Katika mfulululizo wa mafunzo kwa wageni yanayotolewa na kampuni ya Green World, mwezi March 2017, tarehe 5, semina ilifanyika katika mji wa Kibaya- Kiteto. Semina hiyo iliandaliwa na mwanachama Thomas Mpalazi wa mji huo na mwanachama mmoja, ndugu Laurian Mwajombe, alitoka Dar Es Salaam kwenda Kiteto kushirikiana naye kutoa mafunzo hayo.
Mafunzo yalianza saa 10.30 na yalifanyika katika ukumbi wa Community uliopo hapo mjini Kiteto.
Wageni kwa ujumla walionyesha hamasa ya juu ya kuijua fursa hii na walikuwa makini sana katika kusikiliza yale yaliyofundishwa. Kuonyesha kuwa walifuatilia vizuri kile kilichofundishwa, waliuliza maswali mengi na ya msingi mara baada ya kupewa nafasi ya kuuliza maswali yao.
Wengi wa waliohudhuria semina hiyo, waliomba kupewa nafasi nyingine kama hii ili waweze kuwajulisha ndugu zao ambao hawakupata bahati ya kuhudhuria semina hii ya mwanzao.
Laurian.