Jibu ni: NDIYO
Watu wengi wakisikia neno biashara ya mtandao hufikiri ni biashara ambayo lazima uanze kutafuta watu wa kununua bidhaa zako kwa kuwapitishia majumbani mwao au mitaani. Nilishawahi kusikia mtu akikebehi; biashara gani mtu uzunguke na mzigo mgongoni! Neno jingine ni kuwa ukianza biashara hii mwisho wa siku utafute chumba cha kuhifadhi products zilizobaki, yaani kampuni itakujazia mzigo usioenda na mwisho utabakiwa na lundo la bidhaa. Napenda leo nifafanue jinsi unavyoweza kuwekeza katika biashara ya mtandao kama unavyowekeza kwenye biashara nyingine yo yote na ukapata faida za aina nyingi.
Biashara nyingi za mtandao kimsingi zinamruhusu mtu kuchagua mfumo wa biashara anaoutaka. Mfumo huu unaruhusu watu wenye mitaji midogo au wasio na mitaji kabisa kuanza kunufaika na fursa za biashara. Lakini pia zinaruhusu watu wenye mitaji mikubwa ambao wanatafuta kuwekeza kwenye biashara zisizo na usumbufu. Watu wanaohangaika na mizigo migongoni ni wale ambao kwa bahati mbaya wana mitaji midogo sana. Kwa mitaji yao, hakuna namna nyingine ya kuanza biashara isipokuwa kutafuta watu wa karibu kwanza na kuzunguka kutafuta wa nje, taratibu wakijijenga na hatimaye kutulia baadaye.
Kwa hiyo kama una mtaji mkubwa kidogo, unaweza kujiunga na kampuni ya mtandao na kuwekeza. Kwa mfano, ukijiunga na kampuni inayouza bidhaa za kuboresha afya ya binadamu, unaweza na unaruhusiwa kufungua duka na ukauza bidhaa zako hapo. Kampuni hazizuii kufanya hivyo. Unachopaswa kufanya ni kuhudhuria mafunzo ya kufahamu jinsi bidhaa za kampuni zinavyofanya kazi ili uweze kuwashauri vizuri wateja wako.
Kampuni ya uhakika lazima itakuwa na kibali kutoka TFDA kwa kila bidhaa na haizuii mwanachama wake kuomba vivuli vya vibali hivyo ili mwenye duka aweze kuvionyesha pale vitakapotakiwa.
Kampuni za mitandao hutoa faida kubwa ya reja reja kwa wanachama wao. Kampuni nyingi zinatoa faida ya kati ya asilimia 20 hadi 45, kiwango ambacho kimepangwa na kampuni na hakiruhusiwi kupunguzwa na wanachama wengine. Ushindani wa kibiashara wa mitaani wa kupunguza bei ili umzidi jirani mauzo kamwe hauruhusiwi hapa. Kampuni zenye msimamo humsimamisha uanachama mara zikibaini mtu anafanya hilo. Faida za biashara za mtandao kwa hiyo hazibadiliki na zinalindwa.
Kampuni nyingine zitakulipa pia kutokana na asilimia ya manunuzi yako kwenye kampuni. Mathalani, umenunua mzigo wa milioni 1 katika mwezi huo, na kampuni inatoa asilimia 45 ya manunuzi yako kama direct bonus, utapata 450,000/= kama bonus mwisho wa mwezi kutoka kwenye kampuni. Jumlisha na faida yako ya reja reja ambayo kama kampuni inatoa asilimia 25, ni 250,000/=. Utapata jumla ya 700,000/= katika mwezi huo kama faida ya reja reja na direct bonus.
Kampuni nyingi zina njia nyingi za kukupatia kipato na hazikuwekei mipaka. Kwa hiyo pamoja na pesa hiyo hapo juu, unaweza kutumia na njia nyingine zinazotolewa na kampuni, utakazopenda ili kuongeza kwenye kiwango hicho hapo juu, hata kama utapenda kujenga timu pia.
Biashara hizi hutoa zawadi nyingi kwa mtu anayefanya biashara vizuri. Fikiria, kuwekeza na kupata faida kubwa za reja reja na zenye uhakika, direct bonus na halafu kupewa zawadi ya safari ya kwenda nje ya nchi, gari au nyumba kutokana na biashara yako mwenyewe.
Binafsi sifikirii biashara zaidi ya hiyo ya kuifanya!
Nimetoa mfano wa mtu aliyewekeza kwenye duka la bidhaa za kulinda afya ya binadamu (virutubisho), lakini kuna aina nyingine nyingi za biashara, kama vipodozi n.k., unazoweza kuchagua na kuwekeza na kufaidi faida hizo kubwa zenye uhakika na zisizobadilika. Katika biashara za mtandao, ukomo ni uwezo wako wa kifedha na ubunifu wako.
Biashara nyingine ambayo mtu unaweza kuwekeza na kujipatia soko kubwa na hatimaye faida kubwa ni mbolea. Kampuni za mitandao zimekuja na mbolea ya aina tofauti kabisa na zile zilizozoeleka kwa miaka mingi. Mbolea hii ya aina mpya hunyunyiziwa kwenye majani ya mmea na haiharibu ardhi kama zile za kemikali. Faida moja ni kwamba mbolea hii ikitumika inakarabati ardhi iliyokwisha chakaa kwa matumizi ya aina za mbolea za kemikali. Bei ya mbolea hii ni chini sana ya zile za mbolea nyingine. Na kuna faida nyingine lukuki za kutumia aina hii ya mbolea.
Ukizingatia faida za mbolea hii ya aina mpya na uwingi wa wakulima nchini mwetu, soko lake ni kubwa mno na lenye uhakika, hivyo mtu ukiwekeza kwenye biashara hii utapata faida kubwa sana. Maelezo ya aina moja ya mbolea yanapatikana kwenye ukurasa wa ” Semina Ya Matumizi Ya Mbolea Ya Organic Ya Green world” kwenye blog ya tovuti yetu.
Yaweza kuonekana kuwa naandika ili kuzipigia debe kampuni za mitandao kwa kitu ambacho si cha kweli. Mimi binafsi nina ushahidi wa haya niliyoyandika, nafahamu kampuni ambazo zinatimiza haya na watu wengi ambao wamewekeza na wanapata faida kama nilivyoziandika ndani ya ukurasa huu. Unaweza pia kujisomea kuhusu moja ya kampuni zenye mfumo huu, Green World Tanzania.
Usisite kuuliza swali au kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo. Ni furaha kwangu kuona kuwa nimekujibu vizuri na kwa wakati.
Laurian.
Tafadhali tembelea blog yetu kujisomea mada mbali mbali zinazohusu biashara za mtandao na fursa za biashara za mtandao zinazotolewa na kampuni za Green World Tanzania naTrevo Tanzania Ltd. Humo unaweza kuona wasomaji wengine wana maoni gani kuhusu mada zetu tunazoziandika. Pia unakaribishwa kuona video mbali mabali zinazohusu biashara ya mtandao ya kampuni ya Green World kwenye channel yetu ya YouTube.
Kutembelea blog bofya HAPA.
Kutembelea channel yetu ya YouTube bofya HAPA.