Karibu Green World Tanzania

 

Karibu Kwenye Kampuni Yetu Ya Green World Tanzania
Jina langu ni Laurian Raphael Mwajombe.

karibu trevo tanzania

Mimi ni mwanachama hai wa kampuni hii mwenye kitambulisho namba 10160935.

Nikupe pongezi nyingi kwa kuchagua kujiunga na kampuni yetu Ya Green World Tanzania kwani umechagua kampuni bora kabisa kati ya kampuni nyingi za mtandao hapa nchini kwetu Tanzania. Watanzania wengi wameshanufaika kutokana na kufanya kazi na kampuni yetu hadi sasa. Kwa kuchagua kujiunga nasi, tayari upo katika njia sahihi ya mafanikio ya afya yako na maisha yako kiuchumi.

 

Sifa Za Kipekee Za Green World

 

Kampuni ya Green World ina sifa nyingi za kipekee ukilinganisha na makampuni mengine ya biashara ya mtandao yaliyopo katika nchi yetu. Kwanza ni urahisi wa kuuelewa mpango wake wa biashara (Compensation Plan). Green World ina mpango rahisi ambao kila mmoja wetu anaweza kuuelewa na kuufanyia kazi. Si hilo tu, kuna sifa nyingine nyingi ambazo unaweza kuzisoma kwa kupitia ukurasa wa “Ubora Wa Kampuni Ya Green World Tanzania“.

 

Ofisi Za Green World Tanzania

 

Kampuni yetu ina ofisi moja nchini Tanzania nayo ipo eneo la Posta Mpya jijini Dares salaam. Ofisi hii ipo kwenye ghorofa ya pili ndani ya jengo la Patel (Patel Building). Kwa wale wasiolijua jengo hili, maelekezo yafuatayo yatasaidia:

Ukiwa katika mtaa wa Azikiwe elekea kwenye hoteli ya Holiday Inn. Hapa kuna njia panda, fuata ya kushoto ukiiacha ile inayoelekea Serana Hotel. Mita chache tu upande wa kushoto, kuna njia ya lami inayoanzia pale linapoishia jengo jipya linalojengwa (Eneo hili zamani lilikuwa linamilikiwa na kampuni ya AISCO). Ukisimama hapo sehemu ya kuingilia njia hii na kutupa macho mbele, utaliona jengo la ghorofa ambalo kwa juu lina maandishi mekundu- AAR CITY HEALTH CARE-PATEL BUILDING. Elekea kwenye jengo hili na fika ghorofa ya pili na uliza ofisi ya Green World.

 

Namna Ya Kujiunga Na Green World Tanzania

 

Kwa wale wa mjini Dar es Salaam ni rahisi mno kujiunga na Green World. Unatakiwa ufike ofisini pamoja na mtu aliyekutaarifu kuhusu biashara hii ya mtandao ukiwa na pesa za kujiunga na biashara. Kiwango kizuri cha mtaji kwa kuanzia ni Tshs 530,000/=. Nasema kiwango kizuri cha kuanzia kwa sababu si lazima uwe na kiasi hicho chote cha pesa. Kiwango kamili kinachotakiwa kwa kujiunga ni Tshs 30,000/= tu. Nimeandika kiasi hicho hapo juu nikiunganisha na Tshs 500,000/= kiasi ambacho ukitumia kununua bidhaa, kitakufikisha ngazi ya 3*C mara moja, ngazi nzuri ya kuanzia kupata bonus. Maelezo kamili utayapata ukishajiunga.

Kama upo nje ya mji wa Dar Es Salaam usihofu, mimi na wewe tutawasiliana na tutapanga namna nzuri ya wewe kuweza kujiunga kirahisi kulingana na sehemu uliyopo. Kuna wanachama wengi tu mikoani ambao wanaendesha biashara hii bila tatizo.

Jiunge sasa  kwa kubonyeza juu ya maneno JIUNGE SASA.

 

 

Mafunzo Ya  Green World Tanzania

 

Kampuni inatoa mafunzo ya bure ya namna ya kuendesha biashara hii katika ofisi zetu. Unaweza kupata mafunzo siku yo yote unayopenda. Kwa wale watakaojiunga nami katika biashara hii, natoa pia mafunzo kwa njia ya mtandao hasa kwa wale walio nje ya Dar Es Salaam ambayo nayo ni bure, natoa mafunzo ya maandishi na vile vile kwa kutumia video. Ukiwa nami utaelewa biashara yote hapo hapo ulipo ili mradi unaweza kutumia mtandao.

 

Kuwasiliana Na Mimi

 

Ni rahisi sana kuwasiliana na mimi. Chagua kutumia simu kwa namba 0655 858027 au 0756 181651 au kunitumia email kupitia promota927@gmail.com. Tumia njia hizo kuniuliza maswali muda wo wote, hata kama bado hujajiunga rasmi, usiogope, nipo kwa ajili yako.

Ukitaka kuijua kampuni kwa undani zaidi na kuona jinsi watanzania wanavyonufaika nayo soma kurasa za “Kampuni Ya Green World Tanzania” na “Kampuni Ya Kuuza Dawa Ya Green World”.

Nikupongeze tena mara ya pili kwa kuchagua kujiunga na kampuni bora kabisa ya mtandao nchini Tanzania  na ninakukaribisha kwa mikono miwili.

Jiunge Na Green World Sasa, Utimize Ndoto Zako.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                          We Care,  We Share!

 

Tafadhali tembelea blog yetu kujisomea mada mbali mbali zinazohusu biashara za mtandao na fursa za kufanya biashara za mtandao zinazotolewa na kampuni za Green World Tanzania na Trevo Tanzania Ltd. Humo unaweza kuona wasomaji wengine wana maoni gani kuhusu mada zetu tunazoziandika. Pia unakaribishwa kuona video mbali mabali zinazohusu biashara ya mtandao ya kampuni ya Green World kwenye channel yetu ya YouTube.

Kutembelea blog bofya HAPA.
Kutembelea channel yetu ya YouTube bofya HAPA.

 

Laurian.

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii