Mwongozo Wa Tiba Ya Mwanamke Kutokwa Uchafu Ukeni Kwa Kutumia Bidhaa Za Green World

 

mwongozo wa tiba ya uchafu ukeni

 

Katika jamii yetu wanawake wengi wanasumbuliwa sana na tatizo la kutokwa na uchafu ukeni. Kampuni ya Green World ina bidhaa nyingi za kuweza kusaidia tatizo hilo. Kwa vile aina za matatizo hayo ni nyingi na zinatofautiana, nimeona nijaribu kutoa dalili kwa aina zinazosumbua sana na kuelekeza ni bidhaa gani za kampuni ya Green World zinazoweza kutumika.

Kutoka uchafu sehemu za siri kunaweza kusababishwa na sababu nyingi. Kuna matatizo ya kiafya kama kutokuwa na mpangilio mzuri wa homoni au kuvurugika kwa hedhi yanayoweza kusababisha mwanamke atokwe na uchafu ukeni. Maambukizi ya wadudu ni sababu nyingine ya mwanamke kutokwa na uchafu ukeni.

Uke wa mwanamke ulio kwenye ubora wake una aina nyingi sana za bakteria na idadi ndogo ya fungus (yeast cells) wanaoishi humo. Kuna bakteria wabaya na bakteria na fungus rafiki. Bakteria rafiki hufanya kazi ya kuwadhibiti bakteria wabaya. Bakteria mmoja anayejulikana sana ni lactobacillus acidophilus ambaye anafanya kazi ya kuwaweka viumbe wengine pamoja na fungus kwenye idadi inayotakikana. Inaweza ikatokea kuwa idadi ya bakteria wabaya ikawa zaidi ya idadi ya bakteria rafiki.

Inapotokea kuwa uwiano wa viumbe hao umebadilika, matatizo yataanza kujitokeza kwenye mazingira ya uke. Uwiano huo unaweza kuvurugika kwa kutumia antibiotics au kwa sababu ya kuongezeka kwa homoni ya estrogen kutokana na kubeba mimba au matumizi ya dawa za kuiongeza homoni hiyo. Sababu nyingine ni kama kisukari au maambukizi ya HIV. Hali hiyo inaweza kusababisha kuongezeka kwa idadi ya baadhi ya bakteria au fungus kuliko kiwango kinachotakiwa na hapo ndipo uke wa mwanamke unapoanza kutoa uchafu zaidi.

Hapa chini ni mwongozo kwa matatizo yanayojitokeza zaidi kwenye jamii yetu:

 

1. Cytolitic Vaginosis

 

Uke wa mwanamke huwa na uwingi wa bakteria waitwao lactobacilli. Bakteria hawa hutengeneza tindikali, lactic acid, ambayo huweka sawa pH ya uke, na hydrogen peroxide ambayo ni antiseptiki – aina ya kemikali inayozuia kukua kwa bakteria. Lactobacilli huulinda uke dhidi ya wadudu wabaya.

Cytolitic vaginosis ni hali ambapo idadi ya lactobacilli imezidi kiwango na kuwafanya bakteria hawa kushambulia seli za ngozi laini ya uke, na kuzifanya zivunjike. Seli hizi zilizoharibiwa hutoka nje ya uke pamoja na uchafu wa kawaida.

Dalili:

. Uchafu mweupe, mwepesi au mzito
. Miwasho ndani ya uke au nje (pruritus vulvae)
. Maumivu hasa wakati wa kukojoa (dysuria)
. Maumivu wakati wa tendo la ndoa (dyspareunia)

Tiba:

Hakuna tiba maalumu kwa tatizo hili. Yafuatayo yanaweza kusaidia kuongeza pH ya uke na hivyo kupunguza mwongezeko wa lactobacilli:

– Kupunguza au kuacha kutumia sukari
– Kuacha kutumia sabuni au maji ya baridi
– Kuacha kutumia antibiotics au dawa za fungus
– Kujisafisha kwa kutumia baking soda (Sodium Bicarbonate). Koroga vijiko 2-4 kwenye glasi moja ya maji ya vuguvugu.
– Kutumia Royal Jelly Capsules

 

2. Yeast (Monilia) Infection

 

Mazingira ya ukeni yakibadilika yeast, fungus wanaoishi katika uke, wanaweza kuongezeka. Seli za fungus hawa zikiongezeka kwa kiasi kikubwa sana, zinaweza kuleta usumbufu na tunasema kuna maambukizi. Maambukizi mengi huletwa na yeast aitwaye Candida Albicans. Kwa kawaida idadi ya seli za candida albicans hudhibitiwa na lactobacillus acidophilus.

