza tendo la ndoa upesi. Yanawasaidia pia wanaume kuwa na uume unaosimama kwa nguvu zaidi (increased size and intensity of erections). Mazoezi haya huzisaidia jinsia zote mbili kupata raha zaidi wakati wa kufika kileleni (intensity of orgasms). Kwa wanawake, huwasaidia kukaza misuli inayozunguka uke, kitu ambacho ni muhimu sana hasa baada ya tendo la uzazi.

 

 Mazoezi Ya Kegel Ni Nini?

 

Ni mazoezi yanayofanywa kwa kurudiarudia kwa kukaza (kubana) na kuachia misuli inayopo kwenye uvungu wa pelvis. Misuli hii huitwa misuli ya pubbocoxygennus (PC) na ndiyo misuli inayofanya kazi ya kudhibiti ufanyanyaji kazi wa dhakari. Mazoezi haya pia huitwa Pelvic Floor Exercises au PC exercises. Misuli hii hutanda eneo lililo katikati ya miguu kuanzia chini ya kinena hadi unapoishia uti wa mgongo kwa upande wa nyuma.

 

misuli ya pubococcugeus

 

 Namna Ya Kufanya Mazoezi ya Kegel

 

Mazoezi haya hufanywa kwa namna nyingi na mara nyingine yakiambatana na vifaa maalumu. Hapa naelezea mazoezi rahisi yenye lengo kuu la kukusaidia kuimarisha misuli yako usitokwe na mkojo ovyo na uweze kuongeza muda wako wa kufika kileleni.

Ukiwa umesimama au umekaa, legeza viungo vyako vyote vya mwili, usikaze makalio wala misuli yako ya miguu au ya tumbo. Kaza misuli yako ya uvungu wa sehemu nyeti kama vile unazuia mkojo usitoke. Ukiwa bado umeikaza misuli hiyo, hesabu sekunde 3 hadi tano kisha ilegeze (ukiweza kuhesabu sekunde zaidi ni vizuri zaidi). Fuata ratiba uliyopewa hapa chini kuendelea na mazoezi yako. Tazama video hapa chini kwa mfano wa kufanya mazoezi haya:

 

Wiki  1  mikazo 30 kwa siku

Wiki  2  mikazo 30 kwa siku – mara mbili kwa siku

Wiki  3  mikazo 45 kwa siku – mara mbili kwa siku

Wiki  4  mikazo 60 kwa siku – mara mbili kwa siku

Wiki  5  mikazo 75 kwa siku – mara mbili kwa siku

Wiki  6  mikazo 90 kwa siku – mara mbili kwa siku

Wiki  7  mikazo 90 kwa siku – mara mbili kwa siku ongeza mikazo 30

Wiki  8  mikazo 90 kwa siku – mara mbili kwa siku ongeza mikazo 45

Wiki 9 mikazo 90 kwa siku – mara mbili kwa siku ongeza mikazo 60

Wiki 10 mikazo 90 kwa siku – mara mbili kwa siku ongeza mikazo 75

Wiki 10 mikazo 90 kwa siku – mara tatu kwa siku

 

 Video Ya Mazoezi Ya Kegel

 

Mazoezi Ya Kegel

 

Kumbuka kuwa  inabidi uyafanye mazoezi haya kwa muda mrefu kidogo, lakini manufaa yake ni makubwa mno katika kukuwezesha kumudu kufanya tendo la ndoa kwa muda mrefu zaidi na kukufanya usikie raha zaidi unapofika kileleni. Ili uweze kupata maelezo ya kina ya tatizo la kuwahi kufika kileleni, pitia ukurasa huu tuliouandika katika mada nyingine.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo:  0655 858027 au  0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

 

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni

 

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

manmeds.top | 502: Bad gateway

Error 502 Ray ID: 3f2969cf30aea627 • 2018-02-25 08:49:47 UTC

Bad gateway

You

Browser

Working
Indianapolis

Cloudflare

Working
manmeds.top

Host

Error

What happened?

The web server reported a bad gateway error.

What can I do?

Please try again in a few minutes.