Mabadiliko Ya Uongozi Wa Green World

 

 

machinga complex office

 

Historia

Mnamo wiki mbili za mwisho za mwezi Oktoba 2017, Meneja wa Green World Tanzania Branch alitutaarifu wanachama tunaoishi Dar Es Salaam kuwa ofisi ya Green World inatakiwa ifungwe katika siku 3 na kwamba tayari taratibu za kuuza samani za kampuni zilikuwa zimeanza. Sababu halisi za kufungwa kwa ofisi hazikufafanuliwa. Na hadi kufika Novemba mosi, hapakuwepo shughuli zo zote za kiofisi.

Baadaye meneja aliandaa kikao cha watu wachache na kueleza kuwa shughuli za kampuni zitaendeshwa kupitia maduka (shops) zilizopo ambazo moja ipo Mwenge, nyingine Arusha, Tabata, Makumbusho na Karume (Machinga Complex Building). Na ili kupata bidhaa na bonasi za wanachama, meneja alitushauri maduka hayo kuchagua kufanya kazi kutoka Nairobi, Lusaka au Kampala.

Kilichofanyika

Baada ya kauli hizo za meneja wetu, baadhi ya wenye maduka walienda Lusaka na wengine Nairobi ili kukamilisha taratibu za kuagiza mizigo na kupata bonasi za wanachama.

Kwenye ukurasa huu, nitazungumzia kilichofanyika kwa duka namba T029 ambalo linamilikiwa na mwanachama ndugu Laurian Mwajombe.

Ndugu Laurian Mwajombe alielekea Nairobi ili kukutana na uongozi wa huko ambako alipata mwongozo mkubwa kutoka kwa ndugu Lucy (Green World 3* Manager). Akiwa huko alifika makao makuu ya Green World Nairobi na kupata mwongozo wa jinsi ya kuagiza bidhaa, kupata bonasi za wanachama wa duka namba T029, orodha na bei za bidhaa zilizopo na mengineyo mengi ya msingi.

Yatokanayo

1. Taratibu za Kenya zinahitaji mauzo yafanyike mwisho tarehe 30 au 31 ya kila mwezi. Kwa mantiki hiyo, kwetu hapa Tanzania, mauzo yafanyike mwisho tarehe 27 ya mwezi ili kupata muda wa kuandaa na kupeleka marejesho Nairobi.

2. Bonasi zitatumwa kila tarehe 20 ya mwezi.

3. Wanachama ambao hawapo ndani ya T029, ili waweze kupata bonasi zao kutoka Nairobi kama watapenda kufanya hivyo, watapaswa kutoa maombi yao na yatapelekwa Nairobi.

3. Kunaweza kukatokea mabadiliko kidogo katika bei ya bidhaa kutokana na tofauti za pesa za Tanzania na Kenya.

4. Bonasi za mwezi huu hazitaweza kutolewa kwa sababu ya kuchelewa kuziwasilisha Nairobi. Lakini BV zote hazipotei, badala yake zitaunganishwa na za mwezi huu na bonasi ya jumla kutolewa tarehe 20 ya mwezi ujao.

5. Duka letu lipo Karume ndani ya jengo la Machinga Complex. Tupo ghorofa ya 3 karibu na ofisi za DRFA (Dar Es Salaam Region Football Association).

6. Wanachama wapya watapata kadi zao kutoka Nairobi. Itachukua muda kidogo kupata kadi zao na start kit zao kwani zitaletwa pale tutakapokuwa tumeagiza products.

7. Itachukua muda kidogo kupata fomu za manunuzi na za  kuunganisha wanachama wapya kwani gharama hizi zote ni kwa mwenye duka.

8. Sasa hivi ofisi ya Kenya haitoi zawadi ndogo. Zawadi hizi ni za 3*C , 4*C na 5*C katika mwezi mmoja. Wanaanzia zawadi ya 6*C katika miezi 6 (Tripu ya China).

Mwisho

Tunaomba wanachamma kuwa watulivu na kusoma maelezo haya kwa kina na kuyatafakari. Kama kuna maswali, usisite kuyauliza. Tunakuomba kwa kipindi hiki cha mwanzo kutunza BV vizuri zako na kuzifuatilia kutoka kwenye tovuti ya kampuni.

 

Laurian