Wanachama Wa Green World Washiriki Maonyesho Ya 41 Ya SabaSaba

 

 

maonyesho ya sabasaba

 

Wanachama wa kampuni ya Green World wameshiriki kwenye maonyesho ya biashara ya 41 yaliyofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Dar Es Salaam.  Maonyesho hayo yalianza tarehe 28 mwezi  Juni 2017 na kuisha tarehe 13 mwezi wa Julai 2107.

Wanachama hao walionyesha bidhaa za kampuni wakiwa ndani ya hema la Benjamin Wiliam Mkapa, chumba namba 21.

Wananchi kwa mamia kila siku walipata fursa ya kuelezwa kuhusu bidhaa za kampuni na fursa ya biashara inayotolewa na kampuni hiyo. Kwa ujumla, watu walizifurahia sana bidhaa hizo na baadhi walizinunua ili wakazijaribu. Wengi pia waliipenda fursa inayotolewa na kujiorodhesha ili waanze kupewa mafunzo mara baada ya kumaliza maonyesho.

 

sabsaba 2017

Video fupi ya maonyesho ya Green World – Sabasaba

 

Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi, wanachama hao wameamua kutoa fursa kama hiyo kwa wananchi wa Mwanza kupitia maonyesho ya 12 ya nchi za Afrika Mashariki (The 12th East Africa Trade Fair 2017) yatakayofanyika kwenye viwanja vya  Rock City Mall kuanzia tarehe 25 Agosti hadi tarehe 3 Septemba 2017.

Kwa hakika hii ni nafasi ya kipekee kwa wakazi wa Mwanza.