Kwa Nini Green World Ni Kampuni Bora Ya Mtandao Tanzania?

 

shuhuda Wa Hanisha Semfuko

VIDEO YA USHUHUDA WA HANISHA WA UBORA WA KAMPUNI YA GREEN WORLD TANZANIA

 

Hapa nchini kwetu Tanzania kuna kampuni nyingi sana za mitandao nyingine zikiwa ni za muda mrefu sana. Katika ukurasa huu nimeona niandike kuelezea ubora wa kampuni ya mtandao ya Green World ambayo kwa wengi itakuwa ndiyo mara yao ya kwanza kuisikia. Kuna watu ambao wameweza kupata manufaa makubwa kutoka kwenye kampuni hizi za mitandao na kuna wengi zaidi ambao hawakupata kitu. Hali ilivyo kwa ujumla ni kwamba sasa hivi imani ya watu wengi kuhusu biashara hizi ni kwamba si biashara za kweli.

Kuna sababu nyingi zilizopelekea watu kufikia kujenga imani hii. Kubwa kabisa katika sababu hizo ni kuwa watu wamekuwa wakiingia kwenye biashara hizi kwa mikumbo bila kuzingatia vigezo muhimu vya kuzingatia katika kuchagua kampuni za kufanya nazo biashara. Sababu nyingine ni watu kuanza kufanya biashara hizo bila kujifunza kwa makini na kuelewa mipango ya malipo (compensation plans) ya kampuni hizo. Na kadhalika, kuna sababu nyingine nyingi.#

Green World inajitenga kabisa na kampuni nyingine na kuwa ndiyo kampuni bora kwa sabuabu nyingi kama ninavyozichambua hapa chini:

Green World Ni Kampuni Ya Siku Nyingi

Moja ya sifa nzuri kwa kampuni ya mtandao ni kuweza kudumu kwenye biashara hii kwa muda mrefu na kuwa bado katika hali ya kukua kibiashara. Green World imekuwepo toka mwaka 1997 na kila siku inaongeza bidhaa mpya sokoni. Bidhaa zake zimepewa cheti cha FDA kwa miaka 7 mfululizo. Hapa kwetu Tanzania, kampuni hii imekuwa na ofisi rasmi kuanzaia mwaka 2011.

 

Green World Ina Makao Makuu Yanayoeleweka

 

Makao Makuu Ya Green World

 

Kampuni ina makao yake makuu huko Michigan – Marekani – na ina wawakilishi wa kampuni kwenye kila moja ya ofisi zake za nje zilizosambaa katika nchi zaidi ya 50 ulimwenguni.

 

Green World Ina Mpango Mzuri  Wa Malipo

Mpango Rahisi: Kampuni ya Green world imeandaa mpango wa malipo ulio rahisi kueleweka tofauti na mipango ya malipo ya kampuni nyingine za mitandao. Ni mpango wenye ngazi chache na unaoruhusu kila shughuli unayofanya katika kampuni, kukupandisha ngazi yako ya uanachama. Ni mpango ambao mtu ye yote anaweza kuuelezea kwa mtu mwingine.

Malipo Kila Mwezi: Kampuni humlipa mwanachama mafao yake kila mwezi na kwa wakati uliopangwa.

Alama  (Points) Zisizofutwa: Kampuni hutuma alama (BV) kuonyesha thamani  ya bidhaa ulizozinunua katika kampuni na ndio kipimo cha ngazi ya uanachama wako. Tofauti na kampuni nyingine, Green World hutunza rekodi ya alama hizi toka siku ulipojiunga na hazifutwi kwa sababu ya kusimama kibiashara kwa kipindi fulani. Hivyo basi, hata kama utapata dharura kwa kipindi fulani na kushindwa kununua bidhaa kutoka kwenye kampuni, utarudi na kuendelea na biashara yako kwenye ngazi na BV zako ulizoziacha. Katika kampuni hii hakuna kuteremka ngazi ila kupanda tu.

Malipo Kwa Manunuzi Binafsi: Kampuni hii inatoa mafao kwa wanachama kwa njia sita tofauti. Ni jambo la kutegemewa kuwa utalipwa mafao kutokana na mauzo ya wanachama uliowasajili lakini ni nadara kulipwa kutokana na mauzo yako binafsi kama ilivyo katika kampuni hii. Green World itakulipa bonasi kutokana na mauzo yako binafsi kwa asilimia iliyopangwa kwa ngazi. Mwanachama wa ngazi ya juu zaidi hulipwa asilimia kubwa zaidi, asilimia hizi zinazofikia 45.

Kina Cha Vizazi  Kisicho Na Ukomo: Kampuni  ya Green World ni moja ya kampuni chache sana za mtandao ambazo hutoa malipo kutokana na mauzo ya wafuasi wako wa vizazi visivyo na ukomo.

Kurithisha Biashara: Green World inamruhusu mwanachama kumrithisha biashara yake mtu ye yote aliyemchagua ili aiendeleze. Hapa ni kama mtu aliyejenga jango na kuamua kumrithisha mwanaye baada ya kuona yeye anaishiwa nguvu na kuifanya biashara hii kuwa ni kitegauchumi (asset) kama kitu kingine cho chote kile.

Bidhaa Zinazoleta Matokeo: Bidhaa za kampuni hufanya kazi ya kusafisha mwili (kutoa sumu), kuurudishia mwili virutubisho na kufanya uponyaji.

 

dawa ya Vig Power

 

 

Bidhaa za kampuni hii zinaleta matokeo makubwa sana hivi kwamba kila umponyapo mgonjwa sifa zake hueneo na kukufanya watu wengine wakutafute ili nao waweze kutibiwa.

Bidhaa Za Bei Nafuu: Bidhaa za kampuni zimepangiwa bei ambazo hata mwananchi wa kwaida anaweza kuzimudu hivyo kukusaidia wewe mwanachama kupata mauzo makubwa.

Kupata maelezo azidi kuhsu kampuni ya Green World Tanzania soma ukurasa wa “Kampuni ya Green World Tanzania“. Ukipenda kujiunga na kampuni hii jaza fomu kwenye ukurasa wa “Karibu Green Workd Tanzania“.

 

Jisikie huru kutoa maoni yako au kuuliza maswali kuhusu mada hii.

 

Laurian.

One thought on “Kwa Nini Green World Ni Kampuni Bora Ya Mtandao Tanzania?”

Leave a Reply

Your email address will not be published.

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>