Semina Ya Green World Tanzania, New Mwanza Hotel

 

Washiriki Wa Semine Ya Green World World New Mwanza Hotel

 

Katika siku za mwisho kabisa za mwaka 2015, wanachama wawili wa kampuni ya mtandao ya Green World Tanzania walifika mjini Mwanza na kuendesha semina kuhusu fursa ya biashara ya kampuni hiyo. Wanachama hao, ndugu Laurian Mwajombe na dada Hilda Mahende  walielekea kwenye mji huo wa kanda ya ziwa kwa mwaliko wa wanachama wapya wa kampuni hiyo, ndugu Mark Msemo na ndugu Swabuldin Katunzi.

Semina hiyo ilipangwa kufanyika jumapili ya tarehe 27 Desemba 2015 na ilianza saa 10 jioni kama ilivyopangwa katika moja ya kumbi za New Mwanza Hotel.

 

Hotoba Ya Mark Msemo New Mwanza Hotel

 

Ndugu Mark Msemo ndiye aliyefungua semina hiyo na kuendesha shughuli zote. Baada ya ufunguzi na kutoa utambulisho, Mark alimpa nafasi mwanachama mwenzake, ndugu Katunzi aweze kueleza machache, ndipo ndugu Katunzi alipoelezea kwa hisia kali jinsi asivyopenda kuona watu wakiishi maisha duni ilhali wakiwa na viungo vyote vikiwa kamili.

Ndugu Katunzi alielezea kuwa huwa anatazama na kuirudia sana video moja inayomwonyesha mtu asiye na viungo vyote muhimu vya mwili kama mikono na miguu na bado mtu huyu alijishughulisha na sasa hivi ni bilionea. Kisha huwa anajiuliza, “Iweje mtu aliye kamili awe maskini? ” Kwa mantiki hiyo, aliwashauri washiriki kuanza kubadilika kimawazo na kimatendo na kuichukua fursa hii mara moja.

Katika utambulisho, dada Hilda alisema kuwa – “kuzaliwa maskini si dhambi, ila kufa maskini!

Baada ya maneno hayo ndugu Laurian Mwajombe aliielezea kampuni ya Green World Tanzania, historia yake na mafanikio yake.

 

Mafunzo Ya Hilda Mahende Kwenye Semina Ya Green world Mwanza Hotel

 

Mwisho, Hilda Mahende aliezea mafanikio yake na wanachama wengine kutoka Afrika na nchi  za nje ambapo yeye binafsi ameweza kusafiri nchi mbalimbali zikiwemo Afrika ya Kusini, Uarabuni na China na kupata gari moja kama zawadi kutoka kwenye kampuni hii na kununua gari ya pili kutokana na kipato alichokipata kwenye kampuni hii.

Semini hii ilikuwa na mafanikio makubwa sana na wakazi wa Mwanza walionyesha shauku kubwa ya kuanza mara moja kufanya biashara na kampuni hii kwani walipoulizwa ni wangapi baina yao walipenda kujiunga na Green World, vidole vyao karibu vyote vilionekana vikiwa hewani.

Usisite kuuliza maswali au kutoa maoni yako kuhusu ripoti hii, tutafurahi sana kukujibu.

Kwa maoni au maswali jaza fomu hapa chini au tutumie barua pepe kupitia promota927@gmail.com.

 

Hujajiunga Na Kampuni Ya GREEN WORLD?

Jiunge sasa kwa kutumia moja kati ya njia hizi hapa chini:

1. Bonyeza (click) juu ya picha ya dada aliyesimama mbele ya gari iliyoko juu kabisa ya ukurasa huu upande wa kulia kisha jaza fomu itakayotokea. Ukishaituma fomu yako kwa ku-click (kubonyeza juu ya “Submit”), soma maelezo yanayofuata na sisi tutawasiliana na wewe mara moja. Usikate tamaa kama itapita siku moja au mbili, lazima tutawasiliana na wewe tu.

2. Click (Bonyeza) juu ya maneno “Jiunge Sasa” kwenye picha hii hapa chini kisha subiri. Jaza fomu itakayotokea, itume kwa kubonyeza juu ya “Submit” kisha subiri maelekezo kutoka kwetu. Uwe na subira, tutawasiliana na wewe tu.

Mawasiliano

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Jina Lako

Anuani Ya Barua Pepe

Namba Yako Ya Simu

Kichwa Cha Habari

Swali Au Maoni Yako