Ubora Wa Kampuni Ya Green World Tanzania

 

ofisi za green world machinga complex

 

 

Kampuni ya Green World Tanzania ni moja ya makampuni mengi ya mtandao ambayo yameingia hapa nchini kwetu Tanzania. Kampuni hii ilisajiliwa hapa kwetu mwaka 2009 na tangia hapo kuna baadhi ya watanzania ambao wameshanufaika sana na kampuni hii. Mimi nafikiri niseme neno moja kwamba watanzania bado hawajaielewa vizuri kampuni hii na kwa hiyo hawajaitumia fursa hii ipasavyo. Mimi binafsi naamini kuwa hii ni fursa ya kipekee kama mtu ataielewa vizuri. Katika mada hii nachambua kwa nini nafikiri hii ni fursa iliyo bora kuliko nyingi zilizopo na kueleza machache ambayo wengi hawayajui kuhusu fursa hii ili mtu aweze kutoa maamuzi yaliyo sahihi kuhusu kujiunga na fursa hii.

 

Kwa nini Green World Ni Fursa Bora Ya Biashara Tanzania

 

Kwa sababu si kila fursa ni bora kwa kila mtu na kwa kila nchi, tuangalie kwa nini Green World ni bora kwa walio wengi waishio Tanzania. Hapa chini ni sababu za msingi kwa hoja yangu:

 

coco beach

 

Kianzio au Kifurushi cha Kuanzia Green World Tanzania: Kampuni hii haina kifurushi cha kuanzia bali ina kiingilio kidogo cha Tshs 35,000/= tu. Kwa kulipa kiingilio hiki utakuwa tayari mwanachama wa kampuni ya Green World Tanzania, utapewa kadi yenye namba ya uanachama wako wa kampuni, CD ya kuona shughuli za kampuni kimataifa na kitabu cha orodha ya bidhaa za kampuni na maelezo ya mpango wa malipo wa kampuni. Kadi utakayopewa ni ya kimataifa, maana yake ni kwamba po pote duniani utakapoionyesha kwenye ofisi ya Green World, utapokelewa na kupata huduma zote muhimu. Unaweza sasa kuanza kuchagua bidhaa unazozipenda na kuzinunua muda wo wote. Utauziwa kwa bei ya uanachama ambayo ni asilimia 20 pungufu ya bei ya reje reja. Kila mmoja wetu anamudu kutoa kiingilio hiki, hili sina shaka nalo.

Bidhaa zinazohitajika na jamii na kuuzika: Bidhaa za kampuni hii ni virutubisho vya mwili vya kusaidia kuweka afya za jamii kwenye hali bora au watu kuondoa matatizo mbalimbli ya kiafya. Kampuni hadi sasa ina bidhaa za aina tofauti zaidi ya 100. Bidhaa ni nyingi kwa ajili matatizo ya kipekee ya watoto, akina mama, wanaume na binadamu kwa ujumla. Bidhaa hizi zimethibitishwa na waliozitumia kuwa ni bora katika ufanyaji wake wa kazi na watu waliotumia huwaambia ndugu zao pia kuhusu ubora wa bidhaa hizi.

 

ushuhuda wa kupata mtoto green world

 

Kwa vile kila siku watu wanahitaji kuboresha afya zao, soko ni kubwa sana na kila siku linazidi kupanuka. Hapa nchini Tanzania pekee, kuna shuhuda nyingi za watu waliohangaika kwa miaka mingi na kupona kupitia bidhaa zetu.

 

Bei za Bidhaa za Green World Tanzania: Bei za bidhaa za kampuni hii zimepangwa hivi kwamba kila mwananchi aweze kuzimudu na kuifanya biashara yako kuwa na wateja wengi wa kununua bidhaa zako .

Ulipaji wa kampuni ya Green World Tanzania: Kampuni humlipa mwanachama mafao yake kila mwezi.