Dalili:

. Uchafu mweupe, vifungu vidogodogo kama jibini
. Kuwashwa na uvimbe sehemu ya nje (vulva)
. Maumivu wakati wa tendo la ndoa

Tiba:

– Kutumuia dawa za kuua fungus
– Kutumia Royal Jelly Capsules
_ Kutumia Propolis Capsules

 

3. Trichomoniasis

 

Trichomoniasis (“trich”) ni maambukizi yanayotokana na ngono yakienezwa na protozoa wa seli moja aitwaye Trichomonas vaginalis. Ni ugonjwa unaotibika kirahisi.

Dalili:

. Uchafu mweupe, wa grey, njano au kijani unaotoka kama mapovu, wenye harufu mbaya
. Kuwashwa ukeni
. Maumivu ukeni au nje (vulva)
. Kusikia haja ndogo mara kwa mara
. Maumivu wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa

Tiba:

– Kutumia Garlic Oil Softgel, Aloe Vera capsules au Propolis capsules
– Kutumia Royal Jelly Softgel
– Kutumia Cordyceps capsules
– Kutumia Ginseng RHS
– Kutumia Pine Pollen Tea

 

4. Bacterial Vaginosis

 

Bacteria vaginosis ni hali ambapo idadi ya bakteria wabaya inapoongezeka ukeni. Hakuna sababu maalumu inayoeleweka kitaalamu. Hali hii inaweza kujitokeza kiurahisi kwa wale wanaoshiriki ngono na wapenzi wengi au unaposhiriki ngon o na mtu mpya. Kujiosha ukeni na maji na kuvuta sigara vimeonekana pia kuchangia hali hii.

Dalili:

. Uchafu mweupe, njano au wa kijivu mwepesi wenye harufu ya samaki
. Miwasho na kuvimba ukeni
. Harufu inayozidi baada ya tendo la ndoa

Tiba:

– Kutumia Garlic Oil Softgel, Aloe Vera capsules au Propolis capsules
– Kutumia Royal Jelly Softgel
– Kutumia Cordyceps capsules
– Kutumia Ginseng RHS
– Kutumia Pine Pollen Tea

 

5. Kuvurugika Kwa Hedhi Au Kansa Ya Cervix

 

Hedhi iliyovurugika au saratani ya shingo ya uzazi huweza kusababisha mwanamke atokwe na uchafu ukeni.

Dalili:

. Uchafu wenye damu au wenye rangi ya kahawia
. Kuumwa nyonga

Tiba:

– Royal Jelly Softgel
– Pine Pollen Tea
– A Power capsules
– Soy Power capsules (usiitumie kama fibroids ni chanzo cha tatizo)      _   Kidney Tonifying capsules                                                                                            – Propolis                                                                                                                                    – Ginseng

 

6. Kisonono

 

Kisonono (Gonorrhea) ni maambukizi ya bakteria aitwaye Neisseria gonorrhoeae. Bakteria huyu hushambulia maeneo ya mrija wa mkojo (urethra), koo, mkundu na shingo ya uzazi (cervix).
Baada ya muda, bakteria hawa husambaa hadi kwenye mfumo wa damu na sehemu nyingine za mwili. Hali hii huitwa systemic gonococcal infection au disseminated gonococcal infection (DGI).

Dalili:

. Uchafu wa mawingu au njano
. Damu katikati ya siku
. Mkojo kutoka bila kukusudia
. Maumivu ya nyonga

Tiba:

– Kutumia Garlic Oil Softgel, Aloe Vera capsules au Propolis capsules
– Kutumia Royal Jelly Softgel
– Kutumia Cordyceps capsules
– Kutumia Ginseng RHS
– Kutumia Pine Pollen Tea

 

Laurian.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii