UJUE UGONJWA WA HOMA YA MATUMBO – TYPHOID

 

kinga ya typhoid

 

Ugonjwa wa homa ya matumbo au typhoid ni tatizo linaendelea kuzisumbua nchi zinazoendelea. Katika nchi kama Marekani, tatizo hili limepungua sana kuanzia miaka ya mwanzo ya 1900. Katika nchi hizo, wahanga wa tatizo hilo ni wale waliotoka katika siku za usoni na kuingia kwenye nchi ambazo bado zina tatizo hili. Katika dunia, watu zaidi ya milioni 21 hupatwa na tatizo hili kila mwaka na katika hao, watu zaidi ya laki mbili hufariki dunia.

 

Chanzo Cha Typhoid

 

Typhoid husababishwa na aina ya bakteria aitwaye salmonella typhi. Mara chache typhoid husababishwa na bakteria mwingine aitwaye salmonella paratyphi ingawa huyu hasababishi maradhi makubwa kama yule wa kwanza.

Bakteria hawa hupatikana katika kinyesi. Njia kuu ya kuambukizwa bakteria wa typhoid ni kupitia chakula au maji yaliyochafuliwa na kinyesi au kugusana na mtu mwenye typhoid. Katika nchi nyingi zinazoendelea zenye mlipuko wa typhoid, maambukizi hutokana na maji yaliyochafuliwa na kinyesi na kuwa na utaratibu mbovu wa kuondoa majitaka. katiak nchi zilizoendelea, waathirika wengi ni wasafiri ambao baadaye huwaambukiza wenzao kwa njia njia ya kinyesi kwenda kinywani.

Maana yake ni kwamba, bakteria hawa huishi ndani ya kinyesi au mara myingine katika mkojo wa mtu aliyekwisha ambukizwa. Unaweza kuambukizwa kwa kula chakula kilichoshikwa na mtu mwenye maambukizi ikiwa mtu huyo hakuosha vizuri mikono yake baada ya kwenda haja kubwa. Unaweza pia kuambukizwa wadudu hao kwa kunywa maji yanye vijidudu hao.

Wasambazaji Wa Typhoid

Watu wengine (wachache) waliokwisha pata maambukizi wakatibiwa, bado huwa na wadudu hawa wakiwa wamejificha ndani ya utumbo wao au vifuko vyao vya nyongo kwa miaka mingi. Watu hawa huendelea kutoa bakteria kwenye vinyesi vyao na kuwaambukiza watu wengine, ingawa wao wenyewe hawataonyesha dalili zo zote za kuwa na typhoid. Watu hawa hutwa “chronic carriers” au wasamabazaji wa typhoid. Watu hawa ambao wanaweza kufikia asilimia 3 hadi 5 ya wale waliokwisha ambukizwa, wanaweza kuwa vyanzo vipya vya milipuko ya typhoid kwa miaka mingi.

 

Madhara ya Typhoid

 

Madhara makubwa ya typhoid ni kutokwa na damu au kutoboa vijitundu katika utumbo – hali ambayo inaweza kutokea wiki tatu baada ya kupata maambukizi ya bakteria. Kuotkea kwa tundu katika utumbo mdogo au utumbo mkubwa kunaweza kusababisha vitu vilivyopo katika utumbo kupenya na kuingia kwenye mfuko unaolizunguka tumbo na kumfanya kmwathirika asikie maumivu, kichefuchefu, kutapika na maambukizi kwenye mfumo wa damu (sepsis), hali ambayo itahitaji tiba ya haraka.

Madhara mengine yanaweza kuwa:

1. Kuathirika kwa misuli ya moyo (myocarditis.
2. Kuathirika kwa utando unaozunguka moyo na valvu (endocarditis.
3. Pneumonia (homa ya mapafu).
4. Kuathirika kwa kongosho (pancreatitis).
5. Maambukizi kwenye figo na kibofu cha mkojo.
6. Maambukizi kwenye majimaji na ngozi laini inayozunguka ubongo na uti wa mgongo (meningitis).
7. Matatizo ya akili kama kuchanganyikiwa, kuweweseka na ukichaa.

