Tiba Ya Ugumba Kwa Wanawake

 

kutopata mtoto

 

Baada ya maelezo ya mwathirika kuhusu tatizo lake la kutopata ujazito, dakatari anaweza kuamua kuchukua vipimo ili kujua aina ya tatizo linalomsumbua mama huyo na ndipo tiba itakapotolewa kulingana na aina ya tatizo litakaloonekana. Katika ukurasa huu tutaona baadhi ya njia zinazotumika kumsaidia mwanamke mwenye tatizo la kutopata mimba.

Aina Za Tiba Ya Ugumba Wa Wanawake

Tiba itakayotolewa kuondoa tatizo la mwanamke kutopata ujauzito itategemea aina ya tatizo lililobainika, umri wa mwanamke na tatizo hilo limedumu kwa muda gani. Kwa vile ugumba ni tatizo gumu kulitibu, tiba inaweza kutumia kiasi kikubwa cha pesa, muda mrefu na kuhitaji uvumilivu kisaikolojia. Pamoja na kuwa kuna wanawake wanaofanikiwa kupata ujauzito baada ya kupata aina moja au mbili tu za tiba, si jambo la ajabu kama mwanamke mwingine akahitaji kupata mchanganyiko wa aina nyingi zaidi wa tiba kabla hajafanikiwa kupata mimba. Tiba za ugumba hujaribu kurudisha uwezo wa mwanamke kupata ujauzito – kwa kutumia dawa au upasuaji – au kumsaidia mwanamke kupata mtoto kwa njia nyingine za kitaalamu.

Kurudisha Uwezo Wa Kuzalisha Mayai

 

Madawa hutumika ili kuboresha au kurudisha uwezo uliopotea wa kuzalisha mayai – hii ndiyo njia kuu inayotumika kumsaidia mwanamke mwenye tatizo la kuzalisha mayai. Dawa hizi hufanya kazi kama homoni za kawaida za mwili za follicle-stimulating

 

Soy Power Capsule

Dawa Ya Ugumba Kwa Wanawake – Bonyeza juu ya picha kusoma maelezo yake

 

hormone (FSH) na luteinizing hormone (LH) kuamsha uzalishaji wa mayai. Dawa hizi pia hutumika kuwasaidia wanawake wenye uwezo wa kuzalisha mayai kutoa mayai yenye ubora zaidi au kutoa yai zaidi ya moja.
Clomiphene citrate: Clomiphene citrate (Clomid, Serophene) ni dawa ya kunywa inayosaidia tezi ya pituitary kutoa homoni za follicle-stimulating hormone FSH na  luteinizing hormone LH kwa kiwango kikubwa zaidi hivyo kusaidia ukuaji wa ovarian follicle inayotunza yai.
Gonadotropins: Hizi ni dawa za sindano zinasaidia ovari moja kwa moja kwa kusaidia ukuaji wa yai na utoaji wa yai kwa wakati unaotakiwa.

Metformin: Hizi hutumika wakati inapobainika kuwa mwili kushindwa kuitumia insulin ndicho chanzo cha ugumba.

Letrozole: Hii hufanya kazi kama clomiphene kusaidia mwili kutoa yai.

Bromocriptine: Hii hutumika wakati matatizo ya ugumba yanatokana na tezi za pituitary kutengeneza prolactin
(hyperprolactinemia) nyingi kupita kiasi.

 

Upasuaji

 

Kuna baadhi ya operesheni ambazo hufanywa kurekebisha dosari zilizoonekana au kuboresha uwezo wa mwanamke kuzaa. Hata hivyo, operesheni hizi zimepungua umaarufu wake baada ya njia bora na za kisasa kugundulika.

 

ugumba kwa wanawake

 

Laparoscopic or hysteroscopic surgery

Upasuaji wa aina hizi mbili huweza kuondoa au kurekebisha dosari katika tumbo la uzazi la mwanamke. Urekebishaji wa umbo la nyumba ya uzazi, kuondoa endometriosis na baadhi ya aina za uvimbe (fibroids) na kuongeza uwezekano wa mwanamke kutunga mimba.

Tubal surgeries

Pale inapogundulika kuwa mirija ya uzazi imeziba au imejaa maji (hydrosalpinx), laparoscopy mara chache huweza kutumika kuongeza kipenyo cha mirija au kutoboa njia nyingine katika mirija hiyo. Kuongeza uwezekano wa kupata mimba kwa kutumia in vitro fertilization (IVF), kuiondoa mirija ya uzazi au kuiziba karibu na nyumba  ya uzazi ndiyo njia inayopendekezwa pale mirija ya uzazi inapokuwa imejaa maji.

 

Intrauterine insemination (IUI)

 

Hii ni njia ya kumsaidia mwanamke kupata ujauzito inayotumika kama mwanamme ni mgumba, mwanamke ana matatizo ya ute
(cervical mucus) au kama ugumba haujaeleweka chanzo chake. Njia hii ambayo pia huitwa artificial insemination, hufanywa kwa kupandikiza mamilioni ya mbegu komavu ndani ya tumbo la uzazi (uterus) la mwanamke anapokaribia siku zake za kutoa yai.

Assisted Reproductive Technology

 

Njia hizi ni ghali sana na hutumia muda mrefu lakini zimewasaidia watu wengi ambao vinginevyo hawangeweza kupata watoto katika maisha yao.
In vitro fertilization (IVF): Katika moja ya njia hizi, mayai yaliyokomaa huchukuliwa kutoka kwa mwanamke kisha
kuchanganywa na mbegu za mwanamme kwenye maabara. Embryo zinazotokea hurudishwa kwenye nyumba ya uzazi ya mwanamke
ili ziweze kukua. Hii huitwa In vitro fertilization (IVF). Ni njia bora kwa mwanamke ambaye mirija yake ya uzazi imeziba au kama mwili wa mwanamme hauna uwezo wakuzalisha mbegu za kutosha.

 

tiba za ugumba

 

Zygote Intrafallopian Transfer (ZIFT) Au Tubal Embryo Transfer: Njia hii inafanana na ile ya in vitro fertilization ambapo mayai na mbegu huchanganywa kwenye maabara. Hapa embryo hupandikizwa kwenye mirija ya uzazi (fallopian tubes) badala ya kuwekwa kwenye nyumba ya uzazi (uterus).
Gamete intrafallopian transfer (GIFT): Mayai na mbegu za mwanamme huwekwa kwenye mirija ya uzazi na kuruhusu embryo
kuundwa ndani ya mwili wa mwanamke.

Intracytoplasmic sperm injection (ICSI): Ni njia inayotumika pale inapobainika kuwa mwanamme ana matatizo ya kuzalisha mbegu bora. Hapa mbegu moja hudungwa kwenye yai la mwanamke lililokomaa na embryo kupandikizwa kwenye nyumba ya uzazi (uterus) au kwenye mirija ya uzazi (fallopian tubes).

Katika kurasa nyingine ndani ya tovuti yetu tumejadili maana ya mzunguko wa hedhi wa mwanamke na kuona awamu nne za mzunguko wa hedhi kwa mwanamke. Tumeona pia sababu za ugumba kwa mwanamme. Tumejadili kwa kina sababu za mwanamke kukosa mtoto na kuelezea tiba za ugumba kwa mwanamke.

Usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu mada yetu , ni furaha kwetu kuona kuwa tumekujibu vizuri.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Namba Yako Ya Simu

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni Yako


Ukurasa         1         2         3       4        5

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii