Mkutano Wa Green World – Gold Crest Hotel Mwanza – 26 Novemba 2016.

 

Mkutano wa Green World, Gold Crest Hotel, 26 Novemba 2016

 

Kampuni ya Green World hutoa kila aina ya nyezo na mafunzo ili kumwezesha mwanachama wake kufanya kazi zake kwa urahisi na ufanisi zaidi. Mwezi Septemba 2016, kulikuwa na mfululizo wa semina zilizofanywa na mkufunzi mkuu wa kampuni hiyo, ndugu Budiman kutoka Canada, ambaye alitembelea miji ya Morogoro, Mbeya, Arusha, Dodoma na Mwanza.

Kuanzia 24 hadi 26 Novemba 2016, wanachama wawili kutoka ofisi ya Dar Es Salaam, ndugu Hilda Mahende na ndugu Laurian Mwajombe, waliendesha mafunzo katika jiji la Mwanza wakiandamana na mkufunzi wa kampuni ndugu Victor.

Tarehe 24 Novemba 2016, mafunzo yalifanyika katika hoteli ya Vizano kuanzia saa 9 alasiri, ambapo wanachama wapya walifunzwa (New Distributor Training). Siku iliyofuata, wanachama walipewa mafunzo katika hoteli hiyo hiyo yaliyolenga kuwapa mbinu za kuzianza biashara zao kwa ufanisi zaidi (Star Training).

 

Mkutano wa Gold Crest Hotel, Mwanza

Video Ya mkutano wa Green World uliofanyika Gold Crest Hotel Mwanza.

 

Mafunzo katika mji huo wa kanda ya ziwa yalihitimishwa siku ya jumamosi, tarehe 26 Novemba 2016, ambapo watu wote walikaribishwa katika ukumbi wa Mandela wa hoteli ya Gold Crest, na maelezo ya kina ya fursa ya biashara ya kampuni ya Green World yalitolewa.

Kwa ujumla, mafunzo hayo yalikuwa na mafanikio makubwa na wananchi wa mji huo walifurahishwa sana na fursa hii. Wananchi walijitokeza toka miji ya karibu ya Geita, Kwimba, Nzega, Musoma na hata Tabora. Wengi walijiunga ili waanze kubadili maisha yao kupitia fursa hii iliyo tofauti na nyingi ambazo zinatolewa hapa nchini.

Baadhi ya wananchi kutoka kampuni nyingine zinazotoa fursa za biashara walikiri kuwa hii ilikuwa fursa ya kipekee kutokana na kuwa ilikuwa na mpango rahisi wa kukua kibiashara tofauti na kampuni nyingi ambazo hutaka mwanachama kuanza kutetea upya daraja lake kila mwezi na kutoa malipo kutokana na idadi fulani tu ya vizazi vilivyo chini yao.

 

Mkutano wa Gold Crest Hotel Mwanza

 

Kikubwa zaidi ni shuhuda halisi kuhusu utendaji kazi wa bidhaa za kampuni hii na bei za bidhaa ambazo hata mwananchi wa kawaida anaweza kuzimudu, bila kusahau uhakika wa kupata bidhaa wakiwa hapo hapo mjini Mwanza na malipo yao kila mwisho wa Mwezi.

Laurian.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>