Mpango Wa Biashara (Compensation Plan). Mpango wa biashara wa Green World umeandaliwa kuwa rahisi kueleweka kwa kila mtu na rafiki kwa watu wa rika na viwango mbalimbali vya kipesa. Umeandaliwa ili mtu aweze kupanda daraja kiurahisi na kwa kila tendo analolifanya. Kampuni haina kumteremsha mtu daraja alilofikia, hata kama kwa bahati mbaya mwanachama alishindwa kufanya biashara kwa miezi kadhaa, akirudi ataendelea kwenye ngazi ile ile alipoachia.  Green World haina ukomo wa vizazi chini yako vitakavyochangia kwenye kipato chako hivi kwamba unaweza kupata mafao kutoka kwenye kundi kubwa sana la wanachama chini yako (Leveraged Income).

Kampuni ya kuaminika: Kampuni hii ipo kwenye biashara kwa miaka mingi sasa na ipo katika nchi zaidi ya 70 ulimwenguni. Hii ni uthibitisho tosha kuwa hii si kampuni ya kuja kuchukua hela za watu na kutoweka kama yalivyofanya baadhi ya makampuni. Ukijiunga na Green World, unajenga biashara ya kudumu. Kupata ushahidi zaidi unaweza ku-google www.world-food.com.

 

green world members at beach

 

Mfumo Wa Biashara Wa Geen World Tanzania

 

Kampuni ya Green World Tanzania imejengwa kwa kutumia mfumo wa 3*3 Matrix maana yake ni kwamba ukijiunga unaweza kuchagua kunufaika na bonasi zinazotokana na kazi zinazofanywa na watu wengine kwa  kuwashawishi angalau watu watatu kujiunga chini yako. Hao watatu wa mwanzo ni ngazi yako ya kwanza ya mtandao wako unaoujenga. Hao watatu wa chini yako utawalea na kuwafunza wawashawishi angalau watu watatu kila mmoja. Wakifaulu kufanya hivyo, wewe utapanda ngazi na kupata mafao zaidi. Wale tisa nao inabidi wapate watu watatu watatu kila mmoja ndipo utakapopanda ngazi zaidi na kupata mafao makubwa zaidi. Kampuni hii haina ukomo wa ngazi za chini yako, maana yake haina ukomo wa mapato – ukomo wa mapato hapa ni ukomo wa juhudi zako.

 

Ngazi Za Wanchama Wa Green World Tanzania

 

Kampuni ya Green World ina ngazi kwenye hadhi za Consultants, Managers, Directors na ngazi ya juu kabisa ni Honorary Chairman. Unapojiunga kwa kutoa kiingilio chako, tayari unakuwa kwenye ngazi ya kwanza ya Consultants, utaitwa 1*C (First Star Consultant). Utaendelea kupanda ngazi hadi kufikia 8*C.

Ukifanya mambo yako vizuri utaingia kwenye hadhi nyingine ya u-Manager. Hapa kuna One-Star manager hadi Three-Star Manager.

Baada ya ngazi hizi za mameneja unaingia kwenye hadhi ya Directors ambapo unaanza na gazi ya One-Star Director na kuishia kwenye ngazi ya Five-Star Director.

Ngazi ya juu kabisa ya kampuni ya Green World Tanzania ni Honorary Chairman.

 

Mafao Ya Green World Tanzania

 

Sasa tulizungumzie lile lililokufanya uingie kwenye internet na kuanza kupekua, yaani kampuni ya mtandao ambayo ni nzuri kujiunga nayo-Mafao au Malipo na marupurupu. Najua hili ndilo ulilokuwa unalitafuta muda wote, kwani sababu kubwa ya kuhangaika na makampuni haya ni kujiongezea kipato au kupata ajira na kubadili maisha. Kampuni ya Green World itakupa si nyongeza ya kipato tu bali itakupa ajira ya kudumu ukipenda. Ni biashara ya kukupa shughuli ya kudumu isiyo na ukomo. Kuna jambo ambalo pengine hujawahi kulisikia kwenye makampuni mengine -“Ukishajenga biashara yako na Green World Tanzania ikakua, unaweza kumrithisha ye yote yule endapo utaishiwa nguvu za kuendelea na biashara hii au kupoteza maisha. Kwa hiyo kujenga biashara na kampuni ya Green World ni sawa na kuwekeza kwenye jengo au kitu kingine cho chote kikubwa kisichohamishika.” Upo Hapo?

 

MKUTANO JBURG WA GREEN WORLD

VIDEO YA MKUTANO WA GREEN WORLD- ELLIS PARK INDOOR ARENA JOHANNESBURG- 19 NOV 2017

 

Kampuni ya Green World Tanzania inatoa mafao na marupurupu kwa njia 6 tafauti:

  • Retail profit
  • Direct Bonus
  • Indirect Bonus
  • Leadership bonus
  • Honorary Bonus
  • Special Awards

 

green world group photo mwanza

 

Retail Profit au faida ya biashara ya rejareja: Rejea maelezo yetu hapo juu ambapo tulisema ukishajiunga na Green World utanunua bidhaa kwa bei ya kampuni. Unaweza kuziuza bidhaa hizo kwa bei za rajareja kwa wateja wako na kupata faida. Kampuni ya Green world inakuruhusu kufungua duka na ukauza bidhaa hizi pia katika duka lako- Kazi kwako ndugu yangu unayetafuta ajira au njia ya kuongeza kipato.

Direct Bonus: Ukianza kujenga mtandao wako utalipwa kutokana na manunuzi unayoyafanya wewe binafsi kutoka kwenye kampuni. Malipo haya yatategemea ngazi uliyopo na kiasi cha bidhaa ulizonunua. Kwa mfano, ukiwa 3*C, utapewa asilimia 20 ya manunuzi yako kama direct bonus.

Indirect Bonus: Hii ni asilimia ya mauzo ambayo kampuni  itakulipa wewe kutokana na manunuzi yaliyofanywa na watu ambao umewasajili kwenye kampuni. Hii inategemeana na ngazi aliyopo mtu uliyemsajili.

Leadership Bounus: Hii ni tunu endelevu unayopewa mwanachama kwa kujenga na kuisadia timu yako.

Honorary Bonus: Honorary bonus hutolewa kwa wanachama waliofikia hadhi ya Distributor ambapo hupewa asilimia ya pato lote la kampuni la dunia.

Special Awards: Hizi ni tunu ambazo utapewa na kampuni kwa kufikia malengo fulani yaliyowekwa na kampuni. Kwa mfano, ukifikia ngazi ya 6*C katika kipindi cha miezi 6, utapewa fursa ya kutembelea na kuzuru nchi ya China kwa wiki mbili, gharama zote zikiwa juu ya kampuni.

 

Ziara ya Green World ya Jburg

WANACHAMA WA GREEN WORLD KWENYE UWANJA WA NDEGE, JBURG

 

Mfano wa pili, ni pale utakapofikia ngazi ya 7*C katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja ambapo utatunukiwa gari lenye thamani ya $ 10,000. Kuna tunu kubwa zaidi za kufikia kupewa Villa yenye thamani ya $150,000.

 

zawadi ya smartphone

 

 

Umependa Kujiunga Na Kampuni Ya Green World?

 

Kujiunga na kampuni hii soma kwanza ukurasa wa kabla ya kujiunga  na Green World, kisha fuata maelekezo. Mwandishi wa mada hii nitazungumza na wewe moja kwa moja, usikate tamaa endapo mawasiliano yatachelewa kidogo au bonyeza juu ya maneno  JIUNGE SASA kwenye picha ya hapa juu kisha fuata maelekezo.
Kwa maswali au maoni kuhusu mada hii, wasiliana nasi kupitia promota927@gmail.com au jaza fomu yetu hapa chini kwenye ukurasa huu. Vilevile  tunapatikana kwa simu kwenye namba 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali tembelea blog yetu kujisomea mada mbali mbali zinazohusu biashara za mtandao na fursa za kufanya biashara za mtandao zinazotolewa na kampuni za Green World Tanzania na Trevo Tanzania Ltd. Humo unaweza kuona wasomaji wengine wana maoni gani kuhusu mada zetu tunazoziandika. Pia unakaribishwa kuona video mbali mabali zinazohusu biashara ya mtandao ya kampuni ya Green World kwenye channel yetu ya YouTube.

Kutembelea blog bofya HAPA.
Kutembelea channel yetu ya YouTube bofya HAPA.

 

 

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Namba Yako Ya Simu

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni Yako

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii