SEMINA YA PILI KIBAYA-KITETO

 

Kiteto may 2017

 

 

Siku ya jumamosi ya tarehe 6 Mei 2017, semina ya pili ya kampuni ya Green World ilifanyika mjini Kibaya- Kiteto. Semina hiyo iliandaliwa na wanachama wa Green World wa mjini humo, ndugu Thomas Mpalazi na Dorcas Manyama.  Maandalizi yalifanywa kwa ustadi mkubwa na mnamo saa 9.15 za alasiri, semina ilifunguliwa na ndugu Thomas Mpalazi.

Semina hiyo iliendeshwa kwa ushirikiano na wanachama wawili waliotoka Dar Es Salaam, ndugu Laurian Mwajombe na ndugu Hilda Mahende. Semina hiyo ilizungumzia umuhimu wa kulinda afya zetu kutokana na mazingira mabaya yanayotokana na uchafuzi wa mazingira na staili mpya za maisha zinazoendana na kiwango cha sayansi na teknolojia ya sasa. Semina hiyo pia ilitoa fursa kwa wananchi wa Kiteto kujiunga na kampuni ya Green World ili waweze kuboresha vipato vyao.

Kutokana na umakini wa waliohudhuria semina hiyo na kuwa na maswali mengi ya msingi, semina hiyo iliendelea hadi saa 12.30.

 

Hilda Kiteto may2017

 

Ndugu Hilda Mahende aliwasimulia washiriki historia yake ya mafanikio aliyoyapata katika kipindi cha miaka 3 toka alipojiunga, ambapo alielezea safari  mbalimali alizozipata kutokana na kampuni ya Green World na jinsi hamu yake ya kumiliki gari binafsi ilivyobarikiwa na kampuni hii.

Semina ilikuwa na mafanikio makubwa na wananchi walipata nafasi ya kununua bidhaa walizozihitaji. Wote kwa pamoja waliwashukuru waandaaji na waendeshaji wa semina na kuwaomba kuwa wawe na moyo wa kurudi mjini hapo kwa mafunzo zaidi.

 

Laurian.