Lijue Tatizo La High Blood Pressure

 

kupima blood pressure

 

Watu wengi wanasumbuliwa na tatizo la mgandamizo wa damu kuwa mkubwa na kwa lugha nyepesi ya mtaani watu huliita tatizo hili – blood pressure. Katika ukurasa wetu wa leo tumedhamiria kueleza nini maana ya mgandamizo wa damu kuwa mkubwa (high blood pressure), dalili ambazo ukiziona ujue kuwa unanyemelewa na tatizo hili, namna ya kupima mgandamizo wa damu na tiba ambazo unaweza kutumia pale itakapobainika pasi shaka kuwa una tatizo hili la high blood pressure.

Kwanza tuwekane sawa kuwa msukumoo wa damu ni muhimu kwa maisha yetu, bila kuwepo na msukumo wa damu wa kuifanya damu izunguke ndani ya miili yetu, hewa ya oksijeni na virutubisho havingeweza kupita kwenye ateri na kuvifikia viungo vya miili yetu. Sasa msukumo huu wa damu unaweza kuwa mkubwa mno (Hypertension), au mdogo mno kuliko inavyostahili na hapo ndipo tunasema kuna tatizo. Kuna kipimo kinachotakiwa ili kuziwezesha
chembechembe za damu, zikiwemo chembechembe za damu nyeupe kwa ajili ya kinga, kuzunguka katika miili yetu.

 

Mgandamizo Wa Damu (Blood Pressure) Ni Nini?

 

Mgandamizo wa damu ni nguvu ya damu ya kusukuma kuta za mishipa ya damu. Nguvu hiyo inategemeana na uwingi wa damu inayosukumwa na moyo na uwezo wa mishipa ya damu ya arteri wa kuhimili nguvu hiyo. Kiwango cha damu inayosukumwa na moyo kikiwa kikubwa na kipenyo cha arteri kikiwa kidogo, mgandamizo wa damu kwenye kuta za arteri hizo utakuwa mkubwa. Kadri uwingi wa damu utakavyoongezeka kutoka kwenye moyo au kipenyo cha arteri kitakavyopungua, ndivyo mgandamizo wa damu kwenye kuta za arteri utakavyoongezeka.

High blood pressure ni hali ya kuwepo kwa muda mrefu kwa mgandamizo wa damu kwenye kuta za arteri ambao ni mkubwa kiasi cha kuweza kuleta matatizo ya kiafya.

 

hypertension - mgandamizo wa damu kuwa mkubwa

 

Unaweza kuwa na tatizo hili la kuwa na mgandamizo mkubwa wa damu – high blood pressure au hypertension – kwa miaka mingi bila kuanza kuona dalili zo zote au kutopata matatizo yo yote. Pamoja na kuwa hujaanza kuona dalili zo zote, uharibifu wa mishipa ya damu na moyo huendelea na baadaye unaweza kupata matatizo makubwa ya kiafya kama shinikizo la damu (heart attack) na kiharusi (stroke). Yafaa basi kujipima na kujua mapema kuwa una tatizo la high blood pressure ili uanze kuidhibiti hali hiyo.

Tatizo la kuwa na mgandamizo mkubwa wa damu huongezeka taratibu kwa miaka mingi na karibu kila mmoja wetu huathiriwa na tatizo hili. Inakladiriwa kuwa ifikapo 2025, watu bilioni 1.56 katika dunia watakuwa wanaishi na tatizo hili. Bahati nzuri ni kuwa linaweza kugundulika kirahisi sana na kudhibitiwa.

 

High Blood Pressure Ni Nini?

 

Mgandamizo wa damu (Blood Pressure) hupimwa kwa kulinganisha mgandamizo wa damu kwenye kuta za arteri wakati moyo unasukuma damu ( systolic reading) na mgandamizo huo wakati moyo unajilegeza na kuruhusu damu kujaa ndani yake (diastolic reading).

High blood pressure ni kuwa na mgandamizo wa damu unaozidi 140 juu ya 90 mmHg, kama inavyochukuliwa na vyombo vya mwongozo wa tiba.

 

kupima blood pressure

sphygmomamometer

 

Maana yake ni kuwa, mtu atahesabika ana tatizo pale mgandamizo wake wa damu utakapozidi 140 mmHg wakati wakati moyo unasukuma damu na unapozidi 90 mmHg moyo wake unapojilegeza na kujaza damu. Kiwango hiki kimewekwa kwa ajili ya ufanisi katika tiba. Viwango vya chini ya hivi ni vizuri zaidi kwa afya, na nchi nyingine zinaelezea kwa undani zaidi viwango hivi kama ifuatavyo:

. Normal blood pressure ni kuwa kipimo chini ya 120 systolic na chini ya 80 diastolic
. Prehypertension ni 120-139 systolic au 80-89 diastolic
. Stage 1 high blood pressure (hypertension) ni 140-159 systolic au 90-99 diastolic
. Stage 2 high blood pressure (hypertension) ni 160 au juu zaidi systolic au 100 au juu zaidi diastolic
. Hypertensive crisis (Hali mbaya) ni wakati mgandamizo ni juu zaidi ya 180 systolic au juu ya 110 diastolic.
Mgandamizo mkubwa wa damu unaweza kuleta matatizo kwenye viungo vitakavyoathiriwa na mgandamizo huo. Mgandandamizi huo mkubwa wa damu ukienda kwa muda mrefu unaweza kusababisha yafuatayo kutokana na mishipa ya damu kusinyaa (arteriosclerosis).

