Homa ya Ini – Hepatitis B

 

homa ya manjano

 

Mada yetu ya leo ni mfululizo wa mada iliyopita iliyoelezea ugonjwa wa homa ya ini (hepatitis). Katika ukurasa uliopita tuliona kuwa hepatitis ni jumla ya magonjwa yote yanayoshambulia seli za ini. Tuliona kuwa kuna aina kuu tano ya hepatitis ingawa katika ukurasa huo tulizungumzia kwa undani aina moja tu – hepatitis A. Katika ukurasa huu basi tutaendelea kuona aina nyingine ya hepatitis yaani hepatitis B.

Hepatitis B ni maambukizi mabaya sana ya kirusi aitwaye hepatitis B virus (HBV) kwenye maini. Kwa watu wengine ugonjwa huu huweza kuchukua zaidi ya miezi 6 (chronic). Ugonjwa huu ukichukua muda mrefu unaweza kuleta madhara ya kufeli kwa ini, kansa ya ini au liver cirrhosis hali ambayo itaacha makovu ya kudumu kwenye maini. Watu wengi wanaougua ugonjwa huu hupona kabisa. Kuna chanjo ya kusaidia kuzuia hepatitis B lakini hakuna tiba pale ambapo tayari utakuwa umeambukizwa virusi wa hepatitis B. Ukishaambukizwa yafaa kuchukua tahadhari za kusaidia kutowaambukiza watu wengine.

 

Dalili Za Hepatitis B

 

Dalili za hepatitis B huanza kuonekana baada ya mwezi mmoja hadi minne baada ya kupata maambukizi, nazo ni:

. Maumivu ya tumbo
. Mkojo mweusi
. Homa
. Maumivu ya joints
. Kukosa hamu ya kula
. Kichefuchefu na kutapika
. Udhaifu wa mwili na mwili kukosa nguvu
. Macho na ngozi kugeuka rangi na kuwa vya njano

 

Chanzo Cha Hepatitis B

 

Ugomjwa wa hepatitis B husababishwa na kirusi aitwaye Hepatitis B virus (HBV). Kirusi huyu huambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia damu, shahawa na maji maji mengine ya mwilini. Njia kuu za uambukizaji zikiwa:

. Kujamiiana. Unaweza kuambukizwa na mtu mwenye ugonjwa huo kama utajamiiana naye bila kutumia kinga na damu, mate, shahawa au maji maji ya ukeni yakaingia ndani ya mwili wako.

. Kuchangia sindano. Kirusi wa hepatitis B anaambukiza kirahisi sana kupitia sindano zenye damu ya mtu mwenye virusi hivi.

. Mama kumwambukiza mtoto. Mama mwenye mimba mwenye virusi vya HBV anaweza kumwambukiza kichanga wakati wa tendo la uzazi. Mtoto anaweza kupewa chanjo baada ya kuzaliwa na akaepuka kuambukizwa, hivyo ni vizuri kuchukua tahadhari ya kujipima wakati una ujauzito.

Hepatitis B hugawanywa katika makundi mawili; Hepatitis ya muda mfupi (acute hepatitis) na hepatitis ya muda mrefu (chronic hepatitis).

Acute hepatitis B: Hii huchukua chini ya miezi 6 kupona. Kinga zako za mwili zinaweza kupambana na kuuondoa ugonjwa huu na ukapona kabisa katika muda mfupi. Watu wazima mara nyingi huugua acute hepatitis ingawa mara chache huweza kufikia kuwa chronic hepatitis.

Chronic hepatitis B: Ugonjwa huu huchukua miezi 6 au zaidi kupona. Kama kinga za mwili wako hazitaweza kuushinda, basi ugonjwa utakuwa ni wa maisha kwako na uwezekano wa magonjwa makubwa zaidi kama ya cirrhosis na saratani ya ini ukiongezeka. Chronic hepatitis B inaweza isigundulike kwa miaka mingi hadi mgonjwa atakapokuwa mahututi kutokana na ugonjwa huu wa homa ya ini.

 

Madhara ya hepatitis B

 

Kuwa na hepatitis B kwa muda mrefu (chronic hepatits) kunaweza kusababisha madhara makubwa yafutayo;

. Makovu kwenye ini (Cirrhosis). Kuvimba kwa ini kwa muda mrefu kunakotokana na virusi wa hepatitis B kunaweza kusababaisha makovu kwenye ini (cirrhosis) na kulifanya ini lishindwe kufanya kazi yake inavyotakiwa.

 

Liver_Cirrhosis

 

. Saratani ya ini. Watu wenye hapatitis B kwa muda mrefu wanaweza baadaye wakapata saratani ya ini.

. Ini kufeli. Ini likishindwa kufanya kazi zake kabisa, hatua nyingine ya kuwekewa ini jingine itahitajika.

. Matatizo mengine. Mgonjwa mwenye hepatitis B anaweza kupata matatizo ya figo, uvimbe kwenye mishipa ya damu na upungufu wa damu.

 

Tiba Ya Hepatitis B

 

Kama vipimo vikionyesha kuwa una hepatitis B ya muda mfupi (acute hepatitis), huhitaji tiba kwa sababu itaondoka yenyewe baada ya muda mfupi. Badala yake unahitaji kupumzika, kupata lishe bora na vinywaji vya kutosha wakati kinga zako za mwili zikipambana kuundoa ugonjwa huo.

 

Livergen Capsule

Dawa ya kutibu homa ya ini (bofya juu ya picha kusoma maelelzo)

Endapo hepatitis B ni ya muda mrefu (chronic hepatitis) yaani zaidi ya miezi sita, utahitaj tiba ili kuondoa madhara ya ugonjwa huo na kuzuia usiwaambukize watu wengine. Baadhiya tiba ni:

. Dawa za kuua virusi (antiviral medications). Kuna dawa nyingi za kuweza kuua virusi ikiwa ni pamoja na lamivudine (Epivir), adefovir (Hepsera), telbivudine (Tyzeka) na entecavir (Baraclude).

. Interferon alfa-2b (Intron A). Hii hutolewa kama sindano na hasa hutumika kwa vijana wadogo au wanaotegemea kupata ujauzito. Madhara ya tiba hii ni kupata mfadhaiko, kubanwa kifua na kupumua kwa shida.

. Kubadilishiwa Maini. Kama maini yako yameharibika kabisa, upasuaji hufanyika na kuwekewa maini mengine.
Katika ukurasa mwingine tutaujadili ugonjwa wa hepatitis C. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo, ni furaha kwetu kuupokea mchango wako.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

 

 

Ukurasa      1            2             3         4

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii