Mada hii ni mwendelezo wa mada iliyopita iliyogusia baadhi tu ya matatizo ambayo huwapata wasichana na akina mama kuhusiana na sehemu zao nyeti. Matatizo yanayotokea ni mengi mno, hivyo hapa tunanachokoza tu tukitegemea wewe msomaji utachangia zaidi. Yale ambayo tutaona yanawagusa wasomaji wengi zaidi, tutayachambua kwa kina zaidi.
Awali ya yote napenda ieleweke kwamba sisi sio madaktari bali ni watu tunaokusanya taarifa mbalimbali kutoka vyanzo mbalimbali tukiwa na imani kwamba katika kufanya hivyo wewe msomaji utanufaika kwa namna moja au nyingine. Kwa mfano tukieleza jinsi watu wengine walivyotoa ushuhuda wa kupona kwa kutumia product fulani na wewe ukaamua kujaribu na kupona, kwetu sisi tunaamini tutakuwa tumetoa msaada kwako.
Tuliona kwamba baadhi ya matatizo yanayoendana na uzazi kwa mwanamke ni miwasho ya sehemu nyeti, kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu kali na kuwa na maungo mapana au yaliyotanuka. Leo tataongeza baadhi ya matatizo tuliyoona yanafaa kutajwa. Twende moja kwa moja:
1. Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La ndoa
Hii ni hali anmbayo huwapata wanawake ambapo hawatasikia hamu ya kufanya tendo la ndoa (loss of sexual drive or loss of libido). Mara nyingi wanawake waliolalamika kuhusu tatiza hili ni wale ambao wamezaa na wanadai tatizo lilitokea mara ya baada ya uzazi. Kuna njia za kutatua tatizo hili kama tutakavyoona wakati tutakapoichambua mada hii kwa kina.
2. Kutokufika Kileleni
Kutokufika kileleni (loss of orgasm) ni tatizo ambalo ni kubwa hasa katika nchi zetu. Usishangae kuona wakati tunajadili mada hii halafu mwanamke akauliza – “Hivi kwani kufika kileleni ni nini?.” Hili ni swali la kawaida miongoni mwa akina dada au akina mama hapa kwetu. Wenzetu wanatofautisha kufika kileleni kwa namna mbili – clitoral orgasm na vaginal orgasm. Unayajua hayo? Ni ukweli kwamba kuna wanawake wanaokuja kubahatika kufika kileleni miaka mingi (hata zaidi ya 10) baada ya ndoa zao na wengine hawajui kabisa kufika kileleni katika maisha yao yote.
3. Uyabisi Wa Sehemu Nyeti (Vaginal Dryness )
Mwanamke anapokuwa tayari kwa kufanya tendo la ndoa kuna ute unaotoka sehemu zake nyeti ili kulainisha maungo yake. Endapo ute huo hautatoka au ukitoka kwa kiwango kidogo sana, mwanamke atasikia maumivu wakati wa tendo zima. Hali hii ndio tuliyoiita “uyabisi wa sehemu nyeti.”
4. Maumivu Wakati Wa Kufanya Tendo La ndoa
Kuna wanawake wengine hupata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa kutokana na sababu nyingine nyingi tofauti na uyabisi tulioutaja hapo juu. Utatuzi wa suala hili utategemea hali inayotokea au maelezo kutoka kwa mwenye tatizo hili.
Kwa maelezo zaidi na ya kina, tuma ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au tutumie barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.