Tabia Zinazoharibu Mafanikio Katika Timu

 

kuharibu mafanikio katika timu

 

Mafanikio katika biashara ya mtandao yanajengwa juu ya uaminifu na uadilifu wa kiongozi kwa timu anayoongoza na kuwa na uelewa mkubwa wa biashara. Unapomshirikisha mtu kwenye biashara hii, wewe unakuwa ndiye mshauri wake. Unakuwa ndiye dira yake. Watu wengi wanakuwa wamechoshwa na tabia za waajiri, kama kutokuwajibika, kukosa uaminifu, kutoishi kama jamii moja, ubovu wa mahusiano, umbeya, siasa mbaya n.k. na wanategemea kuyaona haya wanapojiunga na biashara tofauti. Hivi ni vitu vinavyowavutia watu zaidi mara nyingine kuliko hata pesa, magari na safari za nje.

Vitu vinavyodumaza au kubomoa maendeleo ya timu:

 

Kutowajali Wale Unaofanya Nao Kazi

Watu uliowaunganisha kwenye timu (wafuasi wako binafsi) na wale ambao wameletwa na walio chini yako wote wanahitaji kujaliwa na kulelewa ili waweze kukua na kufanikiwa. Hii ni biashara baina ya watu ambapo kila mmoja anahitaji kutoa msaada na kusaidiwa ili kupata mafanikio. Kiwango chako cha kuwajali wengine au cha kuonyesha kuwa unawajali wengine kitapima mafanikio yako.

 

kujali wengine

 

Kampuni hutoa mafunzo kila wiki na kuandaa mikutano mbalimbali. Watu walio juu wanapaswa kuwajali walio chaini yao na kuwapa taarifa na kuwakumbusha kuhusu nafasi hizi muhimu za kuweza kujifunza kuhusu biashara ya kampuni. Mafunzo na mikutano huandaliwa na wale wenye uzoefu na uelewa mpana zaidi wa kampuni kuliko wale walio wageni. Kila mmoja katika kampuni anatakiwa kutumia nafasi hizi kadri anavyoweza. Mafunzo na mikutano hujenga hamasa na kuwafariji wale wenye matatizo. Watoa mada na watoa ushuhuda huwafanya watu waamini kuwa inawezekana. Ni pole pole na kwa ugumu, lakini inawezekana.

 

Kuwapunja Maslahi Yao

Watu waliojiunga nawe kwenye biashara wote wana nia moja kuu – KUBORESHA KIPATO CHAO. Ni wajibu wako kama kiongozi kuhakikisha kuwa watu hawa wanafundishwa kuhusu biashara hii pindi wanapojiunga na wanaanza kupata mafao amapema, ikiwezekana katika mwezi wao wa kwanza wanapoanza biashara. Wakipata bonasi zao mapema, watajengewa imani. Watu wanaoanza kupata mafao mapema, wanadumu kwenye biashara.

Inakubidi kuwafundisha mapema namna ya kujaza fomu za manunuzi na za kusajali wanachama ili kazi hizo wazimudu wenyewe wanapotaka kununua bidhaa, wanapowaleta wagonjwa au wanachama wao wapya. Hakikisha wanapata faida zao zote za mauzo ya rejareja na wanaingiziwa BV zao zote kama inavyotakiwa. Ni kosa kubwa na ni wizi kutumia udhaifu wa wanachama wapya kuwavuruga na kuchukua haki zao za pesa taslimu au BV. Mtu anapogundua kuwa amepunjwa kwa namana yo yote ile, hukata tamaa na mara nyingi wanaacha biashara.

Itakusaidia nini kuwapunja wanachama wapya pesa zao ndogo wanapojiunga na kisha ukabaki huna timu ya kuiongoza na kila siku ukawa ni mtu wa kusajili wanachama wapya? Mtu ambaye ana mapungufu haya na ambaye hana maendeleao kwenye biashara ya mtandao huitwa GRINDER. Kwa nini uishie kuwa grinder na kukosa faida kubwa za biashara hii? Kumbuka kuwa watu 4 tu utakaowafundisha na kuwalea vizuri wanaweza kukufikisha ngazi ya 3* Manager, na kama walikwenda vuzuri, utakuwa wamekupa DVD, safari ya China, gari ndogo (milioni 20), Gari kubwa (milioni 70) na nyumba (milioni 300). Hivi vyote unabadilishana na pesa ndogo ndogo za wanachama wapya?

