Namna Ya Kupambana Na Vikwazo Vya Biashara Ya Mtandao

 

Vikwazo Vya mafanikio ya Biashara

 

Mafanikio ni neno lenye maana ya kufanikwa kupata kitu ambacho kilitarajiwa, kilinuiwa au kilifanyiwa mpango ili kipatikane. Hivyo basi, ili kuwe na mafanikio ni lazima kwanza kuwe na matarajio au mpango uliowekwa ili kitu hicho kipatikane. Hapawezi kuwepo na mafanikio kama hapakuwepo na mpango au matarajio ya kukipata kitu hicho au kama kitu hicho hakikunuiwa.

Binadamu tumeumbwa na tabia ya kupenda kuwa na mali, ni hali ambayo tunajikuta tumezaliwa nayo. Tunapenda kuwa na vitu kwa ajili ya kukidhi haja zetu za kila siku na tunapenda pia kuwa na vitu vya anasa vya aina zote. Wakati mwingine bila ya kuwa tumepangilia au kutumia nguvu zetu, tunashitukia tumepata vitu vya kututimizia haja zetu za kila siku – na, tunajisifu kuwa tumepata mafanikio – au, kama tuna ufahamu wa kuwa vitu hivyo tumevipata bila kutumia nguvu zetu au bila kuwa na mipango ya kuvipata, tunatumia maneno yenye usahihi zaidi kuwa kuvipata kwetu ilikuwa ni “bahati au ngekewa.”

Watu wengi hata hivyo, haturidhiki na upatikanaji wa mahitaji yetu kwa bahati, ila tunapenda kuwe na mikono yetu katika mafanikio yetu, angalau kwa kiasi fulani. Tunaweka mipango na kuwekeza nguvu zetu katika vitu tunavyopenda kuvifanikisha.

 

hatua za mafanikio

 

Bila kuwa na mipango wala uwekezaji wa nguvu zetu, hatuwezi kupata mafanikio ya kweli, ila bahati na ngekewa za mara chache. Ili kuwa kwenye njia sahihi ya mafanikio, lazima tuwe na mipango na tutumie nguvu zetu. Lazima kujiwekea malengo na kupanga namna nguvu zetu zitakavyotumika ili kuyafikia malengo tuliyojiwekea. Umakini katika kuweka mipango yetu na namna tutakavyoelekeza nguvu zetu kwenye mipango hiyo tuliyojiwekea, ndivyo vitakavyoamua ni kiwango gani cha mafanikio tutapata. Huu ndio ukweli unaosimama katika jambo lo lote tunalotaka kulifanya katika maisha, ikiwa ni pamoja na kupata mafanikio katika biashara za mtandao.

 

UHUSIANO BAINA YA MATARAJIO NA KUKATA TAMAA

 

 

Kukata tamaa ni hali ambayo mtu anakumbana nayo pale anapoona matarajio yake hayapatikani. Ni hali ambayo inayomfanya mtu kukosa raha wakati anapoona kuwa hafikii malengo yake. Mtu anapoanza kukata tamaa, hupoteza ari aliyokuwa nayo ya kufanya shughuli aliyoipanga na taratibu kuanza kupunguza uwekezaji wa nguvu zake.

 

namna ya kuweka malengo

 

Tunakuwa na matarajio fulani kulingana na malengo tuliyojiwekea. Sasa, kama matarajio yetu ni makubwa sana kuliko uwezo wetu wa kuyafikia, ni dhahiri kuwa tunakuwa tumejiweka kwenye hali ya kuja kuchanganyikiwa baadae. Tunapokuwa na matarajio ya kufikia malengo kwa kutegemea watu wengine wafanye kazi kwa ajili yetu na kwa si kwa kutegemea kazi mabayo tutaifanya wenyewe, tunakuwa tunajiweka pia kwenye hali ya kuchanganyikiwa baadae. Kwa vile hatuna uwezo wa kudhibiti kiuhakika kile ambacho watu wengine wanaweza kufanya kwa ajili yetu bali kile tu ambacho wenyewe tunaweza kukifanya kufikia malengo, ni vizuri kuwa na matarajio ya kufikia malengo kwa kuwekeza nguvu zetu wenyewe na si kwa kutegemea kufanyiwa na watu wengine.

Unapofikia matarajio yako kwa kufanya shughuli zako wewe mwenyewe, unakuwa unajijengea hali ya kujiamini. Na, ukishajiamini unaweza kujiwekea malengo makubwa zaidi na zaidi na kufikia mafanikio makubwa zaidi na zaidi kila siku.

