Semina Ya Budiman Palace Hotel – Arusha

 

Semina ya Budiman Arusha

 

Katika mfululizo wa semina za mkufunzi kutoka Toronto Canada, ndugu Budiman, ya mwisho ilifanyika siku ya jumamosi ya tarehe 1 Oktoba 2016. Semina hii ilifanyika mjini Arusha katika ukumbi wa Jumbo Hall na ilianza muda wa saa 10 jioni.

Kama ilivyotarajiwa, wakazi wa mji wa Arusha walikuja kwa wingi kumsikiliza mkufunzi huyu wa kimataifa. Semina hii ilianza kwa mkufunzi kuitambulisha kampuni ya Green World International. Alitoa historia ya kampuni hii na kutoa mifano ya watu wengi walioweza kunufaika na kampuni ya Green World katika kuboresha afya zao za kimwili na afya za mifuko yao.

Kivutio kikubwa katika semina hii ni maelezo yaliyotolewa na mwanachama wa kampuni hii ya Green World, ndugu Mbuya, ambaye ni mwenyeji wa Arusha alipoelezea mafanikio yake. Mwanachama huyo alieleza kuwa alijiunga na kampuni hii mwaka 2008 na hadi sasa pamoja na kuwa amekuwa akipata kipato kikubwa kila mwezi, ameweza kupata ziara zaidi ya sita za kwenda kupumzika nje ya nchi na zawadi za magari 15 kila moja likiwa na thamani ya Tshs. milioni 20.

Semina hii ilifungwa kwa namna ya kipekee pale sista wa madhehebu ya kikatoliki alipotoa sala iliyoambatana na wimbo mtamu aliouimba kwa lugha ya kiingereza. Kwa hakika waliohudhuria semina hii walipata mafunzo yenye thamani kubwa, kiingilio kikiwa ni BURE – kwa hisani ya mkufunzi huyo.

Mkufunzi huyo anatarajiwa kuondoka tarehe 6 Oktoba, kuelekea kwao Canada.

 

Laurian.