 

Kusema Uwongo

Kusema uwongo ni kusema maneno kwa kinywa chako kama kwamba ni ya kweli, wakati ukijua wazi kuwa si ya kweli. Uwongo unaweza kuwa si wa kuleta madhara na ukiwa umedhariwa kutia moyo au kuleta hamasa (white lie). Lakini, kwa vyo vyote vile, kusema uwongo ni kitu kibaya.

 

kusema uwongo

 

Uwongo humfanya mtu aliyeongopewa ajisikie vibaya kwa sababu ni namna ya udanganyifu. Wakati mwingine ni zaidi ya kujisikia vibaya, kwa mfano kusababisha mtafaruku. Kwa mfano, kumwambia mtu akiingiza mtaji wa kiasi fulani kabika biashara yako, ndani ya mwezi mmoja atapata kiasi fulani cha pesa na kumbe si kweli. Neno kama hili linaweza kuvunja nyumba ya mtu au kuharibu uhusiano wa marafiki. Ukisema uwongo wa namna hii, mtu huyo hatakuamini wala kukuheshimu. Kibaya zaidi, atachukulia kuwa watu wote wa kampuni hii ni waongo – kampuni ya matapeli – na hawa uliowaongopea hawataendelea kufanya biashara nawe. Hata uwongo mdogo kama wa kuahidi kumsaidia mtu kupanda ngazi unaharibu biashara yako kwa sababu wasipopanda wataiacha biashara hii.

Uongozi wa kampuni hupenda kupata ripoti mara kwa mara kuhusu maendeleo ya biashara. Iwapo kama kiongozi utajulikana kusema uwongo katika ripoti zako, wakati utafika ambapo uongozi utatilia mashaka kauli zako. Hii inaweza kuathiri maendeleo ya timu kwa kukosa misaada wakati mwingine kutoka uongozi wa juu.

Kiongozi anayesema ukweli, hata kama wakati fulani hautawapendeza, na kuyasimamia yale anayoyasema, huaminiwa na wale walio chini yake.

 

Umbeya

Kuna sababu nyingi za kuufanya umbeya kuwa ni kitu kibaya. Pamoja na mabaya ya umbeya lakini bado huwa tunafanya umbeya. Wote hapa tu wahanga wa umbea, lakini bado tunaufanya.

 

hasara za umbeya

 

Ni kitu cha mzunguko, lakini tunahiji kuuacha. Umbeya una madhara mengi:

1. Hadhi
Umbeya humpunguzia mtu hadhi yake. Hakuna mtu aliyezaliwa na madhambi. Utapoeneza umbea kuhusu mtu fulani, unaichafua sura yake na kumpa ugumu wa kupokelewa na watu wengine pale atakapojaribu kufanya jambo.

2. Mtafaruku
Watu wanaweza kukufuata (kukusuta) kuhusu tabia yako ya umbeya na ukadhalilika. Mwishowe utachukuliwa kama mtu mbaya na watu hawatatoa ushirikiano kwako na kukutenga kwa kuiogopa tabia yako.

3. Watu watakosa imani na wewe
Watu wakikugundua tu kuwa ni mbeya wataanza kukutenga. Pamoja na watu kuamini kuwa siri zao hazitakuwa salama mbele yako, wataanza kutafuta mabaya yako. Wataanza kutafuta kama unaongeza uongo katika hadithi zako ili kunogesha umbeya wako. Umbeya ni tabia na ikikomaa, watu baadaye watakuchoka na hawatafurahia mazungumzo yako.

