Semina Ya Matumizi Ya Mbolea (Organic Fertilizer) – Green World Tanzania

mafunzo ya mbolea

Hisilicon K3

Kuna aina nyingi za mbolea ambazo wakulima wanazitumia ili kuyafanya mazao yao kukua kwa haraka na kutoa mazao mengi. Zama za kale watu walitumia mbolea ambazo walizitengeneza wenyewe. Kwenye miaka ya 60 na 70, nakumbuka wanafunzi walikuwa na somo la namna ya kutegeneza BIWI. Hili lilikuwa ni shimo lililochimbwa na baadaye majani na kinyesi cha wanyama kufukiwa ndani ya shimo hilo kwa muda fulani. Baada ya mda huo, shimo hili lilifukuliwa na mkulima alikuwa amepata mbolea nzuri kwa ajili bustani na mashamba yake.

Baadaye zilikuja mbolea ambazo ziliagizwa kutoka nje ya nchi au kutengenezwa na viwanda vyetu wenyewe. Mbolea za viwanda vya Tanga na Minjngu (Arusha) ni mifano ya mbolea hizi.

Wataalamu wa miaka ya sasa wanatufundisha kuwa mbolea hizi za viwandani (Inorganic Fertizers) zina madhara mengi na wamekuja na aina mpya ya mbolea ambazo wanaziita Organic Fertilizers.

Kampuni ya Green World ambayo ina vituo vyake vya utafiti nchini Marekani na viwanda vyake katika miji ya Tianjin na Nanjing huko China, inatengeneza mbolea iitwayo Nutriplant Organic Plus Fertilizer (NOPF). Mbolea hii ni ya majimaji na hutunzwa ndani ya kichupa cha plastiki chenye ujazo wa lita moja.

 

Mbolea -  green world

 

Katika semina iliyofanywa katika ukumbi wa kampuni hiyo ulio ndani ya ofisi za kampuni hiyo huko Upanga, Dar es Salaam, wataalamu wawili kutoka China walielezea manufaa ya mbolea hiyo kwa kutoa matokeo ya tafiti walizozifanya katika mashamba yao na kuelekeza namna ya kuitumia mbolea hiyo. Semina ilifanyika siku ya ijumaa tarehe 29 Aprili 2016 kuanzia saa 5 asubuhi.

Katika semina hiyo, Professor Gao Xiang na Bi Xu Ruijie walifundisha mambo mengi sana. Kwa kifupi walieleza haya kuhusiana na mbolea hiyo inayotengenezwa na kampuni ya Green World.

. Mbolea hiyo yenye ujazo wa lita moja huweza kuchanganywa na lita 1000 za maji kabla ya kutumika. Mbolea hii ambayo hutumika kwa kunyunyizia juu ya majani ya mimea ina uwezo wa kutumiwa kwenye eneo la shamba la ukubwa wa hekta 6.7.

. Kama mkulima atataka kutumia kwenye eneo dogo kama la bustani, atamimina kifuniko kimoja ambacho kina ujazo wa ml 50 na kuchanganya na lita 25 hadi 50 za maji.

. Mbolea hii inaweza kutumika kwa mimea ya aina zote; matunda, nafaka, mboga na hata mimea inayotunza chakula chini ya ardhi kama mihogo, karoti n.k. Mimea iliyonyunyiziwa mbolea haina madhara ikiliwa na binadamu au mifugo – maana yake mbolea hii haina sumu.

. Matumizi mazuri ya mbolea hii ni kuinyunyiza mapema alfajiri au baada ya jua kuzama. Jua kali huharibu amino acids zilizotumika kuitengeneza mbolea hii.
Kuna maelezo mengine mengi yanayomfaa yule apendaye kulima bustani au wakulima wenye mashamba makubwa. Kwa bahati nzuri wataalamu hao bado wapo nchini na wanaendelea na mafunzo kuhusu mbolea hii.

Ratiba yao wakiwa hapa nchini ni kama ifuatavyo.

Tarehe 30/4       Morogoro                                Bright Star Hotel
Tarehe 04/5       Arusha                                       Palson Hotel
Tarehe 02/5      Green World Office DSM
Tarehe 05/5      Green World Office DSM
Tarehe 06/5      Green world Office DSM
Tarhe 07/5        Green world Office DSM
Tarehe 09/5     Green world Office DSM

Wito wangu ni kwa wapenzi wa kilimo kuja kujisikilizia wenywe kuhusu mbolea hii. Kampuni inamkaribisha ye yote anayependa kujua au kuinunua mbolea hii. Hakuna kiingilio kwenye semina hizi na vinywaji vinatolewa. Kupata maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi 0655 858027 au 0756 181651 au kutuandikia promota927@gmail.com.

 

Usisite kuuliza swali lo lote ulilo nalo au kutoa maoni yako kuhusu mada hii. Ni furaha kwetu kuona kuwa tumekujibu na kwa wakati mwafaka.
Laurian.