 

KUFURAHIA VIKWAZO NA KUWA NA MAWAZO CHANYA

 

Jenga tabia ya kufurahia vikwazo kwani maisha bila vikwazo hayana ladha. Maisha miaka yote yamekuwa na vikwazo na yatabaki kuwa na vikwazo. Kupambana na kuviondoa kabisa vikwazo hivi sio siri ya mafanikio – hakuna mtu duniani hapa aliyeweza kufanya hivyo. Ukianza kusubiri vikwazo viishe ndio upate mafanikio na furaha katika maisha, utaendelea kusubiri ….. na hakuna siku itakuja kwako kuwa ya mafanikio na furaha. Unapokuwa umejifunza namna ya kupata mafanikio na furaha katika maisha yako pamoja na vikwazo vilivyopo, unakuwa umegundua siri ya mafanikio.

Siri nyingine ya kupata mafanikio ni kuelewa nguvu ya kuwa na mawazo chanya. Unaweza kusoma zaidi kuhusu hili kwenye mada ya “Siri Za kufanikiwa Kwenye Biashara Za Mtandao“, ambako tuliitaja kanuni ya “The Law Of Attraction.”

 

law of attraction

 

Hatua ya kwanza katika kufanikiwa ni mawazo. Ukifanikiwa katika mawazo, utafanikiwa katika dunia. Ukiamini kuwa utashinda vikwazo na changamoto zinazokukabili, kwa  hakika utavishinda. Ukiamini kuwa una fursa mbele yako, utapata fursa hizo hata uwe katika mazingira magumu ya kiasi gani. Siri ya kupata mafanikio ni kuwa na mawazo chanya au kujijengea fikra sahihi za mafanikio. Tumia nguvu ya fikra zako katika kupanga mafanikio yako. Kisha tumia nguvu ya fikra hizo kukupa nguvu ya kuiamini mipango yako. Tegemea kukumbana na vikwazo, lakini kamwe usikate tamaa hadi ndoto zako zitakapokamilika.

 

Kupambana Na Vikwazo

 

Ikitokea kuwa umejitahidi kutumia nguvu zako katika kutekeleza mipango yako lakini nguvu zako hazikuzaa matunda, unaweza kujikuta kuwa unachukua moja kati ya maamuzi yafuatayo: 1) Kukata tamaa na kuachana na jambo hilo 2) Kutafuta ufumbuzi kwa nini unashindwa 3) Kujaribu njia mbadala.

Katika kuanza biashara za mtandao jambo ambalo huwasumbua watu wengi mwanzoni ni jinsi ya kuwapata wanachama wengine wajiunge ili kujenga timu. Katika kutatua taizo hilo inabidi kwanza mtu alichambue kwa makini tatizo lake. Kwanza ni kutazama kama njia anayotumia kuwapata watu wa kujisajili ni sahihi au la. Kuna njia nyingi ikiwa ni pamoja na kutumia mdomo (word of mouth) ukianzia na watu unaowafahamu (warm marketing) au walio katika jamii inayokuzunguka au pengine watu usiowajua kabisa (cold marketing).

Hapa kuna mambo yakuchunguza. Jee, hii ndiyo njia sahihi kwa watu hao na jee, unaitumia njia hiyo ipasavyo? Inaweza kuwa ni njia sahihi lakini pengine wewe mwenyewe huna ufahamu wa kutosha kuhusu fursa unayojaribu kuwaelezea au huna vielelezo vya kutosha vya kuwafanya wakuamini. Watu humwamini mtu wanayemwona kuwa anajua anachokisema na ambaye ana ushuhuda wa kile anachokisema, na hasa ushuhuda binafsi. Hapa tatizo linakuwa watu kukosa vigezo vya kuwafanya watu wengine wawaamini katika kile wanachokisema (loss of credibility).

Inakupasa kuchambua kwa kina kuhusu kiini cha kushindwa kwako na kuchukua hatua za maksudi za kukaa chini na kujifunza kwa undani kuhusu biashara yako na kuongeza nyenzo za kuzitumia katika kuwaelezea watu kuhusu fursa ya biashara yako. Wanachama walio juu yako katika kampuni wanaweza kuwa msaada mkubwa kwako katika kuondoa tatizo lako. Kwa juhudi zako na kwa kupata ushauri uanaweza kuondokana na tatizo hili, watu wakaanza kukubali na ukapata wafuasi wengi kwenye timu yako. Hapa tanasema umepambana kulijua tatizo lako na kufanikiwa kulipatia ufumbuzi.