 

Dalili Za Typhoid

 

Dalili za typhoid huongezeka taratibu na huanza kutokea wiki moja hadi tatu baada ya kupata mambukizi.

Dalili Za  Mwanzo

. Homa inayponda taratibu kadiri siku zinavyokwenda na kufikia nyuzi 40.5C
. Maumivu ya kichwa
. Udhaifu wa mwili na uchovu
. Maumivu ya misuli
. Kutoka jacho jingi
. Kikohozi kikavu
. Kukosa hamu ya kula na kukonda
. Maumivu ya tumboni
. Kuharisha au kufunga choo
. Tumbo kujaaCeftriaxone (Rocephin).

Dalili Za Baadaye

Kama hukupata tiba unaweza

 

dalili za typhoid
. Kuchanganyikiwa
. Kuishiwa nguvu ukabaki umelelala macho yakiwa yamefunga nusu, hali inayoitwa “typhoid state”.

 

Tiba Ya Typhoid

 

Tiba ambayo hufanya kazi vizuri sana kwa tatizo la typhoid ni kutumia antibiotics. Tiba nzuri ni kutumia vidonge vya Ciprofloxacin (Cipro) kwa watu wazima ambao hawana ujauzito. Sindano ya Ceftriaxone (Rocephin) inafaa zadi kwa kundi la watu ambao hawatakiwi kupewa Cipro, kwa mfano watoto.

Dawa hizi huweza kuleta madhara mengine kwa mwili (side effects) na matumizi ya muda mrefu huwafanya bakteria kuzizoea dawa hizi na zisiwe na nguvu ya kuwaua tena (anti-biotic resistance). Hapo zamani dawa iliyotumika sana kwa typhoid ilikuwa chloramphenicol, lakini kutokana na kuwa na madhara mengine mengi na bakteria kuizoea dawa hiyo, haitumiki tena. Tatizo la wadudu kuzizoea dawa za antibiotic ni kubwa katika tiba ya typhoid na ni kubwa zaidi katika nchi zinazoendelea. Katika miaka ya karibuni, S.typhi wameanza kutosikia tiba ya dawa za trimethoprim-sulfamethoxazole na ampicillin.

Mtu aliyeshikwa na typhoid anatakiwa kupewa vinywaji kwa wingi ili kuzuia kupungukiwa na maji mwilini kutokana na homa kali na kuharisha. Kama utumbo utakuwa una matundu sana, upasuaji utahitajika ili kuziba matundu hayo.

Mtu anayetegemea kusafiri kuelekea kwenye maeneo yenye maradhi kwa wingi anaweza kujilinda kwa kupata sindano ya kinga. Kuna aina mbili ya chanzo kwa typhoid.

. Sindano inayotolewa mara moja wiki moja kabla ya safari
. Vidonge vinne vinavyonywewa kimoja kila baada ya siku moja

 

chanjo ya typhoid

 

Kinga hizi hazina uhakika wa asilimia mia moja kwani nguvu zake huisha baada ya muda mfupi hivyo kurudia kupata kinga kila baada ya muda fulani kutajhitajika. Yafaa kuchukua tahadhali za kiafya uwapo safarini kwenye maeneo yenye magonjwa haya ikiwa ni pamoja na kuosha mikono kwa sabuni kabla ya kula na baada ya kujisaidia, kutokunywa maji ambayo si salama, kutokula matunda na mboga ambavyo havimenywi na kuhakikisha kuwa unakula chakula cha moto.

Katika ukurasa mwingine tutauona ugonjwa wa UTI ambamo tutaona bakteria wa aina nyingine anavyoshambulia na kuathiri mfumo wa utoaji haja ndogo wa binadamu.

Usisite kutona maono uliyo nayo kuhusu mada yetu ya leo au kuuliza maswali uliyo nayo. Tutafanya kila juhudi kuona kwamba tumekujibu ipasavyo.

 

Laurian.

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii