Ugonjwa Wa Kisukari Ni Nini?
Neno ugonjwa wa kisukari linajumuisha magonjwa yote yanayosababisha kiwango cha sukari katika mwili wa mtu kuwa juu. Tunasema mtu ana tatizo la kisukari pale ambapo mwili wa mtu huyu unakuwa na ukosefu wa insulin katika mfumo wake wa damu au pale ambapo mwili wake unashindwa kutumia insulin iliyopo katika mwili wake hivyo kusababisaha kiwango cha sukari katika mwili kupanda. Hii ndiyo aina ya kisukari inayowasumbua watu wengi zaidi (diabetes mellitus) ingawa kuna aina zingine za kisukari. Sukari tunayoizungumzia hapa si ile ambayo huuzwa madukani (sucrose) bali ni carbohydrate asilia (glucose) ambayo hupatikana kwa wingi kwenye vinywaji baridi (soda) na kwenye matunda.
Kiwango cha glucose katika damu hudhibitiwa na homoni. Kuna homoni nyingi zinazofanya kazi hii ikiwa ni pamoja na ile inayotengenezwa na kongosho, iitwayo insulin. Homoni ni kemikali zilizopo katika mwili wa binadamu na zinafanya kazi ya kutuma ujumbe tofauti kutoka seli moja hadi nyingine. Unapokula chakula, kiwango cha sukari huongezeka katika mwili wako na insulin hutuma ujumbe kuzitaarifu seli zinazohitaji glucose kuchukua sukari hiyo kutoka kwenye mfumo wa damu. Seli zikiisha kuchukua glucose ya kutosha kwa matumizi yao, ile ya ziada hutunzwa katika baadhi ya seli kama Glycogen. Kama mwili haupati chakula, seli huvunjavunja glycogen iliyotunzwa na kuibadili kuwa glucose kwa matumizi ya mwili. Iwapo insulin haifanyi kazi yake kiwango cha sukari mwilini hupanda. Gluocose hutumiwa na seli kuleta nguvu mwilini.
Kutokana na ufafanuzi wetu wa kisukari cha aina hii hapo juu, tunaona kwamba kuna aina mbili au makundi mawili ya watu wanaosumbuliwa na kisukari cha aina hii, type 1 diabetes mellitus na type 2 diabetes mellitus.
Aina Ya Kwanza Ya Diabetes Mellitus (Type 1 Diabetes Mellitus)
Aina hii ya kisukari inatokea pale sehemu ya kongosho linalotengeza insulin inapokuwa imeharibika na kongosho halitengenezi insulin tena. Hali hii ikitokea, sukari (glucose) iliyopo ndani ya damu haiendi kwenye sehemu za mwili zinazohitaji sukari hiyo. Kumsaidia mtu huyu aishi, lazima apewe insulin kwa maisha yake yote yaliyosalia. Tatizo la aina hii ya kwanza ya diabetes mellitus huwakumba zaidi vijana ingawa huweza kutokea kwa watu wenye umri mkubwa pia. Imeonekana kwamba kati ya kila watu 10 wenye kisukari, mmoja huwa na aina hii ya kisukari.
Aina Ya Pili Ya Diabetes Mellitus (Type 2 Diabetes Mellitus)
Aina hii ya pili ya kisukari ni tofauti kabisa na ile aina ya kwanza kwa sababu hapa mtu ana uwezo mzuri wa kutengeneza insulin lakini mwili unashindwa kuitumia insulin hiyo au kiwango kinachotengenezwa kinakuwa kidogo sana.
Katika hali hii sukari iliyopo katika mwili hushindwa kuongozwa kwenda kwenye sehemu husika. Aina hii ya kisukari hujibainisha zaidi kwa watu wenye umri mkubwa na walio na uzito mkubwa (wanene).
Dalili Za Ugonjwa Wa Kisukari
Hapa chini ni dalili za ugonjwa wa kisukari:
- Kukojoa mara kwa mara, kusikia kiu kila mara na kupungua uzito bila kukusudia
- Mwili kushindwa kupata hisia mbalimbali kama mgandamizo au joto
Madhara Ya Ugonjwa Wa Kisukari
Kisukari ambacho hakitadhibitiwa kinaweza kuleta madhara mengi sana baada ya miaka kadhaa ingawa madhara haya yanaweza kuanza kujionyesha baada ya miezi michache tu kwa watu wengine. Madhara haya huanza kujionyesha kidogo na kuongezeka kadri miaka inavyoongezeka.