Inaweza ikatokea kuwa umebaini kuwa hutakuwa na muda wa kutosha kuwazungukia watu au hutoweza kuendesha semina kwa sasa, hivyo ukaamua kutumia njia mbadala. Kwa mfano ukaamua kutumia mitandao ya kijamii na kurusha matangazo yako kwenye vyombo mbalimbali. Ukianza kupata watu wanaotaka kupata maelezo ya ziada na wengine kujisajili, tunasema umeondokana na tatizo lako la kushindwa kuwasajili watu kwa njia ya mdomo kwa kutumia njia mbadala – njia ya kutumia teknolijia mpya ya utandawazi.

Unaweza kuwa umejaribu njia moja mbadala na haikufanya kazi, bado huo sio mwisho wa kuendelea kutafuta njia nyingine. Thomas Edison aliandika kuwa “Kwamba kitu hakikufanya kazi kama ulivyokuwa umepanga, haina maana kuwa lengo lako halina maana. Jaribu kutafuta njia nyingine ya kufikia malengo yako.”

Baada ya muda utakuja kujua ni kitu gani ambacho kinakufanyia kazi vizuri na utakuwa umefanikiwa kuondoa kikwazo kilichikuwa kinakusumbua. Hakuna kisichokuwa na njia ya kukufanyia kazi, ni wewe kuwa mtulivu, mvumilivu na mtafiti.

 

Epuka Kuchanganyikiwa

 

Usitegemee hata siku moja kuwa mambo yatakunyookea na kwenda kama ulivyojipangia. Endapo umejiwekea matarajio yanayoweza kufikiwa, uwezekano wa kukumbana na vikwazo vikubwa vya kukukatisha kabisa tamaa utapungua. Pokea vikwazo na changamoto zinazojitokeza mbele yako. Ni katika kuvishinda vikwazo hivyo ndipo mafanikio yanapopatikana. Kila wakati amini kuwa unaweza kuvishinda vikwazo hivyo au kutafuta njia mbadala ya kufikia mafanikio.

 

Kujifunza Kutokana Na Vikwazo

 

Katika kupambana na vikwazo, iwe katika kuviondoa vikwazo hivyo au kutafuta njia mbadala ya kuvikwepa vikwazo, utakuwa umepata fursa ya kujifunza. Kama umeshindwa kabisa kuondoa kikwazo fulani, utakuwa umejifunza njia moja ambayo haifai kuitumia katika shughuli zako na kuwa inatakiwa uikwepe. Chunguza kwa makini kisichofanya kazi katika njia hiyo na tafuta njia nyingine inayofanana nayo ya kuijaribu.

 

hatua za kufanikwa katika biashara

 

Usiogope kushindwa kwani hakuna aliyefaulu bila kushindwa mara kadhaa. Mwanasayansi Thomas Edison alisema kuwa ” Nikigundua njia 10,000 ambazo hazifanyi kazi, sijashindwa . Sikati tamaa, kwa sababu kila moja ya njia hizo ambayo sitaitumia tena ni hatua moja mbele …. ”

 

Usisite kutoa mchango wako kuhusiana na mada hii au kuuliza maswali uliyo nayo. Tutahakikisha tunakujibu kwa wakati.

 

Kama una maoni yako kuhusu makala hii au kama una maswali yo yote usisite kuniandikia kupitia promota927@gmail.com au kwa kujaza fomu hapa chini. Pia unaweza kuwasiliana nami kwa simu kupitia 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

Tafadhali tembelea blog yetu kujisomea mada mbali mbali zinazohusu biashara za mtandao na fursa za kufanya biashara za mtandao zinazotolewa na kampuni za Green World Tanzania na Trevo Tanzania Ltd. Humo unaweza kuona wasomaji wengine wana maoni gani kuhusu mada zetu tunazoziandika. Pia unakaribishwa kuona video mbali mabali zinazohusu biashara ya mtandao ya kampuni ya Green World kwenye channel yetu ya YouTube.

Kutembelea blog bofya HAPA.
Kutembelea channel yetu ya YouTube bofya HAPA.

 

Laurian.

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii

404 Not Found

404 Not Found


nginx/1.10.3