Kufuatia mahitaji ya jamii kuhusu elimu ya afya, kampuni ya Green World imaeanza kuendesha semina katika ofisi yake ya Dar
Es Salaam ili kuitoa elimu hiyo kwa wananchi. Elimu hii inatolewa BURE kabisa kila siku ya jumamosi kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana.
Jumamosi ya tarehe 8 Aprili 2017, daktari Frank alitoa elimu kuhusu afya ya saratani ya maziwa na shingo ya uzazi. Daktari alieleza kwa kutumia lugha nyepesi chanzo cha saratani hizi, namna ya kujikinga, dalili zake na tiba ambazo hutolewa pale ambapo imebainika kuwa una tatizo.
Baada ya maelezo ya Dokta Frank, ndugu Mwajombe, mwanachama wa kampuni hiyo ya Green World alielezea kuhusu bidhaa zitokanazo na mimea zinazotengenezwa na kampuni hiyo zinavyoweza kuzuia saratani hizi au kusaidia uponyaji wake.
Baada ya kipindi cha maswali na majibu, wananchi wenye matatizo walipewa fursa ya kumwona daktari huyo na kumweleza matatizo waliyokuwa nayo, ambapo walijibiwa na kupewa ushauri Bure Kabisa!
Kampuni itaendelea na mafunzo haya jumamosi ijayo ambapo wananchi wanakaribishwa kuja kwa wingi kupata mafunzo haya yanayotolewa bure kabisa.
Laurian.