Siri Za Kufanikiwa Katika Biashara Za Mtandao

 

Jee, Unafamu Siri Za Kufanikiwa Kwenye Biashara Za Mtandao?

 

Watu wengi sana sasa hivi wanajiunga na makampuni mbalimbali ya biashara za mtandao ili weweze kubadlisha hali zao za maisha. Katika kufanya biashara hizo wapo watu waliofanikiwa sana na wengine ni mabilionia kwa sababu ya biashara hizi. Sina mfano wa kuutoa hapa kwetu Tanzania lakini nchini Afrika ya Kusini namfahamu mama mmoja ambaye sasa ni bilionia kwa kufanya biashara hizi. Hakuwa na mtaji mkubwa wa kuanzia, yeye alikuwa mwalimu tu katika shule za kawaida. Mama huyu alianza kwa kujitibu mwenyewe upofu alioupata akiwa mwalimu kwa bidhaa za kampuni ya Green World. Baada ya kupona aliamua kujiunga na kampuni hiyo na kuuza bidhaa zake. Leo hii mama huyu ni bilionia mwenye majumba mengi ya kifahari na hata villa huko nchini Afrika ya Kusini. Jee, mafanikio yake ni bahati tu au kuna siri gani aliyoitumia? Si yeye tu, watu wengine wengi waliofanikiwa katika biashara hizi wana vitu walivyovijua na kuvizingatia. Leo katika ukurasa huu nitakupa siri za kufanikiwa katika biashara za mtandao ambazo mama huyu pamoja na wengine wote waliofanikiwa wamezitumia.

 

Mrs Thambisile, Green World South Africa

 

Siri hizi ninazokupa hapa leo zinafuatia baada ya kupata kampuni yako nzuri ya mtandao, haitakusaidia kuyafanya haya ninayokueleza hapa leo endapo umeangukia mikononi mwa kampuni mbovu. Katika ukarasa mwingine “Namna Ya Kuchagua Kampuni Ya Mtandao” nilieleza vigezo vya kuvitazama ili upate kampuni ya mtandao iliyo bora. Kama hujausoma ukurasa huo, nashauri uupitie kwanza.

Moja Kwa moja tuanze kujielimisha juu ya siri hizo za mafanikio katika biashara za mtandao zinazowatenganisha wafanya biashara katika makundi mawili, wanaofaulu na wanaoshindwa. Zingatia siri hizi na moja kwa moja utakuwa katika kundi la wanaofaulu.

 

1. Kujenga Fikra Sahihi Za Mafanikio

 

Ebu tuone tabia moja waliyonayo walio wengi. Mtu ataelezwa na ndugu au rafiki yake kuhusu fursa ya biashara katika kampuni fulani. Atajiunga shingo upande akisema “Ah, ngoja nijaribu bwana pengine Mungu atasaidia”. Hatawekeza muda wake katika kujifunza kuhusu kampuni hiyo na hatashiriki kwa nguvu zake zote katika kuuza bidhaa za kampuni hiyo. Baada ya siku chache, atasoma tangazo la kampuni nyingine inayodai kukupa mamilioni katika muda mfupi sana. Atajiunga na kampuni hiyo mpya akisema kuwa ile ya kwanza haikuwa nzuri. Hivyo hivyo ndio mlolongo wa kujiunga na makampuni utaendelea. Baada ya miaka michache atawaambia watu wengine kuwa “Biashara Za Mtandao Ni Feki Bwana, Uwongo Mtupu.” Jee, wewe linakugusa hili?

Kupata mafanikio inabidi kwanza uwe na picha sahihi ya kuwa wewe ni nani, upo wapi, unataka kufanya nini na unataka kufika wapi.

Nitakudokezea kanuni moja “The Law of Attraction” ambapo inasema binadamu anapata kile anachokifiria zaidi. Ukiwaza kila wakati kuhusu mafanikio, utapata mafanikio. Kama muda wako mwingi unautumia kuwazia matatizo, utapa matatizo. Ni kanuni madhubuti, haina mbadala. Watu waliofanikiwa wameijua na kuitumia kanuni hii kwa karne nyingi.

 

Kanuni ya The law of attraction

 

Sheria hii inatufundisha nini? Tunajifunza kuwa kwanza inabidi kuchagua kitu unachokipenda kukifanya na ambacho kipo ndani ya uwezo wako. Ukishakipata wazo lako au biashara yako, panga unataka kufanya nini na unataka kufikia wapi. Kisha amini kwamba utafanikiwa na ifanye imani yako hiyo kuwa sehemu ya maisha yako. Ni njia yako ya kukufikisha kwenye mafanikio na si nyingine. Huwa naupenda sana msemo mmoja wa wenzetu kwa tafsiri yangu unasema hivi “Kama Hujui Unakokwenda, Njia Yoyote Itakufikisha Huko.” Ukiamua na kuamini kwa dhati bila kutia shaka, akili yako itafanya kazi ya kukupa nguvu na msukumo wa kuendelea. Akili yako pia itafanya kazi ya kukufungulia njia nyingine ili uweze kufanikisha lengo lako kama ulivyojipangia. Ndiyo… mafanikio yanaanza kwa kuwa na picha ya kile unachohitaji na kuamini kuwa utafakiwa kukipata.

 

 2. Kuwa Na Mpango Mzuri (Plan)

 

Ili kufanikiwa jambo lolote unatakiwa uwe na plani nzuri. Fikiria kuanza ujenzi wa nyumba bila kuwa na mchoro mkononi. Hivyo hivyo katika kufanya biashara yako lazima utengeneze plani ya utekelezaji. Tengeneza mpango ulio rahisi na unaotekelezeka. Haina maana yoyote kufikiria kufanya vitu nje ya uwezo wako, anza na vitu rahisi unavyovimudu taratibu ukiongeza spidi kadri hali itakavyoruhusu. Hutaweza pengine kufanya kila kitu wewe mwenyewe, hivyo kuomba msaada kwa wengine itakusaidia. Katika biashara za mtandao kuna mtu aliye juu yako au walio juu yako hakikisha unakuwa karibu naye/nao na unamtumia ili upate uzoefu wake wa kibiashara. Biashara za karne ya leo pamaoja na kuwa bado zinatumia njia ya mawasiliano ya mdomo, zinatumia pia mtandao hivyo tafuta mtu wa kukufundisha ujue kuitangaza biashara yako kupitia simu ya kiganjani, Facebook na mitandao mingine ya kijamii na kupitia tovuti mbalimbali.

Uwe na picha kamili ya nini unategemea kukifanya sasa, katika siku za usoni na miaka kadhaa baadaye.

Katika kutekeleza mipango yako, mambo yanaweza kwenda kinyume na matarajio yako, usihofu, ni jambao la kawaida. Tafiti kwa nini hukufikia lengo lako na fanya marekebisho ipasavyo. Inaweza kutokea kwmaba ukashindwa kabisa, bado si tatizo chukulia kushindwa kwako kama ngazi ya kuelekea kwenye mafanikio – mara nyingi kushindwa ni ishara ya mafanikio yaliyo karibu. Pale utakapoanza kupata mafanikio kidogo, chukulia hayo kama motisha kwako na ongeza juhudi.

 

 

 3. Kuanza Utekelezaji

 

Hili ndilo moja ya mambo magumu kwa walio wengi. Umeshapata ushauri kutoka kwa ndugu na marafiki, umeangalia mikanda mingi ya video, umesoma vitabu vingi na leo tena unasoma ukurasa huu. Baada ya kumaliza hapa leo unasema “Aha, Sasa ngoja nikamilishe kwanza kitu kile….. halafu nianze kwa nguvu zangu zote .” Kumbuka hiyo ni tabia tu ya kuahirisha ahirisha mambo, huhitaji kukamilisha lo lote kabla ya kuanza kitu. Anza sasa na kile kilichopo, ukamilifu utakuja taratibu ukiwa tayari unatembea.

Acha kutoa sababu. Chukua karatasi sasa, orodhesha vitu vyote vinavyotakiwa kufanywa kwa mpango wa kipi kianze kwanza na kufuatiwa na kipi. Kisha andika kipi utakifanya lini. Hakikisha kila siku umefanya kitu fulani katika kujenga biashara yako hata kama ni kidogo kiasi gani. Mafanikio yanakuja kwa hatua ndogo ndogo unazozifanya, si ghafla. Kidogo kidogo utaona kwamba unapiga hatua.

 

4. Kutohamahama Na Kutobalisha Mawazo

 

Unakumbuka hapo juu tulimzungumzia mtu anayehamahama kutoka kampuni moja hadi nyingine halafu mwisho wa siku kutangaza kuwa  biashara za mtandao ni feki? Napenda tena nitumie msemo wa wenzetu nitakaoutafsiri kuwa “Jiwe linalovingirika Kamwe Halioti Nyasi“. Vile vile kuhamahama au kubadilisha mawazo kila wakati kibiashara ni tiketi ya kufeli katika biashara hizo. Watu waliofanikiwa katika biashara hizi ni wale waliofanya maamuzi na kushikilia maamuzi yao hadi mwisho.

Watu wenye tabia ya kuhamahama wanaishia kuzungukazunguka tu bila mafanikio. Fuata njia yako nyembamba ya mafanikio uliyojiamulia mwenyewe hadi mwisho wake bila kuyumba, njiani kuna vikwazo, ni kitu cha kawaida na vina faida moja ya kukupa changamoto ili uweze kukazana zaidi. Elekeza mawazo yako na nguvu zako pale unapotaka kufika, KAMWE, KAMWE usikate tamaa wala kuyumba! Kamilisha na fikia malengo yako kabla ya kuanza kuingiza mawazo mengine yoyote mapya.

Haya ndiyo mambo ya msingi ya kuzingatia katika kufanikisha biashara yako ya mtandao uliyoichagua. Kama ni mgeni katika biashara za mtandao, naomba usome pia ukurasa wa “Biashara Ya Mtaji Mdogo: Jee, Unatafuta Kuanza Biashara Ya Mtaji Mdogo?” Hapa utajifunza maana ya biashara ya mtandao na jinsi biashara hizi zinavyoendeshwa.

Usisite kuuliza maswali na kutoa maoni yako kuhusu mada hii. Nitafurahi sana kuyasikia, kuyajibu na kuyafanyia kazi.

Laurian.

Kwa maelezo zaidi na ya kina, tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au tutumie barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au  0756 181651.

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii