Semina Ya Green World – Nzega – Desemba 2016

 

John Bwana  semina ya Nzega

 

Kutokana na kuwa watu wengi wa mjini Mwanza wameona ubora wa bidhaa za kampuni ya Green World na kuifurahia fursa ya biashara inayotolewa na kampuni hiyo, ombi la kufanya semina mjini Nzega ili ndugu zao waweze pia kunafaika lilitolewa. Mkufunzi wa kampuni ndugu Victor, aliongozana na wanachama wawili wa kampuni kutoka Dar Es Salaam, ndugu Hilda Mahende na ndugu Laurian Mwajombe, ili kufanya semina katika mji huo wa Nzega. Pamoja nao, wanachama wawili kutoka Mwanza, ndugu John Bwana na ndugu Charles Ngalula walijumuika kwenye semina hiyo.

Semina ilifanyika katika ukumbi wa Ukwala Lodge siku ya jumamosi ya tarehe 17 Desemba 2016. Mwanachama mwenyeji wa mji huo, ndugu Zuhura Salum ndiye aliyefungua semina hiyo mnamo saa 10 ya alasiri.

Baada ya ufunguzi, ndugu John Bwana kutoka Mwanza alitoa mafunzo kuhusu historia ya kampuni ya Green World, bidhaa zinazosambazwa na kampuni hiyo na umuhimu wa kutumia bidhaa za virutubishi katika ulimwengu wa sasa uliondelea kisayansi na kiteknolojia.

Katika sehemu ya pili, mkufunzi kutoka Dar, ndugu Victor, alitoa mafunzo ya jinsi mwanachama anavyoweza kunufaika kimapato na kubadili kabisa maisha yake katika kipindi kifupi tu.

 

semina ya nzega

 

Tofauti na miji mingine mingi, watu wa Nzega walijitokeza kwa wingi na kuonyesha umakini wa hali ya juu sana katika kusikiliza yale yaliyofundishwa na kudhihirisha hilo, waliuliza maswali mengi na ya msingi sana.

Mwisho kabisa, muda ulitolewa kwa wale waliopendezewa na fursa hiyo ya biashara ili waweze kujiunga, ambapo baadhi wajiunga moja kwa moja.