 

Kutojiendeleza Binafsi

Watu wengi hawatakuambia moja ya siri kubwa za mafanikio katika biashara ya mtandao kwa makusudi mazima au kwa sababu wao vile vile hawaijui siri hii, ambayo ni; kujiendeleza binafsi.Kujiendeleza binafsi maana yake kujisomea maandishi yanayochapishwa na kampuni yako, yanayoandikwa na watu wengine waliofanikiwa katika biashara ya mtandao, kutazama video mabalimbali na kuhudhuria mafunzo ya biashara yanayotolewa na kampuni na sehemu nyingine n.k.

 

kujiendeleza kibiashara

 

1. Kama utakaa kuyawazia matatizo yako, hutawekeza muda kwenye biashara yako ya mtandao. Sasa kama hutaonyesha mwelekeo wa kuithamini biashara yako, unafikiri ni ki vipi watu watashawishika kuungana na wewe utakapowaambia kuhusu fursa yako ya biashara? Kama utapoteza muda wako wote kufikiria kwa nini hufanikiwi kwenye biashara yako au kwa nini hupati pesa, hicho ndicho kitakachotokea. Hutapata pesa. Endelea kuwazia vitu vinavyokukwamisha, tegemea kupata vikwazo zaidi.. Hii ndiyo sababu, kujiendeleza binafsi ni muhimu. Kutakusaidia kupata pesa, kwa sababu kutakufanya uelekeze mawazo yako kwenye biashara yako.

2. Wafanya biashara wote waliofanikiwa wana sifa moja ambayo ni kujiamini. Hii ni hoja kubwa hivi kwamba inafaa kuirudia tena kwa kusema kuwa: wafanya biashara wote waliofanikiwa, ni watu wanaojiamini wao wenyewe, kibiashara na kimafanikio. Bili kujiendeleza, si rahisi kufikia kiwango hiki kujiamni cha kuiendesha biashara yako. Lakini ukijiamini, ni rahisi kuuza, na ni rahisi kupata pesa.

3. Mwisho, upende usipende, kujiendeleza binafsi ni muhimu pale utakapojaribu kufanya mapya katika biashara yako. Biashara yo yote, hutoa picha ya mmiliki wake, na kwa vile wewe ndiye mmiliki wa biashara yako ya mtandao,biashara unayoifanya itatoa picha ya jinsi ulivyo. Kama bado si mkomavu katika eneo lo lote, hali hiyo itajionyesha kwenye utawala wako, na itasababisha upate kipato kidogo.

Kama tulivyosema mwanzo, unapokuwa kiongozi wa timu, wale wa chini hukuchukulia kuwa ni kioo chao. Ukiyafanya hayo yasiyofaa, baadhi ya wale utakaobaki nao watajifunza pia maovu haya na hatimaye utakuwa ni mwendelezo wa maovu baina ya wachache utakaobaki nao. Kundi kubwa la wanachama wataondoka mara baada ya kujiunga. Hii itakufanya kila siku uhangaike kusajili watu wapya na kamwe hutafaidi matunda ya biashara ya mtandao yanayotokana na mwendelezo wa nguvu zako za kuwafundisha walio chini yako (leveraged income). Walio wengi katika kampuni yenu wakiwa na tabia hizi, kampuni yenu kwa ujumla itakosa maendeleo na kuitwa kampuni ya matapeli.

Una mawazo  ya nyongeza kuhusu mada yetu ya leo? Usisite kutoa mchango wako .

 

Tafadhali tembelea blog yetu kujisomea mada mbali mbali zinazohusu biashara za mtandao na fursa za kufanya biashara za mtandao zinazotolewa na kampuni za Green World Tanzania . Humo unaweza kuona wasomaji wengine wana maoni gani kuhusu mada zetu tunazoziandika. Pia unakaribishwa kuona video mbali mabali zinazohusu biashara ya mtandao ya kampuni ya Green World kwenye channel yetu ya YouTube.

Kutembelea blog bofya HAPA.
Kutembelea channel yetu ya YouTube bofya HAPA.

 

Kwa mawasiliano nasi tuma tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: +255 655 858027 au +255 756 181651.

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii