Green World Yashiriki Maonyesho Ya 12 Ya Nchi Za Afrika Mashariki

 

Moanyesho ya rock city mall mwanza

 

Kampuni ya Green World ilishiriki maonyesho ya 12 ya nchi za Afrika Mashariki yaliyofanyika katika jiji la Mwanza kwenye viwanja vya Rock City Mall. Maonyesho hayo yalianza tarehe 25 Agosti 2017 na kwisha tarehe 3 Septemba 2017. Katika maonyeshio hayo, kampuni ya Green World iliweka bidhaa zake kwenye hema namba 28.

Maelfu ya wananchi wa Mwanza walipata maelezo kuhusu bidhaa za  na fursa ya biashara ya kampuni hii. Wananchi kwa ujumla walizifurahia sana bidhaa hizo na wengi walizinunua ili wakazijaribu.

Pamoja na kununua na kupata maelezo hayo, wananchi pia walipata kujua ofisi ya kampuni hii iliyopo mtaa wa Rufiji karibu kabisa na soko la Mirongo (soko la mkulima).

 

wanachi kwenye maonyesho ya rock city mall mwanza

 

Kampuni ilitunukiwa cheti kwa kushiriki na kuonyesha bidhaa bora katika maonyesho hayo.

 

Laurian.