Semina Ya Budiman Mwanza – 17 Septemba 2016

 

Semina Mwanza 17 sep 2016

 

Katika mfululizo wa semina zinazofanywa na mkufunzi kutoka Toronto Canada, ndugu Budiman, moja na mabayo ilikuwa na mwamko mkubwa sana hadi sasa ni ile ambayo ilifanyika katika mji wa Mwanza katika ukumbi wa Mandela ndani ya hoteli ya Gold Crest. Semina hiyo iliyoanza saa 9 alasiri ilihudhuriwa na wanachama na wageni walioalikwa wapatao 200 na kuufanya ukumbi huo kufurika kabisa.

Katika semina hiyo, ndugu Budiman aliielezea kampuni ya Green World akianza na historia yake, mafanikio yake na mwitikio wa watu duniani kuhusu kampuni hii. Aliezea kwa ufasaha kuhusu umuhimu wa kutumia virutubishi vya kiada katika karne hii ya maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia tunayoishi na kwa nini virutubishi vya Green World ndivyo bora katiak kukidhi haja hiyo. Pia alielezea jinsi mtu mwenye ari ya kuona anabadilika katika maisha yake kiafya na kiuchumi anavyoweza kunufaika na kampuni hii.

Siku iliyofuata, tarehe 18 septemba 2016, katika ukumbi huo huo, ndugu Budiman aliendelea na semina na kutoa mafunzo ya awali ya jinsi ya kuanza biashara na kampuni hii ya Green World. Alieleza kwa nini kuwa na NDOTO ndicho kitu cha kwanza katika kuianza biashara hii. Pia alisisitiza umuhimu wa kuwa na malengo na akafundisha namna ya kuandika malengo. Akitoa mifano iliyowafurahisha wengi, aliweza kuwatia hamasa hata wale ambao walikuwa hawajajiunga na kampuni hii kujiunga mara moja. Alielezea jinsi yeye binafsi alivyokuwa na ndoto ya kuendesha gari ya kifahari aina ya BMW na kwenda kwenye yard ya magari na kuulizia kuhusu gari hilo alilolipenda – wakati huo akiwa hana pesa, na karudi nyumbani kwake na kuanza kufanya kazi kwa nguvu akiwa na wazo moja tu kichwani, la kupata gari la aina ya BMW aliloliulizia kwenye ile yard. Baada ya mwaka mmoja alipewa gari alilotaka BURE na kampuni ya Green World.

Semina hizi zinaendelea hadi tarehe 6 Oktoba siku ambayo ndugu Budiman ataondoka na kurudi kwake Canada.

 

Mafunzo ya Mwanza

VIDEO YA MAFUNZO YA BUDIMAN _ MWANZA

 

Wakazi na wanachama wa Arusha mnakumbushwa kuwa nafasi hii adimu ya kumsikiliza mkufunzi huyu wa kimataifa mtaipata siku ya tarehe 1 Oktoba 2016. Hakuna kiingilio kwenye semina hizi na hakuna ubaguzi wa kipato au elimu – NI KWA WOTE!

 

Laurian