Matatizo mengi yanaanzia kwenye mishipa ya damu. Kiwango cha sukari mwilini kikiwa juu kwa muda mrefu bila kudhibitiwa, husababisha mishipa midogo na mishipa mikubwa ya damu kusinyaa. Kusinyaa huku kwa mishipa husababisha kiwango cha damu inanyofika kwenye viungo mbalimbali vya mwili kuwa kidogo na hapo ndipo mwanzo wa matatizo. Kiwango hiko cha sukari kisipodhitiwa husababisha pia chembechembe za mafuta katika damu kupanda na kusababisha hali ambayo kiutaalamu huitwa atherosclerosis. Atherosclerosis ni hali ambayo chembechembe za mafuta zinajijenga kwenye kuta za mishipa ya arteri ya ukubwa wa kati na ukubwa mkubwa na kupunguza kiwango cha damu itakayopita au kuzuia kabisa damu isipite. Atherosclerosis ndio chanzo cha heart attacks na kiharusi (strokes).
Kuwa na mzunguko mdogo wa damu kwenye ngozi humsababishia mgonjwa huyu wa kisukari kupata michubuko na maambukizi kwenye ngozi. Wagonjwa hawa mara nyingi wanapata vidonda kwenye nyayo na miguu. Mara nyingi vidonda hivyo hupona kwa taratibu sana au haviponi kabisa hali ambayo huweza kupelekea sehemu ya mguu au mguu wote kukatwa.
Wagonjwa wa kisukari huwa ni rahisi kupata maambukizi ya bacteria na fungus hasa kwenye ngozi zao. Kiwango cha sukari kinapokuwa juu sana katika damu, chembechembe nyeupe za damu haziwezi kufanya kazi yake ya kupambana na maambukizi. Maambukizi yoyote huonekana makubwa na huchukua muda mrefu sana kuyaondoa.
Kuathirika kwa mishipa ya damu ya kwenye macho kunaweza kusababisha upofu (diabetic retinopathy). Inashauriwa mgonjwa wa kisukari kupimwa mwacho yake kila mwaka kuhakikisha kwamba hakuna dalili zo zote za matatizo.
Kisukari kinaweza kusababisha figo kushindwa kufanya kazi zake na kuharibu mishipa ya fahamu. Uharibifu wa mishipa ya fahamu hujionyesha kwa njia nyingi sana. Neva moja ikiharibika ghafla, kwa mfano, mkono au mguu utakosa nguvu. Uharibifu kwenye neva za ngozi humsababishia mgonjwa kuumia mara nyingi kwa sababu atashindwa kuhisi pale kiungo chake kinapogandamizwa au kugusa na kitu chenye joto kali.
Katika mada tofauti tunazungumzia dalili za kisukari na madhara ya ugonjwa huu, mazoezi na chakula kwa mtu mwenye kisukari na tiba ya kisukari kwa kutumia insulin.
Kuhusu Dawa Ya GlucoBlock
Dawa ya GlucoBlock ni kirutubisho cha asili kinachotengenezwa na kampuni ya Green World USA. Dawa hii ina madini ya chromium ambayo ni muhimu kwa mwili wa binadamu na mimea.
Dawa hii husaidia kudhibiti matumizi ya sukari mwilini na kusaidia ufanyaji kazi wa kongosho. Husaidia tatizo la kisukari na kuondoa mambo yatokanayo na tatizo la kisukari. Ni dawa bora kwa kisukari cha juu (high blood sugar).
Kama una maoni yako kuhusu makala hii au kama una maswali yo yote usisite kuniandikia kupitia promota927@gmail.com au kwa kujaza fomu hapa chini. Pia unaweza kuwasiliana nami kwa simu kupitia 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.
Viungo Vya Dawa Ya GlucoBlock
Dawa hii ina viungo vya:
– Pyridine chromic formate
– Astragalus hoangtchy extracts
– Balsam pear extract
– Gingko leaf extract
– Mulberry leaf extract
Kuagiza Dawa
Kama utapenda kuagiza dawa hii, jaza fomu hii hapa chini kisha usubiri maelekezo utayopewa kwa barua pepe au simu.