. Kupanuka au kudhoofika kwa moyo hadi kufikia kushindwa kusukuma damu ya kutosha (heart failure)
. Aneurysm – uvimbe mkubwa kwenye kuta za arteri
. Kusinyaa kwa mishipa ya damu – kwenye figo, na kusababisha figo kushindwa kufanya kazi; na kwenye moyo, ubongo na miguu na kuweza kusababisha moyo kushindwa kuendelea kufanya kazi, kiharusi au kukatwa miguu.
. Mishipa ya damu kwenye macho inaweza kupasuka na kusababisha macho kutoona vizuri au upofu ( (hypertensive retinopathies)

 

Sababu Za High Blood Pressure

 

Mgandamizo wa damu katika mwili huwa na kawaida ya kubadilika, hushuka wakati mtu amelala na kupanda anapoamka. Hupanda vilevile mtu anaposhikwa na butwaa, anapokuwa na wasiwasi na wakati anafanya shughuli za nguvu zinazotumia viungo vya mwili. Kwa hiyo ni jambo la kawaid kuwa na mgandamizo mkubwa wa damu kwa vipindi vifupi, mtu atahitaji kuwa makini pale vipimo vinapobakia kuwa juu muda wote.

Sababu za kuwa na high blood pressure (Hypertension) ni pamoja na:

Staili ya maisha: Baadhi ya sababu za high blood pressure zinazotokana na mtindo wa maisha ni:

. Kutojishughulisha
. Chumvi kwenye chakula cha kusindikwa na chenye mafuta
. Pombe na uvutaji wa tumbaku
. Chakula kisicho na madini ya potassium ya kutosha
Mambo mengine ni pamoja na:

Umri: Kila mtu anakuwa hatarini kupatwa na high blood pressure umri wake unapokuwa mkubwa. Tatizo huonekana zaidi kwa watu wenye umri wa miaka 60 na zaidi.
Urithi: Wamarekani weusi wanapatwa zaidi na tatizo hili kuliko watu weupe
Uzito: Watu wenye uzito mkubwa au wanene wapo kwenye hatari kubwa zaidi
Jinsia: Pamoja na kuwa jinsia zote zipo hatarini, wanaume huwa kwenye hatari wakiwa kwenye umri mdogo wakati wanawake hupatwa zaidi na tatizo hili wanapokuwa na umri mkubwa
Msongo wa mawazo: Msongo wa mawazo huongeza hatari ya kupata tatizo la high blood pressure

Sababu hizi zote tulizoziorodhesha hapo juu husababisha aina ya high blood pressure inayoitwa Primary Hypertension. Primary hypertension huwa haitokani na chanzo kimoja bali ni mchanganyiko wa sababu kama tulizoziorodhesha hapo juu – haina chanzo kimoja kinachoeleweka moja kwa moja. Kwa nyongeza; ujazo wa plasma katika damu na homoni ya kudhibiti ujazo wa damu na mgandamizo wa damu, pia huchangia kwenye aina hii ya high blood pressure.

Aina ya high blood pressure ambayo chanzo chake kinaeleweka -ambayo inatokana na chanzo kingine – huitwa Secondary hypertension. Mifano ya vyanzo vya aina hii ya high blood pressure ni:

. Ugonjwa wa figo
. Saratani aina ya Pheochromocytoma
. Cushing syndrome inayotokana na matumizi ya madawa (corticosteroid drugs)
. Congenital adrenal hyperplasia – matatizo ya tezi ya adrenal
. Hyperthyroidism – tezi ya thyroid kufanya kazi zaidi

 

Tiba Ya High Pressure

 

Kubadili namna ya mtu anavyoishi ndicho kitu muhimu zaidi katika kuzuia na kutibu tatizo la high blood pressure, na hili linaweza kuwa na matokeo mazuri kama yale ya kutumia dawa. Wataalamu wanashauri yafuatayo katika kupunguza blood pressure:

. Kupunguza matumizi ya chumvi
. Kupunguza unywaji wa pombe
. Kuongeza ulaji wa mboga za majani na matunda
. Kupuguza uzito wa mwili
. Kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara – mtu mwenye high blood pressure anashauriwa afanye mazoezi kama ya kutembea, jogging, kuendesha baiskeli, kuogelea kwa angalu dakika 30 kwa siku, mara 5 hadi 7 kwa wiki.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wetu wa Facebook wa LINDA AFYA YAKO kupata mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya mwanadamu na tiba mbalimbali. Usikose kuweka LIKE endapo utafurahishwa na mada hizo.

 

Usisite kuulizwa swali ulilo nalo au kutoa maoni yako binafsi kuhusu mada hii yetu ya leo. Tutafurahi sana kusikia kutoka kwako.

Kwa mawasiliano na maelezo zaidi tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: +255 655 858027 au +255 756 